Timu za Watanzania za FC BONGO ya Finland na KILIMANJARO ya Sweden zitachuana rasmi siku ya Jumamosi tarehe 27.6.2009 katika viwanja vya Finnair Stadium Helsinki Finland.
Timu hizo ambazo zilichuana kwa mara ya kwanza mwaka jana huko Stockholm na Kilimanjaro wakabahatika kuwafunga Fc Bongo mabao 4-3 kwa taaabu.
Inasemekana kuwa Fc Bongo walichukiwa sana na uamuzi wa refa kuwapa bao la nne vijana wa kilimanjaro kwa mpira ambao ulikua ushatoka nje, pia baada ya mpira kuisha wakapewa pilau dume bila ya nyama,
Habari kutoka Helsinki zinasema kuwa Vijana wa Fc Bongo wanajinoa vibaya sana Kuwalipizia kisasi watani wao hao kutoka nchi ya jirani.
Kocha na Mlezi wa Fc Bongo Abdalla Ezza ameahidi kuwapa fundisho kubwa la kandanda kwa wageni wake hao wa Kilimanjaro, anaamini kikosi kilichoenda stockholm mwaka jana kilikua hakijatimia kwani wachezaji wake (Key Players) wengi hakuweza kusafiri nao kwani walikua ndio kwanza wamerudi makazini kutoka kwenye likizo zao za summer na hawakuweza kupata ruhusa makazini.
Nao Kilimanjaro wakizidi kujiamini kuwa wataweza kuwanyamazisha wenyeji wao huko Helsinki.
Habari zaidi kuhusu mechi hiyo tembelea website ya kilimanjaro hapa http://fckilimanjaro.snabber.se/
Pichani hapo Kilimanjaro na Fc Bongo kwa pamoja baada ya mpira kuisha mwaka jana huko Stockholm




Tanzanian Shilling Converter
0 comments:
Post a Comment