Mahabuba Yaja Kwa Kishindo
Na Mwandishi Wetu,
FILAMU iliyotamba vilivyo ya Mahabuba sasa inatarajia kuingia mtaani katika
sehemu yake ya pili. Hilo limejulikana juzi baada ya Khalfan Abdalah, Mkurugenzi wa kampuni ya Riyamy Production LTD ya jijini Dar es Salaam kubainisha hilo. Kampuni hiyo ndiyo yenye dhamana ya kusambaza filamu hiyo.
“Mahabuba Part II itaingia kwenye soko la filamu kwa mifumo ya VHS, VCD na DVD, hivyo natumia fursa hii kuwaomba mashabiki wetu wakae mkao wa kula kwa ujio wa filamu hiyo. Kama wanahitaji wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0754-665044 .” alisema Abdallah.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa wale ambao wanahitaji filamu hiyo wafike pale ofisini kwake mtaa wa Msimbazi / Magila karibu na klabu ya timu ya Simba.
Alifafanua kuwa ndani ya filamu hiyo kuna waigizaji wengi maarufu kama vile Single Mtambalike ‘Rich Rich’, Rose Ndauka, Godlivan Gordan na Jacob Steven (JB) ambao wamefanya kazi ya uhakika jambo linalomfanya awe na matumaini makubwa kwamba Mahabuba II itafanya vema sokoni.
Aidha, Abdallah alisema kuwa kampuni yake ipo mbioni kuingiza filamu nyingine tatu mpya ikiwemo Bongo Super Comedy 1 ambayo imechezwa na wachekeshaji nyota wote wa hapa Tanzania kama vile Senga, Bambo, Masele, Kiwewe, Mzee Majuto na wengineo.




Tanzanian Shilling Converter
0 comments:
Post a Comment