Subscribe:

Friday, January 30, 2009

MWANAFUNZI ALIYEPOTEA TANGA APATIKANA


Ndugu zangu katika jamii,

Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, familia ya mtoto Mbarouk H. Massoud ambaye alitoweka nyumbani kwao huko Mikanjuni, Tanga tokea jumatatu 26/1/2009 bila taarifa yoyote, inayo furaha ya kuwajulisha kuwa mtoto wetu amepatikana huko Dar jana alhamisi 29/1/2009 akiwa salama.

Bado hatujajua sababu za mtoto wetu kuondoka bila kuaga na hilo tunalifanyia kazi kifamilia. Tunashukuru kwa msaada mkubwa tulioupata kutoka kwa ndugu,wadau, marafiki,jamaa na taasisi mbalimbali walioshiriki katika kumtafuta mtoto wetu bila kuchoka hadi alipopatikana.
Kwa ujumla wenu nyote tunawashukuru na kuwatakia mafanikio makubwa katika maisha yenu ya kila siku. Shukrani za pekee kwa wanablog na vyombo vya habari vifuatavyo:

Issa Michuzi
Maggid Mjengwa
Michuzi Jr
Haki Ngowi
Tanga TV ITV
Mwambao Radio

Asanteni sana.
Massoud Hamim,
Mzazi wa Mbarouk
Reactions::

0 comments:

Post a Comment