
Na Mwandishi Wetu
Mtwara.
Hayo yamesemwa na mke wea Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Salma Kikwete alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani humu. Alizungumza na wanafunzi wa sekondari ya wasichana ya Mangamba katika manispaa ya Mtwara.
Mama Salma aliwaambia wanafunzi hao kuwa anazo taarifa zinazosema kuna mimba zipatazo 284 katika kipindi cha kuanzia Januari 2008 mpaka Machi 2009 mimba hizo zimepatikana katika shule mbalimbali mkoani humu.
Akitoa takwimu alizo nazo ni katika wilaya ya Mtwara Mjini mimba 11 shule za msingi sekondari 20 wilaya ya Mtwara vijijini msingi 55 sekondari 23 Tandahimba msingi 35 sekondari 48 Newala msingi 21 sekondari 9 Masasi msingi 14 sekondari 2 Nanyumbu msingi 27 sekondari 19. Jumla ya mimba zote za wanafunzi katika kipindi hicho ni 284
Amesema kwa wanafunzi hakuna sababu ya kukimbilia mapenzi iwapo huna elimu. Ni bora kwanza upate elimu hayo mambo mengine yafuate abadae. Amewataka wanafunzi kukataa kufanya mapenzi bali wazingatie elimu ndiyo ufunguo wa maisha yao ya badae. Katika shule hiyo mama Kikwete alitoa cheki ya shilingi 1,860,000/= kwa wanafunzi wanao lipiwa na kutunzwa na shirika lake la WAMA. Pia ametoa shilingi 1,000,000/= kwa shule hiyo kuwasaidia wanafunzi mbalimbali katika mahitaji yao.
Kabla ya hapo Mama Kikwete alizungumza na jumuia ya wanawake mkoani hapa UWT na kuwaambia wasiwaogope watoto wao wa kike kuzungumza nao kuhusu athari za kuputa mimba za utotoni wakiwa wanafunzi. Amewaasa akina mama hao kujitokeza katika kugombea nafsi za uongozi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vitongoji kule vijijini ili kupatikane idadi kubwa ya viongozi wa kuongoza nyazifa mbalimbali.
Katika nyakati za mchana mama Salma alizungumza na baraza la wazee katika ukumbi wa RC HALL na kuwaeleza kuwa wao kama wazee wana wajibu mkubwa wa kutatua matatizo yote yanapo tokea na kuyamaliza. Alishangazwa na hoja iliyo tolewa na mzee Mpeme kuwa kuna mpasuko ndani ya chama cha CCM na kufanya kuwepo na makundi mawili ndani ya chama kimoja hoja ambayo ilipingwa na mzee Rashidi Chilandwa na kumwomba mama Kikwete awaachie wazee mambo hayo watayamaliza wenyewe.




Tanzanian Shilling Converter
3 comments:
watakataeje mapenzi sasa watapataje wachumba, kutafutwe njia muafaka ya kulieleza jambo hilo si njia za mkato tu
Mkato wa ki-dini! kafundishwa na Mama Laura Bush majambo hayo!
Lakini picha na maelezo hayaamabtani. Tafuta picha nzuri...toa hiyo ya ughaibuni.
Picha ya Mama Salma peke yake.
Swala la mimba mashuleni ni complicated issue, kuna economic reasons, lakini ni vyema wanafunzi wafundishwe self respect na with self esteem. Hii itawasaidia wanafunzi kuheshim miili yao na kuwa tayari kusubiri muda muafaka wa kufanya mapenzi.
Pia social activities zitazowafanya wasichana na wavulana kushiriki pamoja zitawasaidia vijana kujielewa zaidi na kulinda heshima zao.
Post a Comment