Subscribe:

Monday, February 23, 2009

Mama Na Mwana!


Ndoroboni, Kwa Mtoro, Kondoa.
Reactions::

9 comments:

Anonymous said...

Nimeipenda sana hii picha mwenyekiti, je unazo nyingine za huyu mama na mwanae?

Kilichonivutia zaidi ni hiyo mbeleko yake aliyombebea mtoto nzuri sana imenivutia, na mtoto mwenyewe mzurii!!!! pia msafiii!!! nimewapenda sana kwakweli.

Ombi naweza kuitumia hii picha?......please!

Jiang said...

Mambo, za Kondoa,
Jiang hapa nimeiiba hii picha, na ile ya mtoto anayecheza golf nataka nizitumie kesho. Nimeattribute kuwa nimezitoa kwako, I hope it is ok.
Thanx,
Jiang.

Anonymous said...

Natural beauty. Nimependa hiyo mbeleko ya ngozi aliyombebea mwanaye. Ahsante sana mwenyekiti kwa kutuletea picha halisi za uhalisia wa maisha wa mwananchi wa kawaida wa kitanzania.
Celine

Anonymous said...

Kaka mjengwa,nakushukuru sana kwa picha nzuri za nyumbani hii ya mama na mwana nimeipenda sana,ubarikiwa sana na keep up the good job.mdau Canada.

Anonymous said...

jamani watu wa singida huyo mama naona usoni mwake kama kajitoboatoboa, inamaanisha nini hasa?
Ms GB

Anonymous said...

Mbeleko safi...ila inatakiwa kuwa na matundu matundu madogodogo kupunguza ufukutu kati ya mwili wa mtoto na wa mama!

Anonymous said...

kaka mjengwa napenda kuzuru blog yako kwa mambo haya tu,nimependa kweli picha toka milima ya nyangoro,dodoma,kwamtoro,ziwa singida,peoples club nimecheza sana mziki pale.na hayo maeneo yote nilipita sana kipindi nasoma,pia huyo mama kama ulimpiga picha kwamtoro hao kabila yao wasandawi kama sikosei na wanapoongea lafudhi yao ni kama waxhosa kutoka south africa,tulikwama hapo chini kabla hujafika kwamtoro kuna kidaraja,sikumbili kipindi cha el ninyo,do nimechukua picha zote nikamwonyeshe mke wangu maisha niliyokulia,ahsante sana.mdau stockholm

Anonymous said...

Huo urembo wa mila na desturi ya wabarabaigi kama sikosei. Ila unaelekea kuisha isha siku hizi. Naona mambo ya kisasa yanachukua nafasi zaidi ktk jamii. Siku hizi hata zile ndonya za kimakonde ni nadra kumkuta anayo. Hata chale za usoni za watani wangu Wahehe ni nadra sana kumkuta nazo mtu.

Anonymous said...

picha very very nice..inaonyesha bado tuna tradition, nimefurahi sana asahnte.

Post a Comment