Leo kuna wengi waliokatisha usingizi wao wa mchana. Kila mtu alikuwa macho jijini Dar Es Salaam. Hata fundi saa huyu wa Mtaa wa Jamhuri nilimkuta akifuatilia kwa makini kinachoendelea Mbagala.
Nilisimama kona ya Jamhuri na Morogoro Road. Nilijiandaa kuvuka barabara kwa miguu kuelekea Kariakoo pale mlio wa kwanza wa bomu uliposikika. Saa yangu iliniambia ni saa 10:30. Milio mingine ikafuatia, si wengi walioshtuka.Kuna hata waliodhani kuwa inatoka kwenye majengo ya maghorofa yanayojengwa jirani. Haraka taarifa zikaanza kupatikana kuwa kuna mabomu yanayolipuka kwenye kambi ya jeshi Mbagala. Dar Es Salaam ikawa imebadilika. Kila kona kukawa na simulizi na watu wanaofuatilia kwa karibu. Majira ya saa nane ikaja taarifa za watu kuambiwa watoke kwenye majengo marefu. Niliona wafanyakazi wengi wakiwa nje ya ofisi zao. Shughuli nyingi zilisimama. Nilifika jengo la Jmall pale Mtaa wa Samora na kukuta maduka yamefungwa na watu wakiharakisha kutoka ndani ya jengo hilo.
Kuna taarifa za majeruhi na watu waliopoteza maisha yao katika tukio hilo. Tunasubiri taarifa zaidi za kuthibitishwa na vyombo husika na vile vile tathmini ya kilichotokea. Tunawapa pole wote walioathirika na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.




Tanzanian Shilling Converter
1 comments:
SUKHDEV CHHATBAR, Associated Press Writer, anataarifu:
ARUSHA, Tanzania – Huge blasts rocked an ammunition dump at an army camp in Tanzania's commercial capital on Wednesday, officials said.
Several people were feared dead, according to police spokesman Mohamed Mhina. The blasts lasted for about two hours and fires were still burning two hours after that, he said.
Local media reports said houses around the military base were on fire and several people had been injured. Local schools have called parents to come pick up their children. The blast rattled windows in houses 37 miles (60 kilometers) away, said resident Kate Esmail.
William Nchimbi, the deputy defense minister, said bombs, bullets and other ammunition exploded in an armory at the Bagala Army Camp in the coastal city of Dar es Salaam.
"We have formed a team to assess the source and the loss incurred," Nchimbi told journalists in the northeastern town of Arusha, where he was attending a regional leaders' meeting. He did not take any questions.
Ammunition dumps are volatile and easily ignited. The Bagala Army Camp is surrounded by civilian homes but is far from downtown Dar es Salaam.
Post a Comment