Subscribe:

Monday, May 25, 2009

Maishani; Kuna Wachache Wanaowekewa Ngazi...


Za Kupandia juu. Kuna wengi tunaolazimika kutafuta mbinu zetu wenyewe za halali za kupandia juu. Hata kama tutaishia njiani, tusichoke kujaribu tena na tena. Pichani ni Kinondoni Biafra leo jioni.
Reactions::

3 comments:

Anonymous said...

Fumbo mfumbie mjinga..mwerevu kama mie.......

nishapata jibu!?

nipe email nikutumie!

Anonymous said...

Asante sana mwenyekiti. Picha nzuri na ujumbe mzuri pia. Message sent!Message delivered!

Anonymous said...

Kaka umenifurahisha sana. Ungekuwa karibu ningekupa offer ya "diner la mchana"

On a serious note, huu ni ujumbe mzuri. Ni ujumbe mzito uliotolewa kwa njia rahisi kueleweka. Kwa kuwa wewe ni mwalimu, sisemi mengi. Unajua mwenyewe umetumia mbinu gani "ya kiualimu"

Ninachopenda kuongeza ni kwamba kuna watu wanakusubiri ukifika juu waanze kukuita FISADI. Nchi yetu imevamiwa na watu wanao haribu maana ya neno fisadi. Wengi kati ya hawa wamesahau kufanya kazi zao za halali wanaimba fisadi fisadi. Bahati mbaya, hata hao "mafisadi" wakipatikana na hatia, effect yake kwa maisha ya mtu mmoja mmoja ni ndogo sana. Na pia itachukua miongo kadhaa kurekebisha "shimo" lilotokana na wizi huwo.

Sina maana ya kukejeli jitihada za kupambana na ufisadi, la hasha. Maana yangu ni kuwakumbusha watu kufanya kazi za halali kujipatia riziki, hili liwe la kwanza na baadaye kwa ujumla wetu tupambane na ufisadi!

Ziko habari za kusikitisha sana za watu kupakana matope kutokana na kukata tamaa ya maisha. Itafikia mahali watu wataamua kuvaa tisheti "mimi fisadi" ili ku "dilute" kabisa hii dhana watu warudi kazini. Vinginevyo ni njia ya kuwapotezea muda watu maskini "wasahu shida zao" kwa wimbo wa kuburudisha wenye kibwagizo "fisadi, fisadi, fisadi" anaye imbisha ana miradi yake ya kiuchumi inayomlipa hata asipopokea au kutoa rushwa. Kila kitu kiwe na kiasi au kwa kidhungu, too much of any thing is harmful!

ANALYST

Post a Comment