Subscribe:

Tuesday, January 27, 2009

Uhaba Wa Maji Chuoni Ilula Sasa Ni Historia



Hatimaye kero ya muda mrefu ya maji katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ilula sasa imekwisha na kubaki kuwa historia. Ule mradi wa ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji ya kuvuna kutokana na mvua umekamilika. Ni mradi uliofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Forum Syd la nchini Sweden. Nami nilishiriki kupanga na kuratibu mradi huo.
Itakumbukwa Novemba 2007 DC wa Kilolo, Iringa Dr Athuman Mfutakamba( mwenye suti nyeusi pichani ) alifika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ilula kuubariki mradi huo wa kuvuna maji ya mvua.
Tunavyozungumza, ujenzi wa matanki mawili yenye uzajo wa lita 48,000 kwa pamoja umeshakamilika. Hivi sasa wanafunzi na baadhi ya wanakijiji wanatumia maji hayo.
Ilula ni moja ya maeneo ya wilaya ya Kilolo, Iringa yenye uhaba mkubwa wa maji.
Mradi huu haukugharimu ' mamia ya mamilioni!' kwa vile nguvu kazi ya wanachuo na utaalamu wa walimu wa ufundi ulisaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za ujenzi wa matanki hayo.
Reactions::

3 comments:

Anonymous said...

mwenyekiti,
mbona nasikia maji ya mvua huharibika haraka sana---sasa hapo ilula wanafanya vipi ili kuzuia uharibikaji huo. N nikichekesho Ilula kuwa na uhaba wa maji wakati mto Ruaha unakatiza hapo---ni sawa na Shinyanga kuwa na ukame wakati ziwa Victoria limetulia kwa pembeni.--kwanza mzee vipi? ma pingesi yamekwisha ingia town?

Anonymous said...

Wahehe wengi wakiwemo wa Ilula wamelaaniwa hawapendi kukaa karibu na mito.Wengi wanakaa mbali sana na mito ilipo.Wanayakimbia maji.Mtu ukiona ankaa mbali na maji yaliko ujue huyo kalaaniwa.

Hata serikali inajua MAJI NI UHAI sasa mtu utakaaje eneo lisilokuwa na maji? liwe mjini au kijijini.

Nilihama Kigogo Dar es salaam baada ya kujua ni eneo lililolaaniwa ambalo halina maji ya Bomba wala visima nikatoroka.Watu wengi Dar es salaam wanaishi maeneo yaliyolaaniwa maana hayana maji.Halafu eti wanajiita wakazi wa Dar es salaam.

Hata kule Mwananyamala kwenu Mjengwa kumelaaniwa hakuna maji ya bomba kule.Uhame na wakwezo.

Anonymous said...

Mzee wa kulaaniwa umenichekesha sana---kwahiyo inamaana wahehe wote wamelaaniwa--na je watu wa central line--dodoma--singida--shinyanga---mzee na dhani ni swala la miundo mbinu---huyu kiwete na serikali yake ndio wajinga--na hasa CCM wote--kwani wameoongoza nchi for so many years lakini hakuna kitu. Tunachoona ni majumba yao makubwa, wototo wao wakienda kusoma ulaya na marekani huku kila likizo wakirudi home wakati wengine ilibidi tukamue mavi. magari ya kifahari wakiendesha kwa fujo mjini ukiwakwangua wanashuka na bastola---serikali ya CCM naona ndio iliolaaniwa na wala sio wananchi-----fikiria pesa yote iloibiwa si ingitosha kusambaza maji hapo ilula----na je mzee jiulize--mkapa angekuwa na nyumba hapo ilula si ingekuwa na maji----

Post a Comment