Subscribe:

Friday, February 27, 2009

NIMERUDI IRINGA JIONI HII

Ni baada ya kukamata usukani tangu saa kumi na moja asubuhi leo hii nikitokea Shinyanga Mjini kupitia Tabora, Singida, Dodoma na hatimaye Mtera hadi Iringa. Nimefurahi sana kurejea nyumbani Iringa baada ya safari hii ndefu iliyonipitisha kwenye vumbi, tope, mashimo na lami. Nimeona na kujifunza mengi. Nimekutana na watu wengi wema. Na hakika, 'watani' zangu Wanyamwezi na Wasukuma ni watu wema na wakarimu mno. Sikulijua hilo hadi nilipofika Unyamwezini na Usukumani. Na wapi tena kwenye wasichana warembo kama Unyamwezini na Usukumani?Tatizo hata zizi la mbuzi sina, vinginevyo ' SAMMA' ingekuwa historia!
Reactions::

6 comments:

Anonymous said...

Pole na safari mkuu na tunashukuru kwa picha nzuri ulizotuletea za huko vijijini. Uzuri wa picha zako huwa zinalenga kwenye maisha ya mtanzania wa kijijini. Thank you

Anonymous said...

Pole sana kwa kukata hizo mbuga! Ni vizuri kusikia kuwa licha ya "vumbi, tope, mashimo" (ndio hali ya barabara zetu nyingi) uliondoka na kurudi Iringa salama u-salimini!

BAP

Anonymous said...

Hahahaa,mwenyekiti umekwenda kipindi kibaya hiki nenda baadaya mavuno, hakika Iringa hutakaa nenda kipindi cha SAGULAGA..... MWANA MBATE....hicho nikipindi ambacho hata aliyejificha uvunguni utamuona, hahahahahaaha kazi kwako mtani.

Anonymous said...

pole sana naomba siku ukipita pale ilula,mtua nenda kijiji cha luganga mbele kidogo ya kanisa la lutheran luganga ukamsalimie bibi yangu MUHAME na wanyalukolo wote

Anonymous said...

kaka mjengwa pole sana kwa safari ndefu,umejifunza mengi na sisi pia kupitia picha zako nzuri tumejifunza mengi pia, tunashukuru kwa hilo, ukienda dar pleaseeeee picha za benjamin mkapa hig school na al haramain, nataka kupaona nimepamiss sana, asante

Anonymous said...

Hongera kwa kusafiri na kurudi nyumbani salama! Ukisafiri ndani ya mikoa ya Tanzania hakika unapata mchanganyiko wa hisia, kuna wakati utafurahi kwa mandhari zuri sana za asili na wingi wa maliasili, lakini kuna wakti utahuzunika kiasi cha kutaka kulia uangaliapo makazi na miundombinu katika jamii ya Watanzania.

Angalia nyumba za tembe Dodoma na Singida zisizo ma madirisha, jiulize hali za afya za wakazi wake, jiulize vipato vyao, wana matumaini yoyote ya Tanzania yenye Neema? Ukiwa na mawazo hayo, jiulize sera mbalimbali za serikali kuhusu UWEZESHAJI, Uchangiaji katika ELIMU, AFYA na huduma nyingine za jamii. Kisha tulia usikilize majigambo ya wanasiasa na watawala wetu (sio viongozi)waweza kata tamaa au kuchukia kila mtawala kuanzia nyumba kumi hadi kileleni!

Sio rahisi kukimbilia kutaka uongozi ikiwa kweli unaguswa na hali za wananchi kama zinvyojidhihirisha katika hali duni za makazi na mazingira kwa ujumla, labda kama unataka kutawala tu! Hebu tuchague kuwekeza vya kutosha katika ELIMU na AFYA kwanza mengine yatabadilika kwa kasi tusiyotarajia ikiwemo UFISADI!

Mungu Ibariki Tanzania

Post a Comment