TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Moi waitambia Kampala Zain Africa Challenge
* Muhimbili, Zambia kuchuana leo
Dar es Salaam, Jumanne, Aprili 28, 2009
Chuo Kikuu cha Moi kutoka Kenya juzi kiliibuka na ushindi dhidi ya Chuo Kikuu cha Kampala kutoka Uganda katika mechi ya tisa ya mashindano ya chemsha bongo ya Zain Africa Challenge (ZAC).
Chuo Kikuu cha Moi kiliwang’oa mashindanoni wapinzani wao Chuo Kikuu
cha Kampala, kwa kuwachapa kwa pointi 650 dhidi ya 540.
Mashindano ya ZAC yanaendeshwa kwa siku 31 katika mtindo wa mtoano na
yanashirikisha vyuo vikuu 32 kutoka katika nchi nane za Afrika zinazozungumza Kiingereza ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.
Mpaka sasa, vyuo vikuu vilivyofuzu raundi ya pili ni Jomo Kenyatta, Egerton kutoka Kenya, Ibadan, Lagos (Nigeria), Mzumbe (Tanzania), Mbarara, Busoga (Uganda) na Valley View (Ghana); ilhali vyuo vilivyoaga mashindano hayo ni Kwame Nkhuruma (Ghana), Chuo Kikuu cha Malawi (Malawi), Njala (Sierra Leone), SAUT, Hubert Kairuki (Tanzania), Copperbelt (Zambia) na Abubakar Tawafa Balewa (Nigeria).
Licha ya kutupwa nje ya mashindano hayo, kila mwanafunzi ataondoka na
zawadi ya dola za Marekani 500 na vyuo vyao kila kimoja kitaambulia dola
5,000.
Mashindano hayo yataendelea leo (Jumatano ya Aprili 29, 2009) kwa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili kutoka Tanzania kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Zambia kutoka Zambia, mchuano utakaooneshwa katika televisheni ya ITV saa tatu usiku.
Tanzania sasa inawakilishwa na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Chuo Kikuu cha Mzumbe na Teknolojia (IMTU) baada ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kutolewa.
Zain pia inatoa zawadi anuwai kwa watazamaji wa televisheni ambao wanapata fursa ya kujibu maswali kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0789 555588. Vyuo hivyo vinashindania tuzo maridhawa kutoka Zain na donge nono la dola 50,000 kwa chuo kitakachoibuka mshindi. Mashindano hayo yameandaliwa na Zain ili kuinua kiwango cha elimu barani Afrika na pia kuwapatia washiriki fursa ya kujenga mtandao na urafiki utakaotadumu kwa muda mrefu.
Vyuo vikuu vingine vinavyoshiriki mashindano hayo na nchi zinazowakilisha katika mabano ni Chuo Kikuu cha Cape Coast, Chuo Kikuu cha Maendeleo, Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Chuo Kikuu cha Kenya na Chuo Kikuu cha Moi (Kenya).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Mzuzu, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Federal,
Chuo Kikuu Akure, Chuo Kikuu cha Nigeria (Nigeria), Chuo Kikuu cha Kampala, Makerere, Chuo Kikuu cha Uganda Martyrs (Uganda) na Chuo Kikuu cha Northrise (Zambia).
Tuesday, April 28, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Tanzanian Shilling Converter
3 comments:
TANGAZO LILILOKUWA LIKIPITA KWENYE LUNINGA YA ITV AMBALO MUDA WAKE ULIKWISHA PITA SIKU NYINGI KUHUSU VYOU VIKUU LINA FAIDA GANI? PIA KIBAYA ZAIDI NI PALE WASOMI WANAPOANDIKA WELLCOME ALL! JE, TUTASHINDA CHEMSHA BONGO HIZI KWA MWENDO HUU?
Kwame Nkrumah!
ANDIKA SASA MATOKEO YA MUHIMBILI, SI TUMEYAONA, KWANINI HAUANDIKI?
Post a Comment