
Je, ni makosa kwa mpiga picha endapo mtoto huyu ataliwa na tai?Au si kosa kwa mpiga mpicha kwani ametusaidia kufahamu ukubwa wa tatizo.Kwamba eneo hilo limekubwa na ukame na njaa kali kiasi cha mama kufa au kuondoka na kumwacha mtoto wake. Picha hiyo iliyopigwa na mpiga picha mahiri barani Afrika ( Marehemu Mohammed Amin) ndiyo iliyouamsha ulimwengu na kutambua kuwa Ethiopia ilihitaji msaada wa haraka kutokana na kukumbwa na ukame na njaa.




Tanzanian Shilling Converter
8 comments:
Masikini ya Mungu!huyu mtoto hakuomba kuzaliwa sijui aliteseka kiasi gani! Kazi yenu ngumu sana wanahabari, natumai huyo mtoto alipata msaada hata wa maji kutoka kwa mpiga picha.
Picha inatia huruma kupita kiasi
Hilo dege lenye uroho si tai wa kawaida huyo ni tai-mzoga ua vulture kwa kimombo
Wakatabahu
Mjengwa langu moja kujibu katika machache uliyouliza,
Hiyo picha haikupigwa na uliyemtaja bali Kevin Carter (marehemu) mnamo mwaka 1994. Picha hii ilimpatia ushindi wa tuzo ya Pulitzer lakini kutokana na lawama alishindwa kuzuia msongo wa mawazo na hatimaye aliazimu kujiua. Habari za Kevin Cater na picha hii na maisha yake zinapatikana katika tovuti hii http://www.flatrock.org
na hii http://www.mukto-mona.com/Articles/kevin_carter/sudan_child.htm
na nyingine nyingi kupitia google.com
majid hii picha nikiiona huwa nawaza siku nzima,mpiga picha alikuwa msouth Africa alienda huko ethiopia kipindi hiko njaa,watu mpaka wakawa wanakula watoto,watu wakafa ndio akaona iyo scene ,akapiga picha ambayo iliwashangaza watu wengi duniani,lakini huyo michuzi hakukaa muda alijiua kutokana na depression iliosababishwa na mambo aliyoyaona huko,ikiwemo hii picha.
Tai huyo hali kiumbe hai. Alikua akingoja mtoto huyo akate roho. Je mtoto huyo aliokolewa? Nina uhakika si Marehemu Mohammed Amin aliyepiga picha hii
The Vulcher is a very patient bird. Huwa ndege huyu hafuatilii kitu ambacho hakitakufa---ukiona ameanza kuwinda kitu ujue hicho kitu ni lazima kita kufaa ----- wapiga picha ni sawa na ile kitu inaitwa catch 22, the are damned if they do and they are damned if they don't. Lakini naona waandish wa habari wanafaidika na matukio mabaya--mfano mzuri ni kama hii picha
Siku zote nikiangalia hii picha najiuliza maswali mengi ambayo mpaka leo sijaweza kuyapatia majibu. Mojawapo ni kwamba, Je mpiga picha aliamua kwanza apige picha alafu baadaye ndio ajaribu kumpatia msaada kwa huyu mtoto au ilikuwa vipi?
Kama aliweza kubeba camera yake je alishindwa kumbeba huyu mtoto kumfikisha mahali ambapo angeweza kupatiwa msaada?
Au yeye kama mpiga picha hiyo haikuwa inamhusu, bali alikuwa pale kukamata "scenes" mbali mbali za janga lililokuwa linaendelea! Na huyu mtoto kwake alikuwa ni kama "subject" tu ... hakuwa akijali well being yake au hata hatma yake ... afe asife kwake sawa tu!
Picha hii ni mojawapo ya picha ambayo hunisikitisha sana kila niiangaliapo!
“Je, ni makosa kwa mpiga picha endapo mtoto huyu ataliwa na tai?Au si kosa kwa mpiga mpicha kwani ametusaidia kufahamu ukubwa wa tatizo. Kwamba eneo hilo limekubwa na ukame na njaa kali kiasi cha mama kufa au kuondoka na kumwacha mtoto wake.”
Swali na tamka hilo hapo juu ni mojawapo ya viini muhimu vya uandishi (journalism) na usambazaji (dissemination) wa habari na mawasiliano. Yote hayo mawili yana utata wake:
Mosi, wanahabari wanakabiliwa na maswali, matatizo, na kero za ki-taaluma. Wakati mwingine huwa ni vigumu sana kuweza kueleza habari bila kuingilia kati, ingawa wataalamu wa taaluma ya habari hujigamba kuwa mwanahabari hawezi kuwa sehemu ya habari!
Nitatoa mifano ili hilo la picha hiyo ya Kevin Carter hapo juu lieleweke vizuri:
Mwanahabari anaweza kumkuta chatu anambana mbuzi ili aweze kummeza mzima mzima. Je, mwanahabari atabakia kuona kisa au tukio hilo likitokea na yeye kulirekodi na huku akijua kuwa pengine huyo mbuzi ndio mwisho wake? Je, ataacha wajibu wake wa kutaarifu ili mradi amsadie mbuzi aliyepatwa na mkasa huo?
Pengine hiyo ni mifano fikirika tu.
Lakini kuna visa vya kweli vilivyotokea.
Katika magazeti yetu na blogu zetu tumeona picha za watu wamemtungika mtuhumiwa (kibaka wa simu ya selula) gurudumu shingoni lenye petroli au mafuta ya taa tayari kumchoma kwa moto. Je, mwanahabri atasimama bila kumsaidia huyo kibaka ili mradi tupate habari za tukio hilo? Je, ingekuwa vizuri kama atawapigia simu Polisi waje kusaidia?
Huko Vietnam, wakati Amerika ilipokuwa karibu kushindwa vita, mwanahabari Ed Bradley wa CBS TV (sasa marehemu) alikosolewa na wataalamu wa habari kwa kutupa maikrofoni baharini shauri ya kuonyesha moyo mwema (compassion) na wajibu kwa jamii (social responsibility) ili amwokoe m-Vietnam mmoja aliyekuwa karibu kuzama na huku amekaribia ufukoni akiogolea!
Kuna stori hapa Amerika sehemu za Kusini (Texas kama sikukosea) ambapo mtu mmoja alijimwagia mafuta ya taa na kujiwasha moto.
Na pembeni kulikuwepo na mpigapicha wa habari za TV ambaye aliendelea kupiga picha hizo bila kumsaidia huyo mnyonge!
Mpigapicha huyo naye kakosolewa na umma kwa kutoonyesha moyo wa huruma (compassion) na wajibu kwa jamii (social responsibility) kwa huyo mwenye kujichoma kwa mafuta ya taa!
Lakini habari za kuaminika ni kwamba mpigapicha hiyo, Kevin Carter, aliamua kutekeleza ya potelea mbali na “objectivism in reportage” kwa kumfukuza huyo tai (ndege) na kusalimisha maisha ya msichana huyo mdogo wa Sudan, kama alivyofanya mwanahabari Ed Bradley wa CBS TV hpao pwani ya Vietnam!
Wengine wataiona picha hiyo hapo juu ya Kevin Carter na kusema kuwa “here we go again”! Ni yale yale tu ya vyombo vya Nchi za Magharibi vyenye kupenda sana kutuandika katika miktadha ya Bara letu kuwa linakabiliwa na utitiri wa majanga yanayoanza na herufi ya D (katika Kiingereza): “Death, Debt, Despair, Despotism, Disaster, Disease, Drought, Dictators and Demagogies!”
Katika Nchi zaMagharibi, baadhi ya waandishi wa habari na wamiliki wake hujitetea kwa kujikita katika “biblia” ya uandishi wa habari (old school of journalism) wakidai kwamba sio wajibu wao kuwa wapigadebe (social engineering or cheerleaders of social or common good)! Kamwe waandishi wa habari hawawezi kuwa sehemu ya habari! Kwani kwa kufanya hivyo ni kupoteza “objectivism in reportage”!
Ndio, kuna hayo majanga. Afrika inalalamika kuwa kila moja la utitiri wa majanga hayo haliwekwi katika mktadha wake ili lieleweke. Vyombo vya habari vya ki-Magharibi vinashindwa kuyaeleza katika hali yake halisi. Kwa mtihani huu, vyombo vya habari vya ki-Magaribi vinashindwa kutekeleza kile ambacho Afrika inakiona kuwa ni sehemu ya “social responsibility” ya kuelemimisha!
Kwa kuwasahau wlalahoi wetu tunakuwa mithili ya huyo tai!
Born Again Pagan
Post a Comment