
" Twendeni Kibugumo na Mwanadilatu kwenye makao mapya!". Bila shaka kuna mnaoukumbuka wimbo huo wa enzi zile za operesheni ya kusaka wazururaji Dar Es Salaam. Vijana ' wazururaji' mjini walikuwa wakipakiwa kwenye malori na kupelekwa vijiji vya Gezaulole, Kibugumo,Mwanadilatu. Leo wenye kuishi huko wanaondolewa kwa ' vijisenti' na wakati mwingine kuondolewa kwa hila kupisha 'wawekezaji' wenye kuvutiwa na maeneo hayo ya kando ya bahari. Naam. Watoto na wajukuu wa 'Wazururaji' wale wa miaka ya 70 wanaandaliwa mazingira ya kurudi tena mjini 'kuzurura'!




Tanzanian Shilling Converter
10 comments:
mjengwa hivi unaweza kutukumbusha ama kutuulizia ni kiongozi gani aliye endesha hilo zoezi la gezaulole nakumbuka ilikuwa mwanzoni yamiaka 70
Hilo lilikua agizo la serikali, ya wakati huo, kutokomeza uzurulaji na vibaka vibaka. waende huko wakalime, kwenye makazi mapya yaliyoya wazi kwa ajili ya kilimo nguvu kazi. tatizo miaka hiyo huko kulikua polini na simba ni wengi. kama hamna roli liloting huko, hat akutoroka huwezi kwani njiani utakutana na wazee wa kazi simba, na hata hivyo kulikua hakuna nyumba nzuri za kujifadhi,ilikua ni patashika tu nguo kuchanika kwani simba wanazunguka hapo kijijini kucha, hizo ni story nilizopata kuzisikia za habari ya huko gezaulole, yaani weee, usije kugeza ukaenda huko mwenywe, labda fagio la chuma likupeleke, hakuna usafiri wa kutoka huko, labda ubatishe usafiri wa roli lilikuja kuwaleta, wazurulaji napo, kwa kuzamia wasukuone, manake kwa mguu simba si mchezo humo njiani, jinsi ya kuwaepuka.
Mimi katika kumbukumbu zangu zoezi hilo lilianzishwa na mzee wa mjini Songambele kipindi hicho alikuwa mkuu wa mkoa Dsm au Pwani.
kiongozi gani? kuna mwengine zaidi ya nyerere?
"biashara ya njugu na korosho sasa haitufai eeh!"
Dawa ya kukomesha uporaji wa ardhi ni kutumia sheria ya kurasimisha mali. Ndio wakazi wa maeneo hayo waungane na waifanye ardhi yao ndio rasilimali yao, watumie hichi kipengele cha kurasimisha hiyo ardhi na anayetaka kuiendeleza apeleke mtaji wake aingie ubia na wenyeji, wao mtaji wao ni ardhi yao!
Hiyo ndio dawa ya waroho wa rasilimali!
Mjengwa ukiweza watembelee wakulima wa Kisukuma maeneo ya huko, wanaolima viazi na mbogamboga kwa wingi. Wenyeji wapowapo tu, watu wanatoka mbali wanatumia ardhi vizuri wanapata pesa kwa kuzaliasha na kuuza mazao. Uzururaji na umachinga ni mambo la kujitakia na uvivu sio kweli kwamba hakuna kazi za kufanya.
Mjengwa umeisahau na Tegeta
du mwneyekiti umekumbusha mbali..nakumbuka niko darasa la pili pale Magomeni nikaona malori ya jeshi yakikusanya vijana wasio na vitambulisho huku mgambo na polisi wakitanda mitaani..wakati huo nilidhani Gezaulole ni karibu na mwisho wa dunia...hivyo Gezaulole ina maana ya "Iga uone" kwa lugha ya kizaramo?..
Ni "Mwanadilatu" au "Mwanabilatu" at that time ndio ilikua Tanzania, Chakula kwa wingi, Jingoistism ndio usiseme ila elimu ndio tulichemsha kidogo.
Post a Comment