
· E bwana hapa ni kitanzini! Mjengwa unaweza kutupa asili ya hilo jina la Kitanzini?
Mwenzetu huyo hapo juu ametaka kujua zaidi ya kihistoria kuhusu Kitanzini, Iringa. Tuliwahi kuelezea maana ya Kitanzini huko nyuma, lakini si vibaya tukarudia. Pichani Mzee Nzowa bado anakumbuka mahala hasa uliposimama mti uliotumika na Wajerumani kuwanyongea Wahehe. Mahala hapo palijulikana kama Kitanzini.
Aliyefikishwa hapo alifungwa kitanzi shingoni na kuning'inizwa hadi kifo. Utotoni Mzee Nzowa alikua akiuona mti huo ingawa watu hawakuendelea kunyongwa hapo baada ya Mwingereza kuingia nchini. Mti huo wa kihistoria anadhani ulikatwa miaka ya 50 wakati wa kutengeneza barabara za mitaa. Hadi hii leo eneo hili linajulikana kama Kitanzini. Kwenye nchi za wenzetu wangeweka haraka mnara wa kumbukumbu ili kuitunza historia kwa vizazi vijavyo.




Tanzanian Shilling Converter
1 comments:
Kumbe ndio maana wahehe wengi hupenda kujinyonga kwa kujitundika kwenye kitanzi kwenye miti.
Kumbe shetani pepo la kujinyonga liliwavamia wahehe toka hapo kitanzini.Walokole wapelekwe haraka wakakemee eneo hilo katika jina la Yesu mapepo ya kujinyonga yawatoke wahehe wote akiwemo Majid Mjengwa.
Post a Comment