Subscribe:

Sunday, February 22, 2009

Kijiwe Cha Kahawa Kondoa


Nimefika Kondoa jioni hii. Kondoa imetulia. Nimepata nafasi ya kutembea mitaa ya Kondoa ikiwa ni pamoja na kukaa na kupiga gumzo na wenyeji kwenye moja ya vijiwe vya kahawa karibu na stendi kuu ya mabasi.
Reactions::

12 comments:

Mbele said...

Shukrani sana kwa taarifa za Kondoa. Sijawahi kufika huko, na kila unaloweka hapa lina umuhimu sana kwangu, kwani ninapangia kuja na wanafunzi Wamarekani miezi ya karibuni, kwenye kozi ambayo nimeielezea hapa. Nimeona niseme hivyo, kwa uwazi na ukweli, ufahamu ni jinsi gani unawafaidia wanadamu wenzako kwa yale unayofanya. Mungu azidi akubariki.

Anonymous said...

Mwenyekiti!!! wee ni mtu wa kawaida! usie hata na mamabo ya kujiona. Manake kuna watu wengine atakwambia mimi sina hadhi ya kukaa hapo, binadam wengine akipata kidogo wee si kuzalau wenzie acha! wengine mpaka wazazi wao wanawadhalau.

Anonymous said...

Mzee hiyo Bakiti na Jeans vipi? au unazo nyingi? sababu kila picha mzee nakuona kwenye hivyo hivyo,

Anonymous said...

mjengwa nimekukubali unajua kujimix,nitazidi kuisoma sana hii blog yako kwavile najua itakuwa ina ladha mchanganyiko kutoka matabaka yote,hivi vp ukiwadadisi watu wa mpwapwa,kondoana sehemu mbalimbali unazozitembelea wanaichukuliaje hii serikali yetu ya mafisadi???nadhani utakuwa unapata faida nyingi sana kuona watu walivyo na mitazamo na upeo tofauti duniani hapa.sidhani hata kondoa wanaoisoma hii blog au mpwapwa kama wanafikawatu watano....lol

Anonymous said...

Mw/kiti ukiwa safarini kama hivi nani anakupiga picha?maana naona nae aniweza sana fani..
kwa mara nyingine tunashukuru kwa kutuwekea habari na picha za mikoani kwa ni wote wamekazania mjini peke yake wanasahau kuwa Tanzania yetu kubwa sana.mi nimekulia mikoani maisha yangu yote na mikoani kuna raha yake tofauti kabisa na sehemu kama Dar...
Mdau
Thessaloniki

Anonymous said...

lazima nirudi kijijini nikitoka ulaya ,wewe mbona unaishi na naona unainjoi kuliko wa mjini.poa kaka, tafuta safari ya magharibi katuletee na picha za huko.
safi sana m/kiti.unapenda udingi,unamiaka mingapi kwani chairman.

Anonymous said...

Thank you sana kwa ku posti hizo picha za Kondoa, Mwapapa, Bukoba na kadhalika Keep up the good job! I wish i could share your Kahawa my friend...

Anonymous said...

Kweli Mwenyekiti mashati hayo yanauzwa wapi?

Anonymous said...

Kaka hapo kondoa kama ndo umefika jioni hii ya leo,jitahidi upate KUKU WA KIENYEJI.
Kuna kuku wengi sana hapo wa kienyeji.Usinywe kahawa tu kavukavu,Hapo sifa yake ni kuku wa kienyeji.Unaweza ukjikuta umekaa mwezi mzima hapo usipoangalia.Kuku bwana,kuku hapo nduguyangu,tena wa kienyeji.

MDAU,UGHAIBUNI.

Anonymous said...

Hapo ndugu Mjengwa umenitembeza na kunionesha mazingira yafananayo na nilikokulia, isipokuwa tu hakuna kunywa GAHAWA ila uji wa ulezi na togwa!!
Kondoa hapo utapata asali safi, mbuzi choma, kuku tena wa kienyeji, karanga, mahindi, je na wale ndege wa kuchomwa uelekeapo Kondoa? hakika raha sana! Pamoja na vyote hivyo kuzalishwa na wenyeji, lakini bado ni maskini kwa kuwa hawajaunganishwa vema kwenye masoko ili nguvu zao ziwalipe kwa manufaa mapana zaidi.
Nikutakie safari njema, ila waweza tafuta shamba ukalima japo alizeti ili SAMMA ikifanikiwa kuwe na alternative kibaoooo!

Mdau Oslo, Norway

Anonymous said...

Maggid kwa vijiwe vya waze!

Kweli wewe ni mtu wa kujimixi

Naona unapata hekima za wazee.

Anonymous said...

du aksante sana umenikumbusha nyumbani kondoa,kwa nyuma hapo kuna sehemu kuna kuku wakienyeji wa kuchoma,maarufu kama kwa muksen...

mdau-university of johannesburg

Post a Comment