Subscribe:

Wednesday, March 25, 2009

" Sisi Ni Ndugu Kabisa!"


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa wanasiasa wa Comoro kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yao ili kulinda na kutunza amani na utulivu kwa manufaa ya wananchi na visiwa vyao.

Rais Kikwete ameyasema katika hotuba yake kwa wananchi wa Comoro katika ukumbi wa Bunge ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara ya kiserikali katika visiwani vya Comoro.

“Wanasiasa wana dhamana ya kulinda wana Comoro, wanasiasa ndiyo chanzo, mkiamua nchi iwe na umoja, amani na utulivu itakua , mkiamua visiwepo nchi itakosa vyote” amesema Rais Kikwete na kuwaasa kuchagua umoja, amani na utulivu.

Amesema siku zote watu wa nje hulaumiwa, lakini nao hushirikiana na watu wa ndani na hivyo wanasiasa wakiacha kushirikiana na watu wa nje dhidi ya maslahi ya nchi amani na utulivu vitadumu.

“Mara nyingine tamaa za madaraka na mali husababisha kuvunjika kwa amani na wananchi ndiyo wahanga wa tama hizi za wanasiasa, heshimuni yale mnayokubaliana kufanya wakati wa mazungumzo, mkikiuka hizo taratibu mlizokubaliana mnaleta matatizo” Rais Kikwete ameongeza na kusema kuwa mkataba wa Fomboni, mkataba ambao umeweka taratibu za mapatano baina ya visiwa vya Comoro ni chanzo na njia nzuri ya maridhiano.

“ Mkataba wa Fomboni umeweka misingi mizuri ya Demokrasia, kwa kubainisha kuwa viongozi watachaguliwa na wananchi, visiwa vyote vitatu vya Ngazidja, Anjouan na Moheli vina heshima moja na sawa na kwamba viongozi watabadilishana baina ya visiwa”. Amesema Rais Kikwete.

Mapema baada ya kuwasili Rais Kikwete amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro mheshimiwa Ahmed Abdallah Mohamed Sambi katika ikulu ya Comoro na kuelezea nia yao ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.

Rais Kikwete ameahidi kufungua ubalozi mdogo visiwani Comoro haraka iwezekano ili kurahisisha mawasiliano baina ya nchi na wananchi wake.

Katika ziara hii, Tanzania na Comoro zinategemea kutiliana saini mikataba mbalimbali ya kibiashara na kijamii.

Baadaye leo (25.Machi, 09) Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajia kutembelea kisiwani Anjouan ambapo atapokea Tuzo kufuatia mchango wa Tanzania katika kuvikomboa visiwa vya Anjouan kutoka katika serikali ya Uasi ya Kanal Mohammed Bacar na baadaye kufungua tawi la Exim Bank.

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Moroni, Comoro

24. Machi, 09
Reactions::

2 comments:

Anonymous said...

http://www.thisday.co.tz/News/5510.html
POINT BLANK: Pinda, tell it to the nawabs spending fortunes abroad


John Nkwazi
Canada

AGAINST the odds, Prime Minister Mizengo Pinda was recently quoted as telling Tanzanians pursuing their education abroad to come back home with tractors. What a hoopla?
When you look at how possible this is, you end up laughing at those making it and those taking it seriously.
Being in the process of becoming a scientist dealing with how nawabs think, especially how power turns them wicked and sick, I am trying to figure out how these winos really think? When you hear their make-believe stuff, you sometimes feel nauseatic.
Being a guru in criminology and penology, my concentration is on how biggies think they know whilst they don�t.
I think Pinda suggested this tractor thing hoping people would like him for having a soft for the forgotten sector of agriculture that was overtaken by hawking and vending. After some smart chaps discovered that by a stroke of a pen one can get away with billions he stashes abroad like one Andrew Chenge, they doomed agriculture.
What forces me to study how big filchers think is the truth I always see. Aren�t they the same creatures that purchased a hand-me-down radar at a super inflated price? Why didn�t they buy tractors instead?
They�re telling us to come back home with tractors. Good and perfect. What about them who spend much of their money and time touring the world? If this is real and serious, I think President Jakaya Kikwete will bring home over a half of these desired machines.
So too will his wife, who always accompanies him almost everywhere abroad, bring many before the paupers like us do.
To help Pinda attain his goal, there are other areas through which tractors can be imported. His government is renowned for liking oil guzzlers we refer to as the shangingis.
Currently, Bongolala is the country of shangingis. Everyone who is a who in Tanzania likes and uses these machines at the expense of a poor taxpayer. From the district level, to the State House, these creatures are much more used by Tanzanians than even the Japanese that make them.
Why doesn�t his government purchase tractors in lieu of these loss-making machines?� What makes the situation worse is the fact that when shangingis are purchased at a super-hiked price, they�re used for a short while. Thereafter they are grounded so as to be sold at a throw away price to the same biggies! My friend calls this theft within theft.

If I were Pinda I�d urge people to come with the copies of the constitutions of foreign countries they�re studying in. This would enable us to have good and democratic governance based on accountability in lieu of technical know- who.
Further, I�d urge them to come with new ideas about development and the rule of law. These countries we call rich and developed did not attain their status by stealing from public offices as we saw at Ubungo Bus Terminal, EPA, Richmond , Kagoda and such.
They attained their development by means of accountability and delivering. They invested in the potentials of people instead of hawking, defrauding and conning.
Another thing I�d urge guys abroad is: Bring with them ideas of abhorring begging especially for the nation endowed with almost everything. This, coupled with monetary discipline, I�m sure would add up especially if they remember strategies on how to curb corruption.
The other day I was at a water hole doing battle on a liquor when this Pinda thing cropped up. You know what? A friend of mine said �I support Pinda although I differ with him on one thing. Instead of bringing tractors, our brethren studying abroad should bring back many fake PhDs just like some of our bigwigs. This will help our country to be regarded as the most educated one.�
From his point of view I realized one thing. What if our government stops employing fake experts?
Things went wrong when we killed ’kilimo cha kisasa’ and ushered in ’kilimo cha kisiasa’. This has had great knock-on effects on our country though we don�t want to face it.
Shall this call make sense, it does so to the likes of Andrew Chenge, Idris Rashid, Amatus Liyumba, Kagoda, ANBEN, Fosnik, Tanpower and such. How many tractors would their loots import?
Folks, you are sitting on riches. So stop bluffing! Why should your money be stashed abroad as you urge others to import tractors to serve non-existent agriculture? Tell it to the birds ’Mheshimiwa PM’.
mail: nkwazigatsha@yahoo.com

Anonymous said...

Jamani hii bitterness inatoka wapi? Maana hata hiyo lugha yote imeharibiwa na bitterness, na mtu ukiwa na hali hiyo hata unachokiandika hakieleweki. Bwana Nkwazi sidhani kama huyo Mheshimiwa Pinda unayemlalamikia ana mapesa ameyaweka huko nje, ana utajiri ya kina Bwana Vijisenti. Na sioni kosa lake la kuwashauri watu kuwaagizia ndugu zao walio vijijini hayo matrekta.

Na kuhusu matrekta wako wanaowayaleta hapa nchini badala ya kuleta ma-Hammer, ma- Mezedez Benz na Macruiser kwa ajili ya kutembelea kilometa chache za hapa Dar. Ni utashi wao hatuwalaumu, lakini kwa sie tuliotoka katika familia za kimasikini kama mheshimiwa Pinda tunafahamu umuhimu wa hayo matrekta huku vijijini kwetu, tena hata yakiletwa yakusukumwa na binadamu au hayo yanayotumia mafuta kidogo kwetu yatatusaidia sana kuondoa umasikini kuliko kuja na magari yenu ya kifahari ya kukogana huko mijini. Hata kama na kashamba kakngu ka eka 4 hilo trakta litaniwezesha kulima hizo eka 4 kwa haraka na nikipatiwa mtaalamu eka 1 nitavuna magunia 20 badala ya 2 ninayovuna sasa. Vile vile nitalima shamba langu kwa muda mfupi sana na nitatumia trakta langu kulimia wakulima wenzangu kijijini. Tena sio bure kwani eka moja nitailima kwa kuanzia shilingi elfu 20 mpaka elfu 30. Sasa hapo hata wewe ndugu yangu, mwanangu uliye nje hutakuwa na majukumu tena ya kunitumia pesa za chakula na matumizi mengine kwani nitakuwa nimejikwamua kwa kutumia trakta langu, hilo hilo trakta itatoka hapo pesa ya mafuta, vipuri, mahitaji mengine kabla ya msimu wa mavuno na hata ada za shule za wadogo na wajomba zenu hazitakuwa mzigo wenu tena.

Sasa hapo kosa la mheshimiwa Pinda liko wapi? Bado mnasubiri serikali itutoe sisi wazazi, ndugu zenu kwenye umasikini au iwe na sera na mipango madhubuti ya kutuondoa kwenye umasikini tukichanga na bidii zetu na zenu pamoja na hizo sera za serikali, umasikini utaondokana.

Hebu ulizeni taasisi kama African in diaspora za watu wa Magharibi wa Afrika wanafanyaje kuondoa umasikini kwenye sehemu walizotoka? Hivi kama mkama mkiamua kujiunga kweli huko mliko mkaacha hizo za kufanya matanuzi na kushiriki kuondoa umasikini huku nyumbani kwa pamoja mtanshindwa nini? Kwani mkiamua kwa kuwa sie tunatoka labda Ilula, Ifunda na Usangu, leo tununue trakta moja la baba yangu kule ILula kesho kwa upatu wetu tumnunulie baba yako wa Usangu keshokutwa zamu ya Ifunda mtashindwa kweli?

Au hili alilosema Pinda limekugusa panapo mtima? Pinda si tajiri wala fisadi pengine yeye ameona faida ya kumnunulia mzazi wake trakta ndio akaona iwapo watu wangefanya kama yeye pengine ingesaidia. Hebu hesabu hivyo vikopo vya castle na sijui larger gani kwa siku unatumia pesa ngapi, ukiamua kupunguza ukadunduliza hata miaka 3 hujapata bado kitu cha kuwasaidia nduguzo? Hebu watazameni wachaga, wahindi, wachina, na wengineo wanavyofanya nasi tujifunze kutoka kwao.

Bi Mkora

Post a Comment