Subscribe:

Saturday, February 28, 2009

Kero Ya Maji: Jamani Wahandisi Tukae Chini...

Mjengwa,

Asante kwa kuteletea picha humu kijiji. Jamani Wahandisi tukae chini tufikiri jinsi ya kupunguza kero hii. Mnaonaje tukianzisha michango kwaajii ya kutatua kero. Mbona harambee za harusi zinafanikiwa tutashindwa kero za jamii? Jamani tufikiri hili kwa makini.Naimani kabisa tunaweza tukilitole macho.

Mdau Pacific Northwest

(samahani usitoe email yangu)
Reactions::

1 comments:

Anonymous said...

Cha kufanya ni kuwa na campaign ya kukusanya watu ili wasaign ya kutuma Ikulu.

Sababu inayo nifanya niseme hivyo ni kuwa watafuti wa mafuta wa Norway waligundua maji mengi ya chem chem (under ground)Rufiji yanayo weza kutosheleza mahitaji kwa nchi nzima hata nchi jirani wakati wanafanya utafiti wa mafuta miaka mitatu iliyopita.

Wataalamu hao walisema kuwa resource ya maji ilikuwa hata na thamani kubwa kuliko mafuta ukizingatia kuwa maji yamekuwa tatizo kubwa duniani kiasi kwamba UN inasema kuwa vita vijavyo vitakuwa ni vya kugombania maji.

Waliwasilisha habari hizi kwa JK na walikuwa wako tayari kuanza mradi wa kusambaza maji Tanzania nzima na hata kuiwezesha nchi yetu ku export hayo maji.

Cha kushangaza wameisha kutana na JK mara nyingi kuhusu swali hili wala haonyeshi nia. Na sasa wanaanza kungumzia kutafuta means zingine kupitia nchi jirani ili waweze ku pump maji kutoka kwetu.

Kinacho sikitisha ni kuona kwamba viongozi wetu hawajali afya na maendeleo ya wananchi. Maji ni mwamzo wa maendeleo ya nchi ukizingatia kwamba jamii ikiwa na maji safi hata infectious diseases zitapungua, muda wa wanawake na watoto wanaotumia kwenda kutafuta maji utapunguzwa kwa kiasi kikubwa na badala yake utatumiwa kwa kujenga taifa au kufanya homework na uchafu wa mazingira utapungua ukizingatia kuwa kutakuwa na maji ya kutosha kusafisha mazingira yetu.

Hivyo inabidi tuandike barua ya wazi kwa Kiwete na kumuuliza ana mipango gani na uendelezaji wa mradi wa maji? Ingawa siishi Tanzania, lakini nina mashaka hata kama hizi habari za ugunduaji wa maji umeisha nenwa kwenye vyombo vyetu vya habari.

SASA NI MUDA WA KUIJULISHA SERIKALI KWAMBA HIZI HABARI TUNAZO NA TUNA DEMAND EXPLANATION NA PIA ACTION!!!!

Post a Comment