Subscribe:

Friday, May 22, 2009

Sanda Nyeusi Yaja ( Si Bu-Sanda Nyeusi!)




Sanda nyeusi yaja

Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam.

BAADA ya jopo la wakaguzi kutoka Afrika Kusini lililokesha likiigakua filamu mpya inayotarajiwa kuleta mapinduzi ya filamu nchini ya Sanda Nyeusi, sasa filamu hiyo itaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa.
Habari kutoka kwa maafisa wa kampuni ya Kiu Investment LTD iliyotengeneza filamu hiyo zinasema kuwa, wakaguzi hao wameorodhesha sehemu kadhaa zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho ili iwe na ubora wa kimataifa.
“Filamu hii imetengenezwa kwa ajili ya kuuzika kimataifa, hivyo basi wameorodhesha sehemu zinazotakiwa kuboreshwa, kwa vile imetengenezwa katika kiwango cha kuoneshwa kwenye majumba ya sinema yenye hadhi ya kimataifa,” alisema Myovelwa Mfwaisa, meneja wa mandhari wa filamu hiyo.
Aliongeza kuwa, flamu hiyo imerudishwa studio kwa ajili ya kumaliziwa kuboreshwa sehemu zilizopendekezwa na wataalamu hao na baada ya hapo itakuwa sokoni nchini nzima na kwingineko duniani.
Filamu ya Sanda Nyeusi iliyorekodiwa mkoani Morogoro, imeigizwa kwa sehemu kubwa na Latifa Idabu, Issa Mussa ‘Cloud’, Korongo Hamis na Hashim Kambi.
Wakitoa maoni yao, wakaguzi hao waliotoka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa, Sanda Nyeusi ni hatua kubwa sana kwa medani ya filamu nchini kwa vile imekidhi matakwa mengi yanayohitajika kwenye filamu.
Reactions::

0 comments:

Post a Comment