Katika kila tufanyalo, tukumbuke, kuwa kuna Watanzania wenzetu kwa mamilioni ambao hawana huduma muhimu kwa mwanadamu. Kuna lazima ya sauti zao kusikika; SIKILIZA: http://www.kwanzajamii.podomatic.com
Kazi nzuri sana. Sasa napata mwanga zaidi kuhusu falsafa na hisia zako, ambazo zinaonekana kweye picha mbali mbali ndani ya blogu, lakini kwa maelezo ya sauti yako, nakuelewa zaidi, hisia na mtazamo wako kuhusu maisha ya wananchi. Mungu azidi kukubariki.
Brother Maggid, hongera sana kwa jitihada za kuielimisha jamii. Podcast imekua nzuri sana pamoja na mafua lakini imesikika vizuri. Hongera sana na Aluta continua!
Iyo bomba sana.Ningepata nafasi ya kua FISADI ningeelekeza nguvu zangu kuwarudishia watu kama hawa kiasi nilichochota,MUNGU tusahidie tuepukane na roho ya VIJICENT
Majjid, kudos naona podcast imetulia na sauti yako inaunganisha hisia halisi za picha zako. Ila ongeza speed kidogo, kwani inaweza kumfanya mtu akasinzia. halafu miziki yako pia nimeipenda sana inavuta hisia za ndani kabisa katika kufikiria kwanzajamii.
Ningependa kama utakuwa unakusanya maoni ya watanzania masikini na kuyaweke hapa jinsi wanavyotaabika, walivyosahaulika hasa vijijini ambako wengi wao bado hawana ndoto hata ya kufika mjini. Hii itafanya wewe kuwa mjumbe na pengine wenye nia mbaya wakakosa cha kukutwisha maana usije kuta wanaanza ku-capitalise kisiasa maoni yako kuhusu unayoyaona hasa in the field.
Hongera sana ndgu Maggid! Kazi uifanyayo ni mfano wa kuigwa katika jamii ya Tanzania ambayo imeanza kuonyesha taswira ya kukosa mwelekeo na huenda tumaini la kilicho bora kwa wote. Jamii yetu imefikishwa mahali ambapo haiwezi tena kumwamini kiongozi kwa lolote asemalo kwa kuwa udanganyifu umekuwa sehemu ya sifa za watawala na wanasiasa wa Tanzania.
Sauti yako inaelezea aina ya mtu mwenye hisia za kuguswa na hali ya maisha duni ya watz wenzetu huko vijijini. Ni watanzania hawa wakabiliwao na adha za kila aina watumiwao na wanasiasa kuendeleza unyonyaji na ukandamizaji wao kwa gharama ya imani na matumaini juu ya watawala wetu. Ni watz hawa walazimishwao kusikiliza malumbano ya watawala juu ya maslahi yao binafsi kupitia miradi iitwayo ya wananchi na kuishia mifukoni mwao, huku wananchi wakiwa hawana uhakika wa japo mlo mmoja, achilia mbali tiba nzuri, elimu nzuri kwa watoto wao, masoko kwa mazao yao nk, nk.
Mambo uliyoyaona ndiyo yaliyomfanya Baba wa Taifa aseme kuwa sio rahisi kwa mtu anayeguswa na matatizo ya Wananchi akakimbilia kwenda Ikulu. Nadhani dhana hii inashuka hadi uongozi wa chini. Kwa kutojali utatuzi wa shida za wananchi sasa kila mtu anataka awe Mbunge au Diwani ili ajinufaishe na mali ya umma, hali hii isingekuwepo kama kungekuwa na kuwajibika kwa wananchi na sio kwa chama.
Usife moyo katika dhamira yako ya kuwatumikia watz, ni kazi ngumu, iumizayo sana kihisia, lakini haina budi kufanyika ili kujenga msingi mpya juu ya mustakabali wa watz. Ubarikiwe sana kwa kazi njema kwa taiifa letu
Sasa nimekutofautisha na M.M Mwanakijiji. Siku moja nilisikiliza kupitia blog hii maelezo ya mtu mwenye sauti kali na kiswanglish kingi, alikuwa anagombeza wale waliomkosoa Sofia Simba kuwa anajidai kwa Elimu yake!
Nilijiuliza sana, je Maggid Mjengwa ndiye M.M Mwanakijiji?? Mbona kauli na kugombeza huku hakusawiri vema taswira iionekanayo ktk sura na maandishi yake?? Nilijiridhisha tu kwa kukubali kuwa saikolojia yangu ilikuwa ndogo juu ya kusoma hisia na tabia za watu kupitia picha na maandiko yao.
Nashukuru leo kwa kukusikiliza nimepata jibu la wasiwasi huo. Endelea kuchapa kazi maana umma wa Watanzania wanakuombea mema kwa kadri uwafikiriavyo. Watanzania, hasa wa kawaida vijijini humpenda na kumheshimu sana mtu anayewaheshimu na kuhangaika kwa ajili yao, ndio maana bado wanamlilia na kumkumbuka Mwalimu Nyerere, hakuwapa pesa bali fursa za elimu bora kwa watoto na afya bila ubaguzi wa kipato.
Mwenyekiti HONGERA SANA, unajua kuna jambo moja kiubinadamu. Ukimuona mtu pichani, huwa unahisi hata sauti yake itakuwa hivi ama vile, kuna wakati inakuwa sawa, na kuna wakati inakuwa tofauti. Kwangu imekuwa tofauti.
Kuhusu hii "podcast" kusema ukweli umefikisha ujumbe mzito ambao ndio maisha yetu waTZ tulio wengi. Sasa wazo langu, pia jaribu kuwa unafanya mahojiano pia na watu mbalimbali kupata mawazo yao. Nakutakia kila jema.
WATANZANIA HAWA NI VIGUMU KUSAIDIWA KWANI WANAYAPENDA MAISHA HAYA NA WAMERIDHIKA NAYO, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. TUKUMBUKE WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU VIONGOZI WALIPITA HUKO VIJIJINI NA KUWAELEZA WANANCHI HAO KUWA HIVI SASA WANA MAJI SAFI KWA SILIMIA 98 YA WATANZANIA NA UMEME, PIA SIMU AMBAPO MALECELA ALISEMA KUWA SASA HIVI HATA MMASAI ANAWEZA KUMPIGIA SIMU MAMA KAYAYII AKIWA MACHUNGONI NA NG'OMBE WAKE WALISHANGILIA SANA KWA MAFANIKIO HEWA HAYO SASA UTAWASAIDIAJE MAGAZETINI? KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWANYIMA ELIMU YA URAIA WATANZANIA NA KUFANIKIWA KUWAFANYA WABAKI GIZANI.
12 comments:
Inasikika vyema.
Mwanzo mzuri!
Kazi nzuri sana. Sasa napata mwanga zaidi kuhusu falsafa na hisia zako, ambazo zinaonekana kweye picha mbali mbali ndani ya blogu, lakini kwa maelezo ya sauti yako, nakuelewa zaidi, hisia na mtazamo wako kuhusu maisha ya wananchi. Mungu azidi kukubariki.
Brother Maggid, hongera sana kwa jitihada za kuielimisha jamii. Podcast imekua nzuri sana pamoja na mafua lakini imesikika vizuri.
Hongera sana na Aluta continua!
Iyo bomba sana.Ningepata nafasi ya kua FISADI ningeelekeza nguvu zangu kuwarudishia watu kama hawa kiasi nilichochota,MUNGU tusahidie tuepukane na roho ya VIJICENT
Hongera Mr Mjengwa.
C/MAN NIMEFURAHI KUSIKIA SAUTI YAKO. SAFI MZEE.MIE NITAKUTAFUTA NIKIRUDI BONGO.NITACHOTA BUSARA ZAKO.
Majjid, kudos naona podcast imetulia na sauti yako inaunganisha hisia halisi za picha zako. Ila ongeza speed kidogo, kwani inaweza kumfanya mtu akasinzia. halafu miziki yako pia nimeipenda sana inavuta hisia za ndani kabisa katika kufikiria kwanzajamii.
Ningependa kama utakuwa unakusanya maoni ya watanzania masikini na kuyaweke hapa jinsi wanavyotaabika, walivyosahaulika hasa vijijini ambako wengi wao bado hawana ndoto hata ya kufika mjini. Hii itafanya wewe kuwa mjumbe na pengine wenye nia mbaya wakakosa cha kukutwisha maana usije kuta wanaanza ku-capitalise kisiasa maoni yako kuhusu unayoyaona hasa in the field.
Aluta....
Hongera sana ndgu Maggid!
Kazi uifanyayo ni mfano wa kuigwa katika jamii ya Tanzania ambayo imeanza kuonyesha taswira ya kukosa mwelekeo na huenda tumaini la kilicho bora kwa wote. Jamii yetu imefikishwa mahali ambapo haiwezi tena kumwamini kiongozi kwa lolote asemalo kwa kuwa udanganyifu umekuwa sehemu ya sifa za watawala na wanasiasa wa Tanzania.
Sauti yako inaelezea aina ya mtu mwenye hisia za kuguswa na hali ya maisha duni ya watz wenzetu huko vijijini. Ni watanzania hawa wakabiliwao na adha za kila aina watumiwao na wanasiasa kuendeleza unyonyaji na ukandamizaji wao kwa gharama ya imani na matumaini juu ya watawala wetu. Ni watz hawa walazimishwao kusikiliza malumbano ya watawala juu ya maslahi yao binafsi kupitia miradi iitwayo ya wananchi na kuishia mifukoni mwao, huku wananchi wakiwa hawana uhakika wa japo mlo mmoja, achilia mbali tiba nzuri, elimu nzuri kwa watoto wao, masoko kwa mazao yao nk, nk.
Mambo uliyoyaona ndiyo yaliyomfanya Baba wa Taifa aseme kuwa sio rahisi kwa mtu anayeguswa na matatizo ya Wananchi akakimbilia kwenda Ikulu. Nadhani dhana hii inashuka hadi uongozi wa chini. Kwa kutojali utatuzi wa shida za wananchi sasa kila mtu anataka awe Mbunge au Diwani ili ajinufaishe na mali ya umma, hali hii isingekuwepo kama kungekuwa na kuwajibika kwa wananchi na sio kwa chama.
Usife moyo katika dhamira yako ya kuwatumikia watz, ni kazi ngumu, iumizayo sana kihisia, lakini haina budi kufanyika ili kujenga msingi mpya juu ya mustakabali wa watz.
Ubarikiwe sana kwa kazi njema kwa taiifa letu
Sasa nimekutofautisha na M.M Mwanakijiji. Siku moja nilisikiliza kupitia blog hii maelezo ya mtu mwenye sauti kali na kiswanglish kingi, alikuwa anagombeza wale waliomkosoa Sofia Simba kuwa anajidai kwa Elimu yake!
Nilijiuliza sana, je Maggid Mjengwa ndiye M.M Mwanakijiji?? Mbona kauli na kugombeza huku hakusawiri vema taswira iionekanayo ktk sura na maandishi yake?? Nilijiridhisha tu kwa kukubali kuwa saikolojia yangu ilikuwa ndogo juu ya kusoma hisia na tabia za watu kupitia picha na maandiko yao.
Nashukuru leo kwa kukusikiliza nimepata jibu la wasiwasi huo. Endelea kuchapa kazi maana umma wa Watanzania wanakuombea mema kwa kadri uwafikiriavyo. Watanzania, hasa wa kawaida vijijini humpenda na kumheshimu sana mtu anayewaheshimu na kuhangaika kwa ajili yao, ndio maana bado wanamlilia na kumkumbuka Mwalimu Nyerere, hakuwapa pesa bali fursa za elimu bora kwa watoto na afya bila ubaguzi wa kipato.
Kaka sasa naongeza heshima kwako,Nilikua na mtazamo mwingine unapotembelea vijijini,nilijua mambo ya mtelemko.

Post a Comment