Subscribe:

Monday, May 25, 2009

....Movement Of Jah People!



Na Mwandishi wetu
Dar Es Salaam.

Washiriki wa chama kinachoitwa Tanzania Rastafari Movement (TARAMO), saa tano asubuhi leo hii walikusanyika pale Posta ya zamani na kuanza kuadhimisha siku ya Ukombozi wa Afrika. Mratibu wa maadhimisho hayo, Ras Mponeja , ndiye aliyekuwa akitoa taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliojisogeza kuangalia kinachoendela maeneo hayo.

Kwa mujibu wa mratibu huyo maadhimisho hayo yamefanyika ili kuwaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga kupigana dhidi ya uvamizi wa wakoloni.

“Leo taasisi yetu imekusanyika hapa ili kuwaenzi babu zetu ambao walijitoa muhanga kupambana na wavamizi au wanyonyaji waliovuamia bara la Afrika na kuanza kutunyonya na kusababisha hali hii tulionayo leo. Hivyo, tumekusanyika hapa na shughuli yenyewe ndio hivyo unaona imeanza na bado kuna jamaa zetu kibao wapo njiani wanakuja, si unajua tena usafiri ulivyo tabu kwenye jiji hili.” Alisema mratibu huyo huku akifunga funga rasta zake .
Reactions::

4 comments:

Anonymous said...

Blessing be to those who remember there History-- Ras mponeja pamoja kaka

Anonymous said...

Nuff Nuff Respect man.

Rasta hapa.

Anonymous said...

Good guys...Tunakumbuka 25/05 ni siku ya kuzaliwa kwa OAU ambapo sasa inaitwa Africa Union..ni budi kuwaenzi waanzilishi wa organistion hii ingawa kazi bado ipo kuondoa huu ukoloni mamboleo...mpaka sasa bado tunanyonywa katika sekta mbali mbali..ni kweli inabidi kufungua macho..

Anonymous said...

Weya izi Jah Kimbute?

Post a Comment