Egerton kuchuana na Wanigeria Zain Africa Challenge
* Hubert Kairuki kupimana na Waganda Jumatano
Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19, 2009
Chuo Kikuu cha Egerton kutoka Kenya kinatarajia kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Abubakar Tawafa Balewa kutoka Nigeria (leo, Jumatatu ya Aprili 20, 2009), katika mechi ya saba ya mashindano ya chemsha bongo ya Zain Africa Challenge (ZAC) yanayoendelea jijini Kampala, Uganda.
Pia wawakilishi wengine wa Tanzania, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki wanatarajiwa kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Busoga kutoka Uganda (Jumatano ya Aprili 22, 2009), mchuano utakaooneshwa katika televisheni ya ITV saa tatu usiku.
Tanzania sasa inawakilishwa na vyuo vikuu vinne ambavyo ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki, Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Teknolojia (IMTU) baada ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kutolewa wiki iliyopita Chuo Kikuu cha Lagos cha Nigeria katika mechi ya tano.
Mpaka sasa, vyuo vikuu vilivyofuzu raundi ya pili ni Jomo Kenyatta kutoka Kenya, Mzumbe, Mbarara kutoka Uganda, Ibadan Lagos na Valley View (Nigeria); ilhali vyuo vilivyoaga mashindano hayo ni Kwame Nkhuruma (Ghana), Chuo Kikuu cha Malawi (Malawi), Njala (Sierra Leone), SAUT na Copperbelt.
Licha ya kutupwa nje ya mashindano hayo, kila mwanafunzi ataondoka na
zawadi ya dola za Marekani 500 na vyuo vya kila kimoja kitaambulia dola
5,000.
Zain pia itatoa zawadi anuwai kwa watazamaji wa televisheni ambapo
watapata fursa ya kujibu maswali kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba
0789 555588. Vyuo hivyo vinashindania tuzo maridhawa kutoka Zain na
donge nono la dola 50,000 kwa chuo kitakachoibuka mshindi. Mashindano
hayo yameandaliwa na Zain ili kuinua kiwango cha elimu barani Afrika na
pia kuwapatia washiriki fursa ya kujenga mtandao na urafiki
utakaotadumu kwa muda mrefu.
Vyuo vikuu vingine vinavyoshiriki mashindano hayo na nchi zinazowakilisha katika mabano ni Chuo Kikuu cha Cape Coast, Chuo Kikuu cha Maendeleo, Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Chuo Kikuu cha Kenya na Chuo Kikuu cha Moi (Kenya).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Mzuzu, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Federal, Chuo Kikuu Akure, Chuo Kikuu cha Nigeria (Nigeria), Chuo Kikuu cha Kampala, Makerere, Chuo Kikuu cha Uganda Martyrs (Uganda) Chuo Kikuu cha Northrise na Chuo Kikuu cha Zambia (Zambia).
Mashindano ya ZAC yanaendeshwa kwa siku 31 katika mtindo wa mtoano na
yanashirikisha vyuo vikuu 32 kutoka katika nchi nane za Afrika zinazozungumza Kiingereza ambazo ni Sierra Leone, Ghana, Nigeria, Uganda, Kenya, Tanzania, Zambia na Malawi.




Tanzanian Shilling Converter
0 comments:
Post a Comment