
"...ndugu zangu,uwaziri hausomewi..." Haya ni maneno ya Mh.Kikwete wakati akitangaza baraza la mawaziri mwaka 2005.Hata urais hausomewi.Ingawa kwa hapa kwetu inahitajika shahada yoyote(si mimi ndivyo ilivyo).
Huko Madagaska DJ amechukua nchi,nna imani ataweza kama wenyewe wamemtaka kwa utaratibu wao,UKIZINGATIA HAUSOMEWI..Imeletwa na Clarence Mahunda, Hale, Tanga.




Tanzanian Shilling Converter
9 comments:
Nikweli uraisi hausomewi, lakini lazima kuwe na standard ambayo itaweza kuchuja chuya na mchele. Nadhani AU inakila haki ya kutomtambua huyu DJ kwa kila sababu za msingi. Uraisi sio tumbo kusema kila mtu kazaliwa nao, uraisi unaitaji uelewo mkubwa wa mchakato mzima wa dunia.
sawa anonymous wa hapo juu. Lakini maraisi wangapi wanauelewa na bado nchi kwao wanashindwa kuongoza? Mugabe ana degree ngapi? AU imejaa unafiki tu hawanauwezo wa kufanya maamuzi ya kijasiri. AU inaundwa na maraisi ambao wengi wao hawajachaguliwa kihalali (wamejitangaza wenyewe). Mugabe, Kibaki, Museveni, Gadafi n.k. Sasa hawa ndio wa kuwakataa wenzao ambao hawajachaguliwa kidemocrasia.
Mwenyekiti Mjengwa, kauli ya mh.Kikwete kwamba uwaziri hausomewi aliitoa kwa sababu maalumu. Na kubwa ni kwamba kuna watu aliotaka kuwateua (wanamtandao wake) ambao alikuwa anajua elimu na uzoevu wao ungeleta minong'ono. Hivyo hiyo kauli ilikuw ni njia ya kujilinda na minong'ono.
angalieni video ya Id Amin..utajua ujuha wa baadhi ya marais wetuuuuu
http://video.google.com/videoplay?docid=4169600956573058582&hl=en
sijaona mahali popote ulipotaja elimu yake. Uliambiwa na nani kuwa wanaofanya kazi ya u-dj hawana elimu?
haya tena ma dj na waimbaji kazeni kamba ,punguzeni maskando ili siku moja muchukue nchi,time imefika,mabadiliko yoyote hivi sasa duniani musiyashangae, LULA DA SILVA WA BRASIL alikuwa ni fundi viatu,hivi sasa ni rais wa taifa kubwa kuliko yote south america,ma dj na waimbaji muna wapenzi wengi sana,munatakiwa mutoe ujumbe wa uhakika kwa wa tz na muache mascando,ili muchukue nchi siku moja
Hata wanamuziki wanaweza tumkabidhi nchi Mrisho Mpoto
huyu jamaa wa kwanza hamna kitu kweli sisi tunaojidai sijui michakatosijui nini ndo hamna kitu dunia ya leo ina kwenda na fect kama utaweza kuwaonesha watu kuwa kuna matumaini japo kwa nadharia tu na wakiwa tayari kufuata maelekezo yako inatosha sisi tunaojidai wa formula ndo hamna kitu hata ukiangalia watu wakawaida tu walioendelea sana si waformula kaaa tu mpaka wamalize phd ndo uwachakuwe wakuongoze shamba kubwa weee tena toka hapa huna jipya kama jamaa zako wasivokuwa na jipya et mabada unadhani yanasaidia sana katika mambo ya uongozi umeniuzi kimbiya kenge wewe
Anon wa kwanza huna hoja. Naungana na anon wa pili. African Union ni wanafiki watupu. Genge la wanafiki. Rais 'halali' hatakuwa halali kwangu pale AU itakaposema marais hawa sio halali. Kabila (alihadaa na kuchukua Congo akiwa na umri mdogo kuliko Rajoelia), Mugabe, Kibaki, Omal al BAshir (Haiwezekani eti Mtwara (darfur) kuna vita halafu unasema nchi (tanzania) iko shwari, ndio maana wenzie wanamburuta the Hague.
AU waache unafiki kwanza ndio wasimtambue huyu rais ambaye amekubalika na jeshi, wananchi na mahakama. Watoe vibanzi machoni mwao kwanza.
hapa swala si kutambulewa na umoja wa nchi za afrika na wala si elimu. swala ni,je kafanya kanuni za katiba ya nchi yake,ni kimaanisha amechaguliwa na wananchi kwa kura kama katiba inavyotaka. au katumia mfumo usikuwa wa kidemokrasia kama vile mapinduzi ya kijeshi.kwa njia hii basi hawezi kutambulika na umoja wa afrika kutokana si rais halali wa madagascar,ilikuwa busara kuitisha uchaguzi na wananchi wakapata fursa ya kuchagua kiongezi wanayemtaka.
Post a Comment