Naomba na mimi nichangie walau mada hii. Kwa wanakao DC mimi ni Padri Mushi. Nadhani waliochangia hoja na kuona ina udini, kwa upande wangu sioni udini wowote. Nadhani ni kama utani mingine ambayo sisi Mapadri tumezoea kuisikia ikielekezwa kwetu. Mimi napenda watu waliogushwa na utani huu wachukulie ni utani wa kawaida, ni kama wanajua Philosophy basi waangalie joke hii in Philosophical approach kuliko kuendelea kuzozona kwenye hili, nadhani ni utani wa kawaida tu. Nadhani baadhi wamekasirika sababu hakuna utani unazungumziwa juu ya Uislam au wachungaji wa madhehebu mbalimbali...kwa wale waliogushwa ningependa mjue kitu kimoja important "we are catholics" hicho ni muhimu zaidi.....mtasikia matani mengi sana juu ya mapadri...
Fr. Mushi
Sunday, May 31, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Tanzanian Shilling Converter
8 comments:
Hello Fr. Mushi, ni wewe unayefundisha Georgetown? mimi sipo kwenye mzozo huu, napenda kuuliza kama unafundisha summer classes, napenda kuchukua kozi ya Social problem uliyofundisha last summer, je unafundisha summer hii pia?
Yaani wewe Father na usomi wako wote huo, unasema kuwa "mapadri tumeishozoea utani," sasa unafungua dirisha kwa watu kama kina Majjid kuendelea kuwatania... kama nyinyi mmezoea sisi waumini tunaumia sana. Tatizo kubwa nyinyi mapadri wenyewe waoga sana, ndiyo sababu Kanisa letu kila mtu anaweza kusema anachotaka. Haya bwana mmezoea kutaniwa.
Wewe Padri gani, unaogopa Waislamu.... nilidhani ungetetea hoja kumbe hupo upande wa Waislamu, unaogopa....
Mdau sitapenda kujadili hili tena. Haya ni mawazo yangu binafsi niliyotoa, usomi wangu ni wangu kaka yangu. Ndiyo maana kama umesoma comment yangu nimesema kuwa muhimu kwetu ni kuwa "we are Catholics" hichi ni muhimu, nadhani kama unaona kuna udini bado iwe changamoto kwako, kujifunza yale yote ambayo Yesu alifundisha kama kupendana, kusemehana, basi kwangu mimi sioni sababu yeyote kukasilika kwenye joke hiii, labda kama kuna jokes nyingine zilikuwa zimewekwa hapa kabla ya hii. Basi ni hivyo tu, na hayo ni mawazo wangu.
Nilishaanza kukubaliana na mawazo yako padre lakini hapa kwa kusema haya ni mawazo yako ndio uliponishanganya kabisa! Mwanzoni ulisema sisi mapadri tumeshazoea kutaniwa . Kumbe kwako sisi maaana yake ni mimi hii kali. Lakini pia ninyi mapadri hmuaminiki kabisa. Mnadai mnaishi useja lakini ni vichecheche wakutupwa. Mkiambiwa mnachukulia utani. Ukiwa DC bila shaka unafahamu vizuri sakata la yule padre wa Miami aliykuwa anafanya mambo ya aibu beach na demu wake.
WADAU WACHANGIAJI,
MIMI NAFIKIRI MTU YEYOTE ALIYEFIKIRIA KUWA MADA HII INA UDINI, HANA TATIZO, ILIMRADI HASHINIKIZI MAWAZO YAKE YAWE KIPIMO CHA KUFIKIRIA MJENGWA ALILENGA HUKO.
MIMI NAONA BAADHI YA WAKATOLIKI WENZANGU WALIOTOA MAONI NDIO WADINI. MAANA WAMESHAWEKA MADA KUPAMBANISHA UISLAMU NA UKRISTU (UKATOLIKI). NA KIGEZO CHAO SABABU MJENGWA NI MUISLAMU (LABDA). LAKINI MJENGWA BINAFSI HAJATAMKA MAHALA POPOTE KUHUSU DINI HIZI MBILI. NDIYO MAANA YEYE MWENYEWE HUSEMA, WAZO MOJA, TAFSIRI ELFU MOJA.
PIA KUONESHA YEYE HAKUMAANISHA UDINI WOWOTE, AKATOA MAONI PIA KAMA MCHANGIAJI, AKISEMA WAKRISTU HUSEMA ".........MGEUZIE NA SHAVU LA PILI", NA WAISLAMU "........JINO KWA JINO". MBONA HAPO HAMSEMI ANAWAKANDAMIZA WAISLAMU? NA MBONA KATIKA HILI HAMNA MWISLAMU ALIYEMLAUMU MJENGWA KUWA ANAUPENDELEA UKRISTU? MIE NADHANI KUNA SHIDA YA KUPAMBANUA MAMBO MIONGONI MWETU. NA HILI NI TATAZO KILA SEHEMU YA DUNIA.
HALAFU WATU WAMENG'ANG'ANIA FR. MUSHI NAYE AFUATE MKONDO WAO, ILIMRADI AWAFURAHISHE TU? JAMANI, HANA UHURU WA KUTOA MAWAZO YAKE KAMA YEYE? NYIE VIPI WAKATOLIKI WENANGU? NYIE SASA NDIO MNALETA SHARI BLOGUNI.
Mkurukutwa# 1 wa blog...
Nipo nje ya mjadala wa mada hii. FR. MUSHI naomba unipigie ukipata muda. Namba yangu ni (541)510.4841. Asante..
Mchangiaji wa hapo juu, ndiyo nitakuwa nafundisha summer II, lakini sifundishi Social Problem, nitakuwa nafundisha Philosophy. Dr. Anthony atakuwa anafundisha Social Problem, ni mwalimu mzuri sana, kama unataka kuchukua somo hilo. Mimi nitafundisha wakati Fall section 1 & 4. Summer hii nitafundisha masomo haya:
1 - Introduction to Ethics
2 - Philosophy of Knowldge
Karibu
Post a Comment