
Kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Singida Bw. Mlade. Kulia ni Bw. Kimweri ambaye alipata kuwa mkuu wa FDC ya Msingi, Iramba Mashariki. Kwa sasa Kimweri ni diwani wa kata ya Msingi (CCM). Mwezi Julai mwaka 1991, kwa mwezi mmoja nilishiriki kwa kujitolea ujenzi wa shule ya msingi ya kijiji cha Msingi ambapo pia ndipo kilipo Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Msingi. Jana nilipata tena bahati ya kutembelea kata ya Msingi, Iramba Mashariki. Nilifika Chuoni Msingi pia na kuongea na wakufunzi na washiriki wa kozi. Kata ya Msingi sasa ina Sekondari pia.




Tanzanian Shilling Converter
2 comments:
Ulipiga picha daraja pale mtoni (Msingi). Nilifika ktk daraja hilo mwaka 1994, ni daraja la kisasa kabisa!
nimeipenda sana hiyo nyumba. ni safi na imejengwa kwa kuzingatia viwango.
Post a Comment