Subscribe:

Tuesday, March 31, 2009

Mpunga Huo, Usipouchagua....


Utaula wa chuya!
Reactions::

6 comments:

Anonymous said...

MPUNGA WA KWETU UNA RANGI YA KAHAWIA KWA SABABU YA MAGANDA YAKE NA MCHELE HUWA MWEUPEE, MPUNGA HUU UKIKOBOLEWA UTAKUWA NA RANGI YA KAHAWIA?

Malafyale Nsana said...

Huo ni mchele au Mpunga, Wasukuma hawajui kutofautisha mchele na mpunga wao au shamba au umekobolewa wanaita mamichele na wale Jamaa ambao wamebahatika kuwa na mchele unanukia vizuri wale Malafyale nao kwao ni Mpunga tu.Naomba mnisaidie mchele ni upi na mpunga ni upi?

Anonymous said...

Mpunga, mchele, wali...?

Mchele mzuri ni ule wenye rangi ya kikahawia ingawa wengine wanapendelea mchele mweupe!

Anonymous said...

kaka mjengwa mchele unachambua siyo unachagua.....

Anonymous said...

Malafyale, mchele ni ule uliokwishakobolewa, na mpunga ni ule uliokuwa bado haujakobolewa. Na kuhusu kuchagua au kuchambua, pwani mpunga unachaguliwa sio kuchambuliwa! Ndio maana tunapoalikana shughuli zetu ambazo zinahitaji maandalizi ya chakula, huambizana "kesho kuna kazi ya kuchagua mchele!"

Mdau Mswahili

Anonymous said...

Kaka Maggid umenikumbusha ile methali ya "Amekula wali wa chuya kwa uvivu wa kuchagua". Baada ya mchele kukobolewa masalio ya mpunga katika mchele huitwa "chuya"
Wa Tanga.

Post a Comment