Subscribe:

Saturday, April 18, 2009

BAP Aeleza Kisa Cha Kujiita Born Again Pagan!



( Ni baada ya kuulizwa na msomaji kwenye Kwanzajamii.com)
Batamwa na wasomaji wengine watukufu:

Ufuatao ni mkitadha wa jina la kalamu la “Born Again Pagan” kwa mwenye kutaka kujua:

Siku moja ya Jumatatu nilisafiri kwa ndege kuelekea sehemu za Midwest, huko Wichita, Kansas, hapa Amerika.

Nilijua safari itakuwa ndefu kwani walisema tungepitia Chicago. Kwahiyo, niliamua kununua gazeti la New York Times – gazeti kubwa kwa wingi wa kurasa na maeneo yake.

Niliingia na kukaa na abiria mwenzangu ambaye alikuwa na Biblia kwenye kimeza chake akienda Chicago. Tuliamkian na kujuliana mambo ya safari.

Baada ya kupaa na kuendelea na safari usalama usalimini, mimi huku nikiendelea kusoma gazeti langu, mwenzangu alifungua Biblia yake.

Kabla ya kutua Chicago, alianza kuniuliza kwa Kiingereza kuwa hilo gazeti la ma-“liberali’ lilikuwa na hadithi gani za maana siku hiyo.

Huku niking’amua kuwa huenda mwenzangu alikuwa ni m-“koservative” (mfaidhina, nilijaandaa kumkabili.

Nilimweleza machache na kuzingatia hadithi moja ya vita huko Afghanistan.

Yeye akaanza kunihubiria kuwa ni wajibu wa watu wa Mungu kuingilia kati katika vita hiyo.

Mimi nikamwuliza endapo binadamu kweli ana haki ya kumpigania Mungu vita.

Akajibu ndio, na kunitolea mifano mingi kutoka Agano la Kale!

Nilimsikiliza kwa makini. Nikasema hiyo ni kweli. Lakini Yesu alikuja kama “Prince of Peace”! Ndio maana hakuna hayo ya vita katika Agano Jipya.

Niliendelea: Yesu anatufundisha kugeuza shavu lingine, na kusamehe saba mara sabini. Mtoa adhabu ni Mungu peke yake, na kadhalika.

Na kwamba Yesu alimwambia Petro aachane na kumpigania. Na kumwonyesha majeshi ya Mungu!

Mara akaniuliza endapo nilikuwa m-Kristu. Nikamjibu ndio. Kumbe nikachokoza nyuki!

Mswali yakazidi…kuhusu ya Biblia na kumhakikishia kuwa naisoma.

Alitaka kujua kama mimi ni mlokole (born again) Nikamjibu ndio.

Punde akapaza sauti, “Aleluya! Mungu asifiwe kwa kutuweka viti vya karibu.”

Hapo ndipo nikamjibu kuwa kakosea. Yeye akaguna kuonyesha kwa nini.

Nikamjibu, “I am a Born Again Pagan”.

Akakaa kimya na kunikodolea macho! Hakuzungumza nami tena!

Mara tukaambiwa kuwa tulikuwa tunatua O’Hare Airport.
Reactions::

13 comments:

Anonymous said...

Story ya kufurahisha, na kusikitisha

Anonymous said...

Mjengwa, niko nje ya mada. Lakini hii story imeifanya Tanzania kusubiri kwa hamu.

Habari za kuaminika ni kwamba Mrisho Ngassa hakubahatika kuingia hatua ya pili ya majaribio katika timu ya West Ham.Na tayari ameagizwa kupanda ndege kurejea Tanzania.

Sababu zinazotajwa ni kushindwa kwake kumudu mchakato wa majaribio - fitness na awareness.

Lakini pia kulikuwa na utata wa nyaraka zake. Mengi mtasikia zaidi BBC leo jioni.

Anonymous said...

sasa hii stori ina faida gani kwetu?

Anonymous said...

Hapo ndipo mimi natofautiana na Born agains (Walokole) wao ni wabaguzi sana wanajitenga wanaona sisi wengine tuna dhambi na hatustahili kwenda mbinguni, wakati Yesu alikufa kwa ajili yetu wote na hakubagua mtu. Maana ya upendo wao wanaitafsiri kuwa ni kupendana wao kwa wao na sisi tuliogizani tutajijua wakati ukiwaangalia matendo yao wengi wao ni mabaya kuliko sisi wa duniani. Angalia huyo mlokole kulikuwa na sababu gani ya kumnunia jirani yake actually alichosema yeye ni sahihi mpagani aliye zaliwa upya sasa kuna kosa gani hapo. Well, huku kwa Mungu tutashangaana?We acha tu!

Anonymous said...

this's story if a propaganda.How comes can a Pagan be a born again?

Anonymous said...

lini utabadili na hilo!

kwani kila ukikutana na kituko una ondoka na jina..

sorry what is your name today ..bwana Born Again Pagan?

Anonymous said...

Fanyeni hima!!!!!!!!!!!!!

Haihusiani...lakini kwa wale wenye kutaka scholarship katika taaluma ya habari, fungueni,
http://www.journalism.berkeley.edu/press/african_journalists/

BAP

Anonymous said...

Mimi nilidhani wewe ulikuwa mpenzi wa bendi ya muziki iliyokuwa maarufu miaka yenu iliyojulikana kama BornAgainPagan.
Msomaji Kijana.

Anonymous said...

Wanakijiji:

Jina hili sitalibadili!

Sijui una maana gani ya neno 'propaganda"?

Natumaini kuwa mtu wa namna hiyo anaweza pia kuwa hivyo. Yaani kuzidisha imani yake kwa kile anachokiamini!

Bendi yetu pale Mlimani enzi hizo ilikuwa ikiongozwa na W. Mwabulambo --- kwa jina The Jungle Birds.

BAP

Anonymous said...

Uliyeuliza, "How comes can a Pagan be a born again?" yaani huyo pagan kwa kubobea katika imani ya paganism, hajambo!

Tutenganishe maana za dini na Ukristu. Ukristu ni dini; sio kila dini ni ya ukristu!

Kwahiyo, kama paganism ni dini, kuwa na wasifu wa a born again pagan ni kulokoka kulingana na imani ya paganism!

Anonymous said...

How comes can a Pagan be a born again?

Kiingereza safi:

How come a Pagan to be a born again?

Anonymous said...

Na wewe anon. Tue Apr 21, 01:47:00 AM EAT, Kiingereza safi kabisa:

"How can a pagan be a born again"?

or

"How comes a pagan be a born again"?

By the way, English isn't written in stone! I think, I should ask first, "Which English, you are talking about?" (lol!) as there are lots of English these days i.e Nigerian English, Zimbabwean, Canadian English etc!

What you think is your perfect English, can be grammatically undesirable to others! (fact!)

I'm here to be corrected.

Thank you.

Anonymous said...

i mimi wa Tue Apr 21, 01:47:00 AM EAT

Kwa bahati mbaya, samahani, nilikosea kidogo!!!!!!!!!!!


lakini tuache kufurunda lugha za wengine!

Kiingereza safi, narudia, narudia, narudia ni:

How come a Pagan be a born again?

Post a Comment