Subscribe:

Tuesday, May 26, 2009

CCM Washinda Busanda


Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Busanda Finias Magesa (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo mara baada ya kupata matokeo kwamba chama chao kimeshindwa kwenye uchaguzi huo.


MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lolesia Bukwimba ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Busanda baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine vilivyokuwa vikishiri uchaguzi huo mdogo wilayani Geita kwa kura 29,242 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho hata hivyo kimekataa matokeo, kilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 22,799.


Chama cha Wananchi (CUF) kilichopata kura 977 na cha United Democratic (UDP) chenye kura 271, viliingia mtini baada ya wagombea na mawakala wake kutoshiriki mchakato wote wa kuhesabu na kuhakiki kura katika hatua ya mwisho.


Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, Dani Mollel alisema idadi ya waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 135,163, jumla ya waliopiga kura ni 55,660, kura halali zilikuwa 53,309 na zilizoharibika ni 2,069. ( Chanzo na habari na picha: Michuziblog)
Reactions::

0 comments:

Post a Comment