Subscribe:

Thursday, February 26, 2009

HONGERA SANA STARS YETU!!

Ni kwa ushindi wa kutia matumaini dhidi ya Ivory Coast.
Reactions::

7 comments:

Anonymous said...

JK BOYS OYEEEEEEEEEEE.
HAKIM

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mwanafunzi wangu mmoja kutoka Misri amenipigia kunipa hongera. Nilipomuuliza hongera ya nini akasema timu ya Tanzania imeshinda. Basi na mimi nikaanza kujimwambafai na kujidai. Ushindi huu basi uwe ni taswira na ushahidi wa kupanda kwa kiwango chetu cha soka na siyo (kama tunavyosema sisi washabiki wa masumbwi) one punch wonder.

Anonymous said...

Ikifungwa mechi inayokuja itaitwa Taifa Stars ya Maximo!!!
Watanzania bwana, kwa unafiki ni maprofesa.

Anonymous said...

We mdau wa tatu, mnafiki mwenyewe! Umejuaje kama Watanzania ni maprofesa wa unafiki kama wewe sio mwenyekiti wao?

Anonymous said...

Watanzania wanafiki sana, Jana ungesikia kipindi cha michezo cha radio one asubuhihizo msg zilizokuwa zinatumwa kumnanga Maximo ungesikitika, na kuna mtu anaitwa SAPI alimuongelea Maximo in a negative way as if hakuna zuri alilofanya tangu aichukue timu. Inasikitisha. Taifa Stars ikifungwa kashfa na dharau kibao kwa Maximo lakini ikifunga Maximo hatajwi kabisa. Watanzania tujirekebishe, tuache dharau, tuache na UNAFIKI PIA. WE HAVE TO BE PATIENT.

Anonymous said...

Nakubaliana nawe ann#3
Kweli stars ikishinda yetu..ikishindwa ya maximo. Mi nashindwa kuelewa ni kwanini tunakuwa na tabia hii ya kichawi? Hasa hao akina mziray ni ma-ndumila kuwili

Anonymous said...

Unafiki ni kama huu.. baada ya kufungwa mechi ya kwanza

Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
Na Mwandishi Wetu

MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.


Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.


Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.


“Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.


“Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba.


“Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu...,” alisema.


Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: “Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena,” alisema.

Post a Comment