
Klabu ya Yanga juzi ilichukua ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2009/10. Na Clarence Mahunda, Hale, Tanga.
( Yanga siku zote ni Yanga, utawajua tu. Simba ubingwa hatuutangazi hivyo!) Tukiweka utani pembeni, tunawapongeza Dar Young Africans, ubingwa mwaka huu mlistahili.




Tanzanian Shilling Converter
3 comments:
Jambo moja ambalo wengi wanaweza kuwa hawajashituka ni kwamba tangu 2006 Kikwete alipoingia madarakani Yanga wamekuwa wakichukua ubingwa mfululizo.
Wapo wanaojipendekeza kuipa ushindi Yanga kumfurahisha Kikwete ambaye siyo siri ni shabiki wa Yanga.
Kwa mtindo huu, mpaka atakapoondoka madarakani ndiyo wengine mtapata fursa ya kubeba kombe, probably 2015 au mapema zaidi...who knows.
Anonymous Date: Thu Mar 26, 04:50:00 PM EAT,
We anon hapo juu hebu wacha unazi usiokuwa na mantiki bwana, hivi kweli kwa upeo wako unaweza ukasema kuna njama zinafanywa ili kuipa yanga ubingwa kisa mheshimiwa Rais anaipenda Yanga duh kwanza napata mashaka kidogo juu ya uelewa wako kwenye medani ya soka ya Tanzania, hivi bi kweli Yanga wamechukua kombe mfululizo toka Kikwete ameingia madarakani?? Nikuulize swali moja tu ni timu gani ilikuwa bingwa kwenye ligi ndogo ambayo ilichezwa pale uwanja wa jamhuri morogoro kutokana na matengenezo ya uwanja wa Taifa/ Uhuru kwa sasa?? na kama utajua ni timu gani je ilikuwa ni mwaka gani na mwezi gani? Na kama ukijua hili je katika kipindi hicho nani alikuwa raisi wa Nchi hii? Na kama ukijua hili ni nani aliyeenda kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya klabu bingwa Africa? Na kama ukijua hilo ni nani aliyepewa kichjapo cha mbwa mwizi na Enyimba??
Ni matumaini yangu utakuja na hoja zilizoenda shule na zenye muelekeo wa kuonyesha njia sahihi juu ya hili, ukishindwa basi muandikie private msg mheshimiwa mwenyekiti wa kijiji hiki am sure atakuelekeza kwa ufasaha maana yeye ni mnazi mkuwa wa SIMBA
Willy-Udsm
Hii alama ya Wanajangwani NZURI SANA.
Post a Comment