taifa stars na senegal leo huko ivory coast
Na Florian Kaijage, Abidjan
Taifa Stars leo inashuka katika dimba la Felix Houphet Boigny jijini hapa kuwakabiri Simba wa Teranga, Senegal katika mchezo wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan) huku ikizungukwa na hisia za kulipa kisasi kwa Taifa Stars.
Mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya pili ikitanguliwa na ya ile ya ufunguzi kati ya wenyeji Ivory Coast na Zambia itachezwa saa moja usiku kwa saa za hapa sawa na saa nne za usiku za Afrika Mashariki.
Ni kisasi kwa hasa kwa Taifa Stars kwa sababu March 24, 2007 Stars ilichapwa mabao 4-0 mjini Dakar wakati wa kampeni za kufuzu kwa fainali za Afrika zilizofanyika 2008 huko Ghana na katika mchezo wa marejeanp jijini Mwanza Stars iliwakosa Senegal kwa kulazimishwa sare ya 1-1 Juni 2 2007 jijini Mwanza. Nizar Khalfan alifunga bao la dakika ya 17 lakini Demba Ba akaisawazishia Senegal zikisalia dakika 17 mpira kumalizika. Mbele ya mashabiki zaidi ya 20,000 akiwemo Rais Jakaaya Kikwete.
Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha Stars walioshiriki michezo hiyo miwili bado wapo kama vile Shadrack Nsajigwa, Salum Swed, Nizar, Haruna Moshi, Athuman Idd Shabaan Nditi, Henry Joseph toufauti na Senegal ambayo wachezaji we ngi wa kikosi cha kwanza wanasakata kandanda barani Ulaya.
Na ifahamike kuwa hicho kipigo cha mabao 4-0 ndicho kikubwa zaidi kwa Stars tangu Maximo aanze kibaru cha kuinoa timu hiyo Agosti 2006.
Hata hivyo Stars inashuka dimbani bila viungo wake wawili Athumani Idd ambaye Maximo anasema hayuko fiti asilimia 100 na Kigi Makasi mwenye kadi mbili za njano huku Godfrey Bonny ambaye alikuwa akisumbuliwa na tumbo akianza, inatarajia kushuka ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi.
Stars ilikuwa ya kwanza kutua katika mji wa Abidjan kwa fainali hizo za kwanza na wachezaji wake wameonesha kuwa na ari ya mchezo hasa kutokana na mazoezi waliyoyafanya wakichekelea hali ya hewa inayofana na ya Dar es salaam kutoka na nyuzi nyoto kufikia sentigrade 29.
Mbrazili Maximo alisema:’kushinda mchezo wa kwanza ni muhimu mno ili kupandisha ari na hamasa ambayo tayari iko juu miongoni mwa wachezaji wangu’.
‘Tanzania sasa inaapanda kufanikiwa kushiriki mashindano makubwa baada ya miaka 29 kieleelzo kuwa nchi iko katika mwelekeo wa kuwa moja ya miamba ya soka sote tinawajibika kuonesha kuwa kufuzu kwetu kwa fainali hizi haikutokea kwa bahati bali kazi kubwa ilifanyika’ alisema Maximo ambaye meci ya leo itakuwa ni 42 kwake kuongoza timu ya Taifa.
Kulingana na mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika tangu timu kuwasili hapa Abidjan ukiondoa wachezaji ambao hawawezi kushiriki mchezo wa leo ni dhahiri kuwa kikosi kitakuwa kama ifuatavyo:
Shaaban Dihile, Nsajigwa, Juma Jabu, Swed, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Geofrey Bonny, Henry Joseph Nizar, Haruna, Jerson Tegete na Mrisho Ngasa.
Mchezaji chipukizi Mwinyi Kazimoto aliyevaa jezi ya Stars kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Zimbabwe anatarajia kuwapo katika benchi la wachezaji wa akiba pamoja na Deo Munishi, Kevin Yondani Nurdin Bakari Mussa Hassan Mgosi, Abdi Kassim na Amir Maftah.




Tanzanian Shilling Converter
0 comments:
Post a Comment