Subscribe:

Monday, January 26, 2009

Mama Na Mwana

Kilolo, Iringa.
Reactions::

2 comments:

sara said...

Mwenyekiti na hiyo ndio nyumba wanayoishi? au ni kibanda tu cha pembeni?

Anonymous said...

Hi Maggid,
Picha ni nzuri sana, nimefurahi na kusikitika kuona picha hii. nimefurahi kumuona mama ambae bado ni msichana mbichi akimnyonyesha mtoto wake, wote wawili wanaonekana ni wenye afya. Siwezi kushangaa kwani vyakula wanavyokula vitakuwa ni fresh kutoka shamba pia havijaweka kemilali ya kukuzia au kuhifadhia. Swala la kunyonyesha watoto maziwa ya mama ni muhimu sana kwa maisha ya mwanzo ya binadamu.

Nimesikitika kuona hali ya nyumba wanayoishi, hii ni hatari kwa wanyama na wadudu kama vile panya, nyoka, mbu, inzi nk. kuingia ndani ya nyumba na kuhatarisha afya na maisha ya wakaaji.

Kuna wakati nilifanya research ya mafanikio na matatizo yanayolipata shirika la afya duniani (WHO) katika kuboresha hali ya afya kwa wananchi wa nchi zinazoendelea. Niliwahoji maofisa wa shirika hilo na majibu waliyonipa ni kuwa kama kila mkazi wa nchi hizi angekuwa na nyuma boroa zenye madirisha
yenye wavu wa mbu, ceiling board (samahani nimeazia lugha) basi wangeweza kutokomeza malaria lakini kwa hali ya sasa wanapopuliza dawa mbu hujificha kwenye nyufa na kuvuta hewa safi kutoka njem, baada ya dawa kupungua makali huwa wanarudi ndani.

Maisha bora kwa kila mtanzania inaelekea bado ni safari ndefu.

Muugwana.

Post a Comment