
Mwanamziki wa dansi MR.Buti Jiwe aka Garinoma,Jr. anayefanyia shughuli zake nchi Holland! ameibuka na Album ya moto wa kuotea mbali yenye jina na nembo yake
"Buti Jiwe".Mwanamziki huyu Mr.Buti Jiwe,ni kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi" wa
bongo,Mr.Buti Jiwe amejijengea umaarufu nchini Uholanzi na amepania kwa mwendo
wa kasi wa kutimia BUTI JIWE lake kuhakikisha dansi lake linasambaa kila mahali duniani!
Nia yake hiyo nzuri inamfanya kupokelewa kwa mikono miwili ya washabiki pamoja na
bendi mabali mbali za mziki wa dansi katika kila kona.
Mr.Buti Jiwe anatoka katika familia ya wenye damu ya mziki,lakini mafanikio yake yanatokana na kujitima pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyo nayo,ambayo inawezekana kuwa mfano wa kuigwa na kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi".
Mr.Buti Jiwe na CD yake "Samahani" inaonekana kuanza kutawala vituo mbali mbali vya radio barani Ulaya.
Mwendo huo wa kasi wa MR.Buti Jiwe,Garinoma (Jr) unaelekea kupiga teke kwa njia ya mziki katika kila kona duniani,Mwanamziki huyo kijana mwenye majina ya kutisha
Mr.Buti Jiwe aka Gari!Noma! anafananishwa na gari lenye mwendo wa kasi ya hatari kimziki! gari ambalo ukidandia ni hatari ya NOMA.
wale wadau wanaotaka kuisambaza CD ya Mr:Buti Jiwe wasisite kuwasiliana na buti jiwe
at butijiwe@yahoo.com




Tanzanian Shilling Converter
2 comments:
kaza buti kaka, tutapenda kusikia vitu vyako, naamini vitakua vinatisha, mdau
yoh vitu nimevikubali,kaza uzi sasa toa video yake kamanda,najua itakuwa hoooot,come en shoot in groningen yoooooooooooooh.butijiwe
Post a Comment