Subscribe:

Wednesday, May 20, 2009

IJUMAA YENYE TOFAUTI: KUTANA NA FREDDY!




IJUMAA YA KUKUTANA NA MWANDISHI

Wiki hii katika mjumuiko wetu wa kila Ijumaa katika Mkahawa wa Vitabu Soma tunawakaribisha kukutana na mwandishi wetu wa mwezi Mei ndugu yetu FREDDY MACHA. Mwandishi huyu ambaye pia ana fani kadhaa za kisanii atazungumzia kitabu chake cha “Mpe Maneno Yake” ambacho ni mkusanyiko wa visa mbalimbali alivyovishuhudia katika jamii alizowahi kuishi na kutembelea. Vilevile Freddy atatumbuiza kwa nyimbo, ghani na mashairi na pia atazungumzia kwa nini uandishi na fasihi ni muhimu kwa jamii. Freddy Macha ni mwandishi na mwanamuziki wa Kitanzania anayeishi nchini Uingereza. Kwa miaka zaidi ya 30 amekuwa akiandika makala mbalimbali katika magazeti yetu hapa nchini kuhusiana na mikasa ya kijamii.

Siku: Ijumaa 22 Mei, 2009 :

Muda: Saa Kumi na Moja Jioni- Saa Mbili

Mahala:Soma Mkahawa wa Vitabu

Tafadhali njoo na daftari au shajara yako. Njoo na maswali yako. Vitabu, matini na kanda za muziki zitakuwepo dukani. Nyama choma toka mgahawani itakuwepo
Reactions::

1 comments:

Anonymous said...

Sawa kabisa mwenyekiti ni furaha kubwa kuona mmeanzisha "vita" ya uzinduzi wa usomaji wa vitabu na magazeti.
kiwango cha usomaji wa magazeti na vitabu kwa vijana kimeshuka saana kwa wakati huu,turudishe furaha ya usomaji wa vitabu na magazeti kwa vijana,tunawahitaji warithi wenu wana habari kwa kizazi kijacho.

mickey@mail-online.dk

Post a Comment