Subscribe:

Monday, February 23, 2009

Ubatizo Huu!

Kwenye moja ya vijiji vya njiani, Kondoa jana Jumapili.
Reactions::

13 comments:

Anonymous said...

wewe kaka mi naomba mambo ya dini we achana nayo kwani kuna mambo mengi katika jamii ya kutuonesha si dini tu.mbona haupigi picha ninyi mkiswali kwani we vile unaona ni jambo la kawaida kwa dini nyingine???? nacho pia ni kihoja kwa dini nyingine . pia ninyi mnajaziba sana ninyi mkipigwa picha kama hizo zinazo husiana na dini yenu hamchelewi kuandamana . kumbuka katuni walizo wachora mtume wenu kule dernmark.mlifanyaje ???. tena jiheshimu acha kukashifu dini ya mtu yeyote kuwa feya..hii blog haisomwi na waisilamu wenzio tu . kama umebadili imekuwa ya kukashifu ukristo zaidi sema na ujitahidi kupata picha zao.SIJAPENDA UNACHO FANYA . TENA UNAONEKANA UNA BUSARA .USIONGOZWE NA UKELELEKETWA WA DINI.CHUKI SI NZURI

Anonymous said...

Yes, this is real Biblical way of baptising; fully immersed in water.

Shimba ya Buhongo said...

Weye anony wa kwanza hapo juu hujui ulichoandika. Kwenye hiyo picha kinachoonyesha kuna suala la udini ni kitu gani? Au hata unazodai ni kashfa ni ipi hapo? Kama huna chakuandika siyo lazima ulete utumbo wako hapa. Siyo tu kwasababu unaweza kudonoa keyboard ndiyo useme ujinga wako. Ningekutukana vibaya sana ila mjengwa ataacha kufikisha ujumbe kwako mbuzi weee

Anonymous said...

Akitokea mamba au kiboko hapo! mmh mi simo!

mgogo muuza kahawa! said...

huyo anayesema kuwa unaleta chuki binafsi katika dini wala hajui anachokisema mwenyekiti,na wala hajui nini maana ya uandishi wa habari,hasa zinazohusiana na matukio halisi ya mahali pamoja na mazingira,hapa me sioni kosa kueleza na kutuonyesha tukio ambalo umekuta likiendelea mahali fulani,mbona kwenye swala za idd watu wanapiga picha? na sehemu nyingine mbalimbali,watu wamepiga picha vatican! iweje hapo singida!watu wanapiga picha hadi mecca huko,
chamsingi ni kuwa huyu anaetoa hizo porojo hapo juu naweza kumuita limbukeni(aishakum si tusi)na watu kama hawa ndio wanachomwa kama wale waliochomwa na kibwetere(walale pema peponikwakuwa na kasumba za ajabu na sizizokuwa na malengo ya kimaendeleo,namnukuu,´´nyinyi mkipigwa picha mnaandamana na kumbuka zile katuni alizochorwa mtume wenu``mwisho wa kunukuu,tafadhali jua tofauti ya kutoa taarifa (reporting)na kutoa kashfa,,na tafadhali kabla hatujatoa maoni wadau tufikirie kwanza,hapa sio kijiwe cha kihuni,hili ni baraza la kistarabu..wapi tatizo mtu kuonyesha picha ya ubatizo?unatuaibisha wakristo.alaaa!

Anonymous said...

Imeandikwa 'Enendeni ulimwenguni mwote (na kondoa imo) mkaihubiri injili kwa kila kiumbe (hata mjengwa na wewe msomaji).Aaminiye na kubatizwa(hata mtoni)ATAOKOKA'. Asiyeamini ATAHUKUMIWA.' Injili ya marko 16:15-16.
Heri kuliwa na mamba na kiboko kuliko JEHANAMU.
Mjengwa angekuwa mdini kama msimavyo wengine asingegusia kabisa issue hii. Nampongeza kwa kuwa open-minded.

Anonymous said...

anony: wapili, hakuna haja ya kumtukana m2 aliyetoa maoni yake. Huo ni mtazamo wake, mawazo yake.

hiyo picha haina kashfa wala haijataja ukristo.

Wa2 wa anony wa kwanza wapo wengi.

Tuwasamehe, kwani sote tunaelewa DINI hizi Ukristo na Uislam ni MAPOKEO TU. Wenye busara hupuuza, hawalumbani. Ukilumbana utaonekana nawe ni mdini (-)

Anonymous said...

bwana nyieeee, huyo anony wapili yuko right kabisa huko nikutuchoresha sisi wasabato na wengineo wanaotumia staili hiyo. mbona hatoi watu wakiwa wanaswali?alafu ninyi niwatu wavurugu sana hamna dogo kwani hamjijui?

Anonymous said...

mjengwa nmbona maoni yangu umeya DELETE? au ndo umeniona mimi natoa PUMBA?basi bwana kuanzia leo nimejiengua uanachama ktk familia ya blog yako.nakutakia maisha mema.IMENIUMA SANA

Anonymous said...

Mjengwa asante kwa picha hii Mungu akubariki. Unapoongelea jamii, dini ni sehemu moja wapo. Mimi nilishabatizwa kwenye maji mengi kama haya, hii ndo inavyotakiwa, hivyo nimefurahi sana kuona picha hii kwamba ubatizo unaendelea kufanyika sawa sawa na maagizo ya Biblia Takatifu. Keep it up...

Anonymous said...

picha ikiwekwa kila mtu anatafsiri anavyoona labda mwenzetu kaona vingine. kamwene mjengwa
tm

Anonymous said...

anonymous wa kwanza

Ndugu yangu, hakukuwa na sababu ya kumshutumu Maggid kuwa mdini-yeye kaweka kinachofanyika na wenye imani zao, sasa kwa nini wewe umeona hii ni kama udhalilishaji mpaka unataka ku compare na makatuni ya Mtume?

Mbona magazeti yanaweka picha za waislamu wanasali na hakuna anayelalamika, kwa nini ujisikie vibaya kwa picha ya kile amabacho unakiamini mwenye na kukifanya?

Waislamu hupigwa picha za kusali, kuhiji, kufuturu etc na hakuna hata tone ya kudhania kudhalilishwa, iweje wewe uone picha ibada zetu kuwa ni udhalilishaji. Ina maana hii picha imekufanya uone hii ni kejeli?

Ps be proud of what u believe na nakuombea kila la heri.

Anonymous said...

mwenyekiti pole ndio binadamu tulivyo hatuwezi kuwa na mtazamo sawa, pia inasikitisha kuona shule zimeongezeka kujengwa lakini bado watu wanaujinga kichwani, kosa liko wapi kwenye hiyo picha mimi ni mkristo na tukienda kubatizwa tunaita wapiga picha ili tupate picha tuwaonyeshe ndugu na jamaa. na huyo anony aache kuwapaka matope wasabato yeye atoe maoni yake sio kupaka matope wasabato hawana ujinga kama huo, ushauri wangu kama unapicha zingine wewe zitundike. hao watu wanamna hiyo ndio wanatuletea vurugu kwenye makanisa.

Post a Comment