Subscribe:

Thursday, April 30, 2009

" Hapa Ilikuwa Lazima Vumbi Litimke!"



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya vipande na mabaki ya mabomu vilivyookotwa katika makazi ya watu wanaoishi karibu na kambi ya Jeshi la wananchi Mbagala jijini Dar es Slaam ambapo nyumba kadhaa ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kupoteza maisha wakati ajali ilipotokea katika ghala la kuhifadhia silaha za kivita katika kambi hiyo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa usalama na utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali Paul Meela,Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Emmanuel Nchimbi,Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema.(Picha na Freddy Maro)
Reactions::

5 comments:

Anonymous said...

Nasikia ilikuwa VUMBI haswa sii mchezo.Mbona hatupati simulizi za wanakijiji wenzetu waliokuwa karibu.Simulizi zinaweza kutufundisha mawili matatu na kutupa uzoefu wa siku zijazo. Ile post ya fundi saa nilidhani kuna wanakijiji watatupa "kutoka kwa mdomo wa farasi" Poleni sana wakazi wa Dar.
VUMBI

Anonymous said...

Sipati picha ya Baghdad ilikuwaje, pole watz

Anonymous said...

Sijapenda mueonekano wa rais ni kama vile amekwenda kwenye part vile yaani mikono mfukoni duh hii mimi sijapenda kwa kweli.

Anonymous said...

Ukiondoa huyo wa kushoto (Meela)wengine wote wanaonekana kuchekelea utadhani kilichotokea ni jambo zuri.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

najiuliza ikitokea mengine yakaanza kulipuka wakati raisi yupo itakuwaje na atakimbilia wapi?

ni raha iliyoje kukutana naye anahema na kuhaha mitaani akitafuta uhai, si walinzi wake nao wanaokufa??

tehe tehe tehe

Post a Comment