Subscribe:

Sunday, February 22, 2009

Kondoa Hapa


Habari kubwa hapa Kondoa hii leo ni tukio la jaribio la majambazi kuliteka basi la Machame Investiment kwenye pori la Mtunguti barabara ya Dodoma- Arusha. Ilikuwa jana asubuhi majira ya saa moja. Kwa kawaida mabasi yanayopita pori hilo yanasindikizwa na askari. Katika tukio hilo zilipigwa risasi tisa na dereva wa basi alijeruhiwa mkono wa kulia kwa risasi. Hata hivyo, kwa ujasiri mkubwa dereva huyo aliweza kuendesha basi hilo kwa kuvuka mawe yaliyopangwa barabarani. Leo majira ya saa nane nilipita kwenye kizuizi cha askari kuingia pori hilo. Hapo nilipata kwa mara ya kwanza taarifa ya tukio hilo. Askari yule niliyemkuta kwenye kizuizi alionekana hakuwa tayari kusindikiza gari nililoendesha bila kupewa chochote. Badala yake alinidanganya kuwa kuna msafara wa magari matatu na basi moja uliondoka kwenye kizuizi hicho dakika tano zilizopita na kwamba ningeweza kabisa kuwawahi. Kumbe, hakukuwa na kitu kama hicho. Kwa bahati niliweza kuvuka pori hilo salama ingawa nilijawa na mashaka makubwa.
Reactions::

2 comments:

Anonymous said...

pole sana mwenyekiti ,miminilishawahi kuandika comments hapa kuwa naona raha sana askari akipata kichapo kwavile askri wengi wa bongo ndio haohao majambazi,na sijui ni kwanini watu wengine hawalioni hilo????mfano mzuri fuatilieni kesi ya aliekuwa kamanda wa upelelezi wa mkoa nyeti kama daresalaam ZOMBE hao ndio asilimia 80 ya askari wetu.mungu ibariki tanzania.

Anonymous said...

yaani Mwenyekiti unatupeleka TANZANIA yote kwa picha! manake ukiona picha, unapata picha harisi ya maeneo ya hapo.Mwenyekiti wewe ni mchapa kazi kweli, ndio invyotakiwa na Taifa linapata kuendelea, kama hapo umesha wabarisha wasiojua ni sehemu mbaya inayosumbuliwa na watu wenye kutaka kukwapua vya wenzao bila kuvitolea jasho, maanake ni watu hatari hao, kiasi kwamba hata mnyama ana afadhali,sasa serikari ni jukumu lake la kuakikisha watu hatari wanasafishwa kwa kuwa hawafai katika jamii, mpaka watapokua na moyo ya kibinadam. ya kuacha kusumbua wenzao,na kutafuta njia kwa njia iliyo harali, bila kumkwapulia mwenzio.

Post a Comment