Subscribe:

Saturday, February 28, 2009

Zain Yadhamini Tamasha La FESPACO

Zain yadhamini tamasha la FESPACO

* Lina lengo la kuendeleza utamaduni wa Afrika

Dar es Salaam, Februari 27, 2009

ZAIN, kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa huduma bora Afrika na Mashariki ya Kati, imetangaza kujitosa kudhamini tamasha maarufu la filamu na televisheni la Pan African Film and Television Festival of Ouagadougou (FESPACO) litakalofanyika Burkina Faso.

Tamasha hilo la kila mwaka, ndilo kubwa zaidi la kuendeleza utamaduni wa kiafrika barani Afrika na linahusu zaidi filamu za Afrika na waandaaji filamu wa Afrika. Mara ya kwanza tamasha hilo lilifanyika mwaka 1969, na mwaka huu litakuwa tamasha la 40 la FESPACO linalotarajiwa kufanyika kuanzia leo (Februari 28 hadi Machi 7, 2009) kwa sherehe za ufunguzi kwenye Uwanja wa Taifa wa Stade du 4-aout, mjini Ouagadougou.

Tamasha hilo la kimataifa limejijengea heshima barani Afrika na duniani kwa ujumla, lengo likiwa ni kupanua wigo wa medani ya filamu Afrika, kudumisha ushirikiano, kubadilishana mawazo na kupromoti kazi za filamu. Lengo lingine la FESPACO ni kupanua wigo na maendeleo ya sinema Afrika. Akizungumza kuhusu udhamini huo, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zain Afrika, Tito Alaiaid alisema: "Tunaona fahari kuwa wadhamini wa tamasha hilo kabambe.

Udhamini huu unaonyesha jinsi Zain inavyowajibika kusaidia jamii na kupromoti sanaa na utamaduni wa Afrika. Tunaamini Afrika itafikia malengo na Zain tutaendelea kusaidia kadri ya uwezo." Katika udhamini huo, Zain itatoa huduma ya simu katika tamasha hilo na kupamba uwanja kwa ajili ya sherehe za ufunguzi na kufunga ambapo kutaonyeshwa filamu za kitamaduni za Afrika. Kwa miaka kadhaa sasa, Zain imekuwa ikidhamini matukio mengi yanayohusu utamaduni na elimu Afrika ikiwa ni pamoja na tamasha la kimataifa la kusherehekea Nelson Mandela kutimiza miaka 90 jijini London, kudhamini tamasha la MTV Africa Music Awards (MAMAs).

Kwa kushirikiana na Ericsson na Earth Institute, wamesaini mkataba wa kutoa huduma ya mawasiliano ya simu selula na intaneti katika Mradi wa Vijiji vya Milenia unaohusu watu 400,000 katika nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Pia Zain inadhamini mashindano ya vyuo vikuu ya Zain Africa Challenge, ZAC, yanayoendeshwa kwa njia ya televisheni yanayogusa mamilio ya watu katika nchi nane barani Afrika.

Katika tamasha la FESPACO ambalo kauli mbiu mwaka huu ni "Simena za Afrika: kukuza utalii na utamaduni", Zain pia imeshirikiana na RFI na BBC, kudhamini zawadi maalumu yenye thamani ya dola 4,000 itakayotolewa kwa washindi. Tamasha la mwaka huu limeandaliwa kwa heshima ya Ousmane Sembene, mmoja wa waasisi wa kutengeneza filamu za kiafrika na mwasisi wa FESPACO, aliyefariki dunia Juni 9, 2007.
Reactions::

0 comments:

Post a Comment