Subscribe:

Friday, January 30, 2009

Kwa Wanaoijua Iringa: Wapi Hapa?


Reactions::

12 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli naomba tu niwe nje ya topic. Kwa kweli mimi hapo sijui ni wapi.. ila kilichonifanya nishindwe kuvumilia, ni huo mpango mji... du.. hivi hao maafisa mipango wa miji kazi yao ni nini????

Anonymous said...

Hapo kwa kweli Mwenyekiti,Sasa sijui tuite nin? manake hakuna mpangilio wowote wa ramani, ilimradi kila mtu akipata nafasi anajenga, itakua uelewi unaingia wapi wala unatoka wapi! kwa mstakhabali huu, baada ya miaka zinakua slums,Africa sasa itakua baade inaongoza kwa kuwa na slums nyingi ulimwenguni

Anonymous said...

Serikali ikianzisha bomoa boma ili kuweka barabara nayo inazua jambo!

Anonymous said...

Hapo ndugu yangu Mjengwa ni maeneo ya Ilala na kule mbele kunako onekana kama unapanda mlima ni Frelimo.

Anonymous said...

Mwenyekiti ameuliza swali hapo wapi? Waswahili wanaanza kasoro zao, jamani hamuelewi swali? Tukiwapa kazi ya mipango mji mtafanya vizuri au majungu yenu tu? Waswahili bwana.....

Anonymous said...

Hapo ni Kihesa,kushoto mwa picha mbele kny uwazi ni sehemu ya Iringa girls Secondary School,juu kny kona ya kulia hiyo barabara inaelekea Mtwivila na katikati ya picha hiyo barabara inaitwa Dodoma(Dodoma Rd) inaelekea Kihesa kilolo,Isimani,Mtera mpaka Dodoma.Inanikumbusha pia mgahawa mmoja ulikuwa unaitwa Vantella Inn sijui bado upo.
Mdau Birmingham

Mdau, Dfw said...

Mwenyekiti,
Baada ya kufikicha sana macho, hatimae nimepata jibu kwamba hapo ni maeneo ya Kihesa. Kwa wenyeji wa Isoka, Mwangata na Kihodombi kama mimi inakuwa vigumu sana kuitambua picha hiyo.

Anonymous said...

Hapo ni Kabla hujafika kihesa ,hicho kinjia kinachoonekana kwa juu ni njia ya kwenda Tumaini university na hiyo shule ya msingi inayoonekana ni kichangani

Mliakuvana said...

Sijapatambua hapo ni wapi. Kuhusu mipango miji - inasemekana mji wa Iringa hauna squatters, na ni mmoja wa miji iliyijengwa kwa kufuata mitaa, kama Tanga. Picha hii lakini haionyeshi hiyo - labda utupigie picha zingine zitakayoonyesha hii.

Iringa mitaa ni mirefu na wanyalukolo wamejenga jiwe hadi jiwe ya viwanja vyao, nyumba wanaziita "lipaala", yaani nyumba inakuwa na sehemu mbili zilizotenganishwa na ua.

Kwetu bwana!!

Anonymous said...

Hapa ni mafifi nini? Ninakubali Mliakuvana. Sehemu kubwa ya Iringa imejengwa kwa mpango. Sema ni mji wa zamani sana. Kama ulivosema , labda tunahitaji picha nyingine,maana hiki ni kitongoji tu na si sehemu kuba ya mji. Maana nijuavyo mimi Dar imejengwa ovyo kwa mpangilio kuliko hata Iringa. Nilishaenda Keko ndani ya mitaa, nikakuta naishia chooni kwa mtu. Nikaanza kurudi kama dakika 10 nyuma ndipo nipate njia nyingine tena. Hadi uwe mwenyeji.
Mdau wa blogu

Anonymous said...

Mwenekiti hapo hiyo barabara inaenda mafifi,kulia ni shule ya wasichana Iringa,ukishuka chini hapo kwenye makutano barabara ya kulia inaenda kanisa katoliki..Kreluu mpaka Gangilonga..kushoto inaenda msikitini,ngome mpaka kwa semtema.na hiyo barabara ya mafifi ukinyoosha juu kuna kanisa la walokole..inatosha.

Anonymous said...

Hapo ni ni kihesa ,hicho kinjia kinachoonekana ni cha kwenda Tumaini University

Post a Comment