Wapendwa,
napenda nieleze wanajamii wote jinsi mimi binafsi nilivyofurahishwa na taarifa za kupatikana kwa mtoto Mbarouk. Kwa kweli nilikuwa nimeumia roho sana baada ya kupata taarifa za kupotea kwa kijana huyu kwa kuzingatia kuwa siku hizi dunia imeharibika kimaadili, utu hakuna, huruma ndiyo imetoweka kabisaaaa.
Hongereni wazazi na poleni kwa mshikemshike uliowakumba ndani ya siku hizi chache ,pasipo kuwasahau wote waliofanikisha kupatikana kwa kijana huyu.
Ushauri wa bure jitahidini kumshirikisha MUNGU kwa kumshukuru kwa muujiza aliowatendea.
Ni mimi,
mdau Mbwambo J
Friday, January 30, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Tanzanian Shilling Converter
0 comments:
Post a Comment