Subscribe:

Sunday, February 22, 2009

Kuijenga Nchi Yetu Ni Jukumu Letu Wenyewe




Watanzania tumeanza kujijengea mazoea ya kunung'unika. Jana nikiwa njiani kwenda Chisalu niliguswa sana na kitendo cha akina mama watano niliowakuta wakijitolea kufukia mashimo ya barabara inayopita kijijini kwao. Kwao ilikuwa ni kazi ya maendeleo katika siku ya Jumamosi. Wamelitambua jukumu lao, wamelichukua bila kusimamiwa na mtu yeyote. Tukipunguza kunung'unika na kuanza kuchukua hatua katika maeneo yanayotuzunguka, basi, tunaweza kupiga hatua za maana za maendeleo.
Reactions::

4 comments:

Anonymous said...

Mjengwa asante sana kwa kutubandikia picha za mandhari ya Dom na Mpwapwa. Sisi vijana wa zamani tunakumbuka miaka ya sitini na sabini huko vijijini kila m'kiti wa nyumba kumikumi alikuwa na jukumu la kuhamasisha kaya zake kwenda kujitolea kusafisha vyanzo vya maji ya kula, kutengeneza njia za kwenda mitoni na marishoni, na hata kubeba matofali au mawe ya kujengea shule au zahanati. Watu walifanya kwa moyo mkunjufu kwa sababu walitambua na kuona matunda yake!! Hizo zilikuwa zinaitwa enzi za 'ujamaa na kujitegemea'. Mabepari wa kimataifa hawakupendezwa na hilo na wakatulazimisha tuzike ujamaa na kujitegemea na tukumbatie sijui niite 'utajirisho na utegemezi'. Walioko madarakani kuanzia vijijini hadi taifa wakaanza kutekeleza hiyo itikadi kwa kupwaua fedha za walipa kodi kadri wanavyoweza (kesi hizo zilizo Kisutu ni ushahidi wa wazi)!! Sasa utaanzia wapi kumuhamasisha mlalahoi akajitolee kubeba tofali la shule wakati hela anayolipa kodi inaliwa na AKINA HAO!! Tuko njia panda!!!!!

Anonymous said...

Na hao wa mijini lau kama wangechangia kusafisha miji yetu wakati wa sasa kuyumba kwa uchumi!

Anonymous said...

asante sana kaka mjengwa kutuonesha sehemu mbali mbali za nchi yetu. namna hii tutaweza kufahamu jinsi nchi yetu ilivyo. kwakweli kuna kazi ngumu kuiendeleza tanzania. mara nyingi tunaona picha za miji tu na kumbe sehemu nyingi watu wanaishi kwa shida sana.

Anonymous said...

huyu jamaa wa kwanza, inaonekana haelewi kuwa enzi za ujamaa/nyerere pesa za wananchi zilikuwa zinachotwa pia, kwa mfano ATC augustine mwingira,mustafa nyang'anyi,cleopa msuya, hembu tuache kulaumu wazungu!!!! reli ya mjerumani ndiyo inapeleka mafuta mwanza mpaka leo.

Post a Comment