Subscribe:

Friday, April 24, 2009

Kibera


Nairobi. Asante ya picha Eric Mchomu aliyetembelea Kibera hivi karibuni. Maelezo na picha zaidi za Kibera nitaziingiza.
Reactions::

9 comments:

Anonymous said...

Nia na lengo la picha za kibera ni nini mdau? Kama ni slums mbona kwetu bongo pia zipo zimejaa tele? Mnyamani,manzese kwa mfuga mbwa/uwanja wa fisi, mchikichini shule kwa bondeni kule hayohayo.
Nia la kutuonesha Kibera slum ni nini? Onesha slum zetu ili wadau watoe maoni nini kifanyike katika kuboresha makazi yetu.

DUNDA said...

Lawama hiyo au kuna uhaba wa maeneo ya kujengea

Anonymous said...

Yaaaap!!!
Haya ndo maisha, juu nyumba chini swiming pool. Hongera sana wana PNU+ODM.

Anonymous said...

Holy Moses
The governments have a responsibility to look after the citizens,allowing someone to live in such squalor is an infringement of the individuals basic human rights, a violation of the unwritten covenant between the government and the governed, there is a failure here to protect the citizen
Where are the community workers
Wakatabahu

Anonymous said...

he he he mjengwa hiyo picha wakenya watakataa watasema hapo sio nairobi

Anonymous said...

Ndugu zetu wa Kenya walitutangulia katika ukumbatiaji wa ubepari na walikuwa wakitubeza sana na ujamaa wetu. Nasi sasa tumejiunga na hiyo njia ya 'ukombozi'. Ndugu anayelinganisha Kibera na Manzese anahitaji kuonyeshwa picha zaidi. Manzese ni bora mara kumi. Kibera ndio matunda ya ubepari, na sisi baada ya miaka kama kumi hivi tutaanza kuziona kibera nyingi tu. Kwa hiyo tusiililie Kibera. Yaja! Kadri utakavyoona vikwanguaanga vinapaa angani, ndivyo na kasi ya kibera inavyoongozeka, Huo ndio ukweli wa ubepari bandia, ubepari unaolazimishwa katika mtandao wa ufukara!!!
mlalahoi

Anonymous said...

kaka mbona kwetu manzese, kwa Mnyamani/tandika nafuu ipo saaaaana wewe unayesema Kibera nenda kwzna upaone ndio utoe comment zako kunatisha pili hata usalama hakuna habari ndoo hiyo mdau.

Anonymous said...

Ni kweli unayesema Manzese unakosea sana, Kibera hali ni mbaya sana, hakuna hata vyoo, watu wanajisaidia kwenye mifuko ya rambo na kurusha hewani bila kujali litaangukia wapi hata kama ni kwa kichwa ya mtu. Watoto wanacheza ndani ya hayo maji machafu, kuna ukora na unyang'anyi wa hali ya juu, hakuna hewa safi na takwimu inaonyesha hilo ndilo eneo lenye makazi mabovu (slums) kuliko popote in Africa na ni la pili baada ya lile la kule India (anagalia movie ya Slumdog Millionnaire) so tushukuru Mungu Tanzania hatuna makazi ya aina hiyo kama Kibera.

Anonymous said...

jamani kibera nimefika huwezi fananisha na manzese au hata jangwani pakufurika. wanasema ni slum ya 2 ktk bara ya afrika na ya kwanza ni soweto south afrika.

Post a Comment