Subscribe:

Thursday, May 21, 2009

Ma- Miss Wa Mjini



Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam.

KAMPUNI inayoandaa shindano la cha Miss Dar City Centre , Sisi Entertainment ya jijini Dar es Salaam , mapema leo ilitaja baadhi ya makampuni ambayo yamejitokeza kudhamini shindano hilo ambalo limepangwa kufanyika mwezi ujao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, John Doto , alitaja makampuni hayo kuwa ni kampuni ya simu Vodacom Tanzania,
Sycko Media , AMREF kupitia Angaza Zaidi na Global Publishers.

Kambi ya kitongoji cha Miss Dar City Centre ilianza siku ya Ijumaa jioni ambapo waandaaji , washiriki na mwalimu wa shindano hilo walijitambulisha kwa waandishi wa habari pale Ramada Hotel, Ilala , jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alitaja majina ya warembo ambao wamejitokeza kwenye shindano hilo ni Anne Moses (19), Neema Mashala ( 20), Caroline Izidor (18), Christine Ivan (22) na Husna Maulidy( 18).

Wengine ni Elizabeth Ernest (20), Emma James (22), Bhoke Misiwa (22), Mary Thomas (22), Judith Muro (20), Magreth Peter (21)Ziada Hemba (19), Mariam Othman( 19) na Emaster Charles (19). Washiriki wengine ni Jovina Michael (18), Mwantumu Yusuph (18), Golder Mmari(21), Catherine Rajabu (23), Everine Johan na Brender Alewis .
Warembo hao wameanza mazoezi ukumbini hapo chini ya mkufunzi wao anayeitwa Rehema R. Uzuwiy ambaye aliwahi kuwa Miss Ruvuma mwaka 1999.
Reactions::

0 comments:

Post a Comment