Subscribe:

Tuesday, March 31, 2009

Mheshimiwa Mwenyekiti


Pichani ni Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania waishio Mysore, India. Anaitwa Mwinga Mungwe. Alichaguliwa jana jioni. Hongera sana!
Reactions::

8 comments:

Anonymous said...

Analipa

Anonymous said...

Wewe dada mzuri. Hiyo mdomo! Tuwekee contacts dada yetu.

Anonymous said...

anahitaji "proactive"

Anonymous said...

mbona kachoka au ana mimba?

Anonymous said...

Lakini na wabongo bwana, mbona mpenda kukandia wenzenu hivyo, wewe hiyo mimba ulimpa? wewe umemfahamia wapi mpaka useme amechoka? tamaa hiyo wapigwa vumbi,

Anonymous said...

Wape hongera zao, mdau, Solan, Himachal, India.

Anonymous said...

wee mimba ni ishara ya kukamilika wee kama unaona ni jambo la aibu kivyako! sijampa mimba maana sina kifaa!

Anonymous said...

Mwe! ndi mana mimi naogopa kuleta picha yangu kwenye blogu! Jamani tena picha yenyewe ilivyo ya bibi kizee na pua yangu kubwa, ngozi imebabuka si ndio mtatukanana kabisa na kunitukana na mie kizee cha watu! Hakuna haja ya kugombana wajukuu zangu hizi picha kila mtu anatafsiri kifyake, wengine wataalamu wakiangalia pua ya mwanamke, hapo shingoni panapokuwa kama panahema, muonekano wa sura, na matiti kama yanaonekana basi hata kama mwanamke huyo ana mimba ya wiki moja watamjua tu! Basi usiombe mtu wa namna hiyo ndio awe matron kwenye shule za wasichana za bweni! wasichana watakoma!! Au mtu wa aina hiyo awe shangazi yako ukinasa tu kishakudaka! Wasichana wana kazi kweli kweli!

Lakini ukishakuwa mtu mzima mimba zinatafutwa mahospitalini mpaka kwa waganga wa kienyeji! Usiombe ukakutana na mwanamke anayetafuta ujauzito ili angalau na yeye aje aitwe mama! Yaani akisikia kadalili tu hata kama ni mabadiliko ya hali ya hewa atakwenda kupima! Hamjasikia wengine wanapataga mimba za mawazo? Yaani anawaza mimba wee mpaka anaathirika kisakolojia, mpaka anafunga siku zake na kujikuta na dalili zote za ujauzito wakati hana kitu! Ni mateso makubwa anapokuja kugundua kuwa alikuwa na mimba ya mawazo!

Basi jamani wajukulu zangu msigombane bure kwa ajili ya picha ambazo mwenyewe hamumjui! Nyie furahieni changieni elimishaneni ndio malengo ya kuwepo hapa duniani wala msikarike mkazalisha nyogo ambazo zikawazeesha bure kabla ya siku zenu, kwani hasira zinazeesha ndio maana zikaitwa hasara.

Mswahili

Post a Comment