
Picha hizo nimezichukua karibuni mji uitwao
Adama au Nazareth kule Ethiopia. Bajaj hizo kule ni maarufu kwa jina
"BIMBI" ambapo tafsiri yake ni MBU. Jina hili nimelipenda maana ukitafakari
kwa kina utaona vipikipiki hivi kweli vinafanana na mbu kimaumbile hata mlio
wa injini yake vinapotembea. Moja la muhimu nililoliona jipya ni bimb hizo
kuwa na milango kwenye cabin ya abiria ambayo unaweza kuwekwa na kutolewa.
Ubunifu huu naona haujafika hapa kwetu. Unaonaje na huku kwetu tukaana
kuvitaiza jina la kihehe la "SOOGO"
Mwenyekiti nawasilisha wanachi nao wafaidike.
Mwanakijiji Pasumilemnyiga Changalakiki (Louis Kasuga)




Tanzanian Shilling Converter
7 comments:
vinaleta uchafu nchini, nchi maskini ndio wanatumia, sasa sisi tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?
ni kweli anonymous unaweza kuwa sawa kwa upande mmoja na si hilo pekee pia havina security yo yote, vinasababisha usumbufu barabarani, ni rahisi kuvamiwa kama mtenja anaweza kuwa na mali, ila kwa upande mwingine vinasaidia sana kwa safari fupi fupi sisizo za haraka na hasa kwa walala hoi ambao uwezo wao wa kukodi taxi huwa ni mdogo au wanaoishi maeneo ambayo gari za kawaida haziwezi kufika kwa urahisi. utafiti wa kina wa vi MBU hivi inabidi ufanyike kabla hali haijafikia the point of no return, vinginevyo tunakokwenda vitakuwa uchafu mkubwa na itakapolazimika kuvifuta tutakosa mahala pa kuvipeleka vitaishiwa kufanywa chuma chakavu.
ni kweli kabisa vinaleta uchafu nchini, visingeruhusiwa kabisa hivi vitu
Uchafu huo,,hasa kwa nchi zinazoendelea? Angalia hata Africa magaribi hakuna,,,wentu wanawaza usafiri wa umeme sisi mnataka kuturudisha huko tulipotoka wakati tunalipa koda kila siku,,,uwezo wa kutoresha usafiri Tanzania tuna ila tunaviongozi mafisadi sana,,,leteni picha na mifano iliyo ya kisasa ili tuwaumbue viongozi wetu kuliko hivyo vimmbu watajisifia wao wanafanya kazi sana za maendeleo wakati hakuna kitu wanatunisha matumbo yao kila kukicha
wadau waliochangia hapo juu wameangalia dalili(symptoms) na sio kiini(source) cha tatizo. Uchambuzi wao umelenga mji wa dar es salaam, wakisahau kuna maeneo mengi Tanzania hii amayo watu hawana usafiri wa aina yoyoye zaidi ya baiskeli.Nadhani hatuwezi kuendelea kwa kuruka hatua. Bajaji ni usafiri mzuri kwa watu wa kipato cha chini na kati(asilimia kubwa ya watanzania) Zimetengenezwa zikiwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya petrol. Madhara kwa mazingira (CO2 emmission) ni kiasi kidogo ukilinganisha na kile cha magari.Usafiri wa aina hii ni maarufu sana nchi kama India ambazo ukilinganisha na Tanzania zina maendeleo zaidi kiteknologia na kiuchumi kwa ujumla.Usafiri wa baiskeli ni maarufu katika maeneo ya mijini na vijijini kwa nchi za dunia ya kwanza. Kama bajaji zinaitwa uchafuu baiskeli amabazo watanzania wengi bado hawawezi kumudu mtaziita nini?? Nakubaliana na mdau aliyeanzisha maada hii na kushauri watanzania wengi wanunue aina hii ya usafiri (soogo). Kinachotakiwa ni kufuata sheria za usalama barabarani kuzuia ajali na kuwa na mipango madhubutu endelevu ya kutokomeza tatizo la foleni kwa upande wa mijini.
Mdau, Luhota
Wadau tuangalie hali halisi ya Tanzania, zahanati na vituo vingi vya afya huko vijijini havina hata baiskeli za magurudumu mawili. Wakina mama wajawazito wanajifungua njiani kutokana na kutembea umbali mrefu wanapotakiwa kupata huduma katika hospitali za wilaya na mkoa.Nilidhani tungeshauri kila kituo cha afya angalau kiwe na sogoo kama mdau alivyoshauri.
Mdau
Wadau nakubaliana na nyie kweli hali halisi ya mtanzania wa kawaida ni duni,hasa aliye kijijini,,lakini chanzo cha huo uduni kipo wapi? kuhusu bajaji kutumika kijijini hakika kitafia njiani kikiwa kinapeleka mgonjwa hospitali,,,barabara hakuna jamani?? au hamjui hata mazingira ya vijijini? serikali yetu ikiboresha miundo mbinu ya barabara hadi vijijini hata wakulima watajikongoja na kununua magari yao,,kwanza hakuna barabara huko vijiji na njia zenyewe ni zile ambazo mifugo ilipita au wakati wa uchaguzi wanakijiji walikarabati kwa majembe na mashoka,,,mimi binafsi nasema hizi bajaji ni uchafu,,kuna njia mbadala na serikali ikiamua inawezekana kabisa,,,kweli serikali yetu inashindwa kuboresha miundombinu ya barabara? mbona wakati wa uchaguzi ahadi zinakuwa tele? Tuamke watanzania wenzangu,,,acheni kabisa kuwaza bajaji na tuwaze jinsi gani kodi zetu zitatuletea maendeleo na kuwa ma usafiri wa maana zaidi na wabei nafuu,,Mdau uliotolea mfano wa India nakubaliana na wewe ila umasikini wao pia hujagusia,,nadhani kule kuna watu wa hali ya chini sana kuliko Tanzania,,,Teknolojia yao na maendeleo yao bado hayatoshi na tusipende kujilinganisha kwa mambo ambayo hayata tuletea maendeleo
Mdau
Post a Comment