Subscribe:

Saturday, February 28, 2009

Nikifika Hapa Nimefika Iringa


Hata kwa kukimbia ni umbali wa nusu marathoni, nazimudu! Mbele kushoto ni uwanja wa ndege wa Iringa maarufu kama ' Nduli Airport'. Pichani ni jana jioni.
Reactions::

KILA LA HERI STARS YETU!

TUNACHOHITAJI LEO NI USHINDI, NA INAWEZEKANA. ZAMBIA NI 'FAVORITE' NA NDIO UDHAIFU WAO. SISI NI 'UNDERDOGS' NA NDIO NGUVU YETU KUBWA. BAO LA MAPEMA LITAPELEKEA TUPATE MASHABIKI WENGI WA IVORY COAST WATAKAOTUSHANGILIA. HILO LITAPELEKEA KUWACHANGANYA VIJANA WA CHIPOLOPOLO. TAHADHARI: TUSAHAU USHINDI ULIOPITA, HII NI MECHI MPYA!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Reactions::

Mpira Pasi!

Leo asubuhi nilishuka uwanjani kwa mazoezi ya timu ya watoto niliyoshiriki kuiunda, inaitwa G-Kids na mimi ni kocha msaidizi. Kocha wetu mkuu anaitwa Saitoti. Ndiye Scolari wetu wa Kimasai! Naam. Mpira una vitu vingi, kuna vya muhimu pia. Mpira ni pasi kwa maana ya kuondokana na dhana ya "Anakwenda Lunyamila, Lunyamila anakwenda!" Mpira wa kisasa unahitaji uwezo wa mchezaji katika vitu vitatu; umiliki wa mpira, ufundi na ubunifu. Anatakiwa kuwa na uwezo wa kumiliki mpira na siyo tu kusafirisha mipira ( ball transportation). Ni muhimu kwa mchezaji kukimbia na mpira na siyo kukimbiza mpira. Na katika yote hayo , uwezo wa kutoa pasi 'zenye macho'.
Reactions::

Mazoezi Na Mawaidha






Mazoezi ya mpira ina maana pia ya kutoa mawaidha kwa wachezaji. Pichani ni kijana Saitoti, kocha mkuu wa G-Kids. Miye kocha msaidizi ni mpiga picha pia wa timu!
Reactions::

Zantel Yafungua Duka La Kisasa Dar



Ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma zetu kwa haraka na ukaribu, Zantel imefungua duka la kisasa jijini Dar es Salaam. Duka liko katika jengo la Hadi Apartments, lililopo kati kati ya Jiji katika makutano ya Mtaa wa Morogoro na Libya eneo la Kisutu. Mstahiki Meya wa Jiji la Dar Es Salaam Alhaji Adam Kimbisa alikuwa mgeni rasmi siku ya ufunguzi.
Reactions::

Mambo Ya Leo Sweet Eazy!


Reactions::

Viriyala Tena!


Reactions::

Zain Yadhamini Tamasha La FESPACO

Zain yadhamini tamasha la FESPACO

* Lina lengo la kuendeleza utamaduni wa Afrika

Dar es Salaam, Februari 27, 2009

ZAIN, kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa huduma bora Afrika na Mashariki ya Kati, imetangaza kujitosa kudhamini tamasha maarufu la filamu na televisheni la Pan African Film and Television Festival of Ouagadougou (FESPACO) litakalofanyika Burkina Faso.

Tamasha hilo la kila mwaka, ndilo kubwa zaidi la kuendeleza utamaduni wa kiafrika barani Afrika na linahusu zaidi filamu za Afrika na waandaaji filamu wa Afrika. Mara ya kwanza tamasha hilo lilifanyika mwaka 1969, na mwaka huu litakuwa tamasha la 40 la FESPACO linalotarajiwa kufanyika kuanzia leo (Februari 28 hadi Machi 7, 2009) kwa sherehe za ufunguzi kwenye Uwanja wa Taifa wa Stade du 4-aout, mjini Ouagadougou.

Tamasha hilo la kimataifa limejijengea heshima barani Afrika na duniani kwa ujumla, lengo likiwa ni kupanua wigo wa medani ya filamu Afrika, kudumisha ushirikiano, kubadilishana mawazo na kupromoti kazi za filamu. Lengo lingine la FESPACO ni kupanua wigo na maendeleo ya sinema Afrika. Akizungumza kuhusu udhamini huo, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zain Afrika, Tito Alaiaid alisema: "Tunaona fahari kuwa wadhamini wa tamasha hilo kabambe.

Udhamini huu unaonyesha jinsi Zain inavyowajibika kusaidia jamii na kupromoti sanaa na utamaduni wa Afrika. Tunaamini Afrika itafikia malengo na Zain tutaendelea kusaidia kadri ya uwezo." Katika udhamini huo, Zain itatoa huduma ya simu katika tamasha hilo na kupamba uwanja kwa ajili ya sherehe za ufunguzi na kufunga ambapo kutaonyeshwa filamu za kitamaduni za Afrika. Kwa miaka kadhaa sasa, Zain imekuwa ikidhamini matukio mengi yanayohusu utamaduni na elimu Afrika ikiwa ni pamoja na tamasha la kimataifa la kusherehekea Nelson Mandela kutimiza miaka 90 jijini London, kudhamini tamasha la MTV Africa Music Awards (MAMAs).

Kwa kushirikiana na Ericsson na Earth Institute, wamesaini mkataba wa kutoa huduma ya mawasiliano ya simu selula na intaneti katika Mradi wa Vijiji vya Milenia unaohusu watu 400,000 katika nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Pia Zain inadhamini mashindano ya vyuo vikuu ya Zain Africa Challenge, ZAC, yanayoendeshwa kwa njia ya televisheni yanayogusa mamilio ya watu katika nchi nane barani Afrika.

Katika tamasha la FESPACO ambalo kauli mbiu mwaka huu ni "Simena za Afrika: kukuza utalii na utamaduni", Zain pia imeshirikiana na RFI na BBC, kudhamini zawadi maalumu yenye thamani ya dola 4,000 itakayotolewa kwa washindi. Tamasha la mwaka huu limeandaliwa kwa heshima ya Ousmane Sembene, mmoja wa waasisi wa kutengeneza filamu za kiafrika na mwasisi wa FESPACO, aliyefariki dunia Juni 9, 2007.
Reactions::

Hii Ndio Milima Ya Nyang'oro



Ni mirefu, yenye kona kali na msitu mnene. Pichani ilivyoonekana jana jioni.
Reactions::

Kero Ya Maji: Jamani Wahandisi Tukae Chini...

Mjengwa,

Asante kwa kuteletea picha humu kijiji. Jamani Wahandisi tukae chini tufikiri jinsi ya kupunguza kero hii. Mnaonaje tukianzisha michango kwaajii ya kutatua kero. Mbona harambee za harusi zinafanikiwa tutashindwa kero za jamii? Jamani tufikiri hili kwa makini.Naimani kabisa tunaweza tukilitole macho.

Mdau Pacific Northwest

(samahani usitoe email yangu)
Reactions::

Asali Mbichi


Inauzwa kuanzia shilingi elfu tatu kwa chupa ya konyagi. Ni kati ya Singida na Dodoma kabla ya kufika Manyoni.

Reactions::

Daira Bar!

Utemini, Singida.
Reactions::

Utemini


Singida Mjini, leo asubuhi.
Reactions::

Kuna Wanayotafuta Maji Kama Dhahabu


Picha hii niliyoipiga leo itabaki katika kumbukumbu zangu za safari ya Kanda ya Kati. Mama huyu wa kijiji cha Fufu ni kielelezo cha tatizo kubwa la maji linalowakabili wengi.
Reactions::

Untitled


Kijiji cha Chipogoro, Dodoma, leo alasiri.
Reactions::

Friday, February 27, 2009

NIMERUDI IRINGA JIONI HII

Ni baada ya kukamata usukani tangu saa kumi na moja asubuhi leo hii nikitokea Shinyanga Mjini kupitia Tabora, Singida, Dodoma na hatimaye Mtera hadi Iringa. Nimefurahi sana kurejea nyumbani Iringa baada ya safari hii ndefu iliyonipitisha kwenye vumbi, tope, mashimo na lami. Nimeona na kujifunza mengi. Nimekutana na watu wengi wema. Na hakika, 'watani' zangu Wanyamwezi na Wasukuma ni watu wema na wakarimu mno. Sikulijua hilo hadi nilipofika Unyamwezini na Usukumani. Na wapi tena kwenye wasichana warembo kama Unyamwezini na Usukumani?Tatizo hata zizi la mbuzi sina, vinginevyo ' SAMMA' ingekuwa historia!
Reactions::

Thursday, February 26, 2009

Nimeingia Shinyanga Mjini

Jioni ya leo nikitokea Kahama. Shinyanga Mjini imetulia. Nimevinjari mitaani hata usiku wa saa tatu, kuna taa za barabarani pia.
Reactions::

Milima Na Mabonde Ya Sekenke


Ni kati ya Sindida na Tabora
Reactions::

Kahama

Reactions::

HONGERA SANA STARS YETU!!

Ni kwa ushindi wa kutia matumaini dhidi ya Ivory Coast.
Reactions::

Nimefika Kahama Shinyanga

Jioni ya leo. Ni baada ya kufanya kazi katika vyuo vya Mwanhala na Nzega. Kahama ni mji mdogo uliochangamka. Kuna mtu ananiambia Kahama ni wilaya inayokua kwa kasi sana baada ya Kinondoni.
Reactions::

Wednesday, February 25, 2009

Kijiwe Cha Kahawa Chenye Tofauti!

Nimekikuta leo Nzega. Wanaume wanakaribishwa.
Reactions::

Wanaelekea Sokoni

Nzega
Reactions::

Mitaa Ya Nzega

Leo asubuhi.
Reactions::

Mboga Na Matunda Ya Asili

Nzega, Tabora leo asubuhi.
Reactions::

Tabasamu La Kinyamwezi!

Nzega hapa.
Reactions::

Waweja Kuzugha!

Nilifika Nzega jana usiku wa saa mbili. Nzega ni ya watani zangu Wanyamwezi. Nilipofikia niliwakatilia watani zangu kuwa sitakula nyama ya kuku wa kuchoma wala chipsi maana hakukuwa na chakula kingine. Niliwaagiza watafute Nzega nzima nyumba ya mwoka chapati. Kwamba waje na chapati ili ninywe chai na chapati. Iliwezekana kama inavyoonekana pichani. Waweja kuzugha! Ina maana ya ' asante kwa kupika!'
Reactions::

Mnaojua Kifini Humu Ndani Kuna Biashara Gani?

Nimeyakuta maandishi hayo kijijini Msingi, Iramba Mashariki jana jioni.
Reactions::

Nimefika Nzega

Jana usiku nikitokea Singida.
Reactions::

Inakumbusha Mbali


Kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Singida Bw. Mlade. Kulia ni Bw. Kimweri ambaye alipata kuwa mkuu wa FDC ya Msingi, Iramba Mashariki. Kwa sasa Kimweri ni diwani wa kata ya Msingi (CCM). Mwezi Julai mwaka 1991, kwa mwezi mmoja nilishiriki kwa kujitolea ujenzi wa shule ya msingi ya kijiji cha Msingi ambapo pia ndipo kilipo Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Msingi. Jana nilipata tena bahati ya kutembelea kata ya Msingi, Iramba Mashariki. Nilifika Chuoni Msingi pia na kuongea na wakufunzi na washiriki wa kozi. Kata ya Msingi sasa ina Sekondari pia.
Reactions::

KILA LA HERI STARS YETU

Katika mechi muhimu dhidi ya wenyeji Ivory Coast hii leo. Pichani ni Kondoa siku ile Stars ilipopambana na Senegal.
Reactions::

Hindi Lina Utamu Wake!

Likichomwa likachomeka. Pichani ni Kondoa Mjini.
Reactions::

Tuesday, February 24, 2009

Singida Ina Maziwa Yake!


Pichani ni ziwa Singidan, lingine ni Sindai. Singida Mjini inazidi kupanuka na kupendeza.
Reactions::

Monday, February 23, 2009

People's Club: Aliko Alianzia U-Dj Hapa!


Hapa ndipo mwenzetu Aliko Mwakanjuki alipoanzia U-Dj wa muziki. Ni Singida Mjini. Picha hii ni ya leo alasiri.
Reactions::

Kwa Mtoro- Singida Mjini!

Leo alasiri.
Reactions::

Mama Na Mwana!


Ndoroboni, Kwa Mtoro, Kondoa.
Reactions::

Dr. Asha- Rose Migiro Wa Kesho!


Leo nilitembelea Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, Kondoa. Dr. Asha- Rose Migiro akiwa Waziri wa Maendeleo Ya Jamii Jinsia Na Watoto alifika Munguri Agosti 14, 2001. Bweni la wanawake ( pichani) limeitwa kwa jina lake kama kumbukumbu. Mkuu wa Chuo hicho mama Anna Mokoki amenieleza wako mbioni kuandika jina kamili la ' Dr. Asha!'
Reactions::

Ubatizo Huu!

Kwenye moja ya vijiji vya njiani, Kondoa jana Jumapili.
Reactions::

Sunday, February 22, 2009

Dodoma- Kondoa Road


Ni sehemu ya Great North Road.
Reactions::

Kondoa Hapa


Habari kubwa hapa Kondoa hii leo ni tukio la jaribio la majambazi kuliteka basi la Machame Investiment kwenye pori la Mtunguti barabara ya Dodoma- Arusha. Ilikuwa jana asubuhi majira ya saa moja. Kwa kawaida mabasi yanayopita pori hilo yanasindikizwa na askari. Katika tukio hilo zilipigwa risasi tisa na dereva wa basi alijeruhiwa mkono wa kulia kwa risasi. Hata hivyo, kwa ujasiri mkubwa dereva huyo aliweza kuendesha basi hilo kwa kuvuka mawe yaliyopangwa barabarani. Leo majira ya saa nane nilipita kwenye kizuizi cha askari kuingia pori hilo. Hapo nilipata kwa mara ya kwanza taarifa ya tukio hilo. Askari yule niliyemkuta kwenye kizuizi alionekana hakuwa tayari kusindikiza gari nililoendesha bila kupewa chochote. Badala yake alinidanganya kuwa kuna msafara wa magari matatu na basi moja uliondoka kwenye kizuizi hicho dakika tano zilizopita na kwamba ningeweza kabisa kuwawahi. Kumbe, hakukuwa na kitu kama hicho. Kwa bahati niliweza kuvuka pori hilo salama ingawa nilijawa na mashaka makubwa.
Reactions::

Kijiwe Cha Kahawa Kondoa


Nimefika Kondoa jioni hii. Kondoa imetulia. Nimepata nafasi ya kutembea mitaa ya Kondoa ikiwa ni pamoja na kukaa na kupiga gumzo na wenyeji kwenye moja ya vijiwe vya kahawa karibu na stendi kuu ya mabasi.
Reactions::

Mtoto Mbele Baba Nyuma!

Kijiji cha Matomondo, Mpwapwa, jana Jumamosi.
Reactions::

Kuijenga Nchi Yetu Ni Jukumu Letu Wenyewe




Watanzania tumeanza kujijengea mazoea ya kunung'unika. Jana nikiwa njiani kwenda Chisalu niliguswa sana na kitendo cha akina mama watano niliowakuta wakijitolea kufukia mashimo ya barabara inayopita kijijini kwao. Kwao ilikuwa ni kazi ya maendeleo katika siku ya Jumamosi. Wamelitambua jukumu lao, wamelichukua bila kusimamiwa na mtu yeyote. Tukipunguza kunung'unika na kuanza kuchukua hatua katika maeneo yanayotuzunguka, basi, tunaweza kupiga hatua za maana za maendeleo.
Reactions::

Maji Ya Mtoni

Chisalu, Mpwapwa, Dodoma.
Reactions::

Maonyesho Ya Magari Japan



Kaka Jana Hapo Mjini Yokohama Kulikua Na show Kali ya Magri. ili Kua Hatari mno. Hata Mimi nilikuepo moja ya gari ninayosukuma Japan . Iko hapo
asante
Reactions::

INSHALLAH NA KILA LA HERI STARS YETU

taifa stars na senegal leo huko ivory coast
Na Florian Kaijage, Abidjan
Taifa Stars leo inashuka katika dimba la Felix Houphet Boigny jijini hapa kuwakabiri Simba wa Teranga, Senegal katika mchezo wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan) huku ikizungukwa na hisia za kulipa kisasi kwa Taifa Stars.

Mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya pili ikitanguliwa na ya ile ya ufunguzi kati ya wenyeji Ivory Coast na Zambia itachezwa saa moja usiku kwa saa za hapa sawa na saa nne za usiku za Afrika Mashariki.

Ni kisasi kwa hasa kwa Taifa Stars kwa sababu March 24, 2007 Stars ilichapwa mabao 4-0 mjini Dakar wakati wa kampeni za kufuzu kwa fainali za Afrika zilizofanyika 2008 huko Ghana na katika mchezo wa marejeanp jijini Mwanza Stars iliwakosa Senegal kwa kulazimishwa sare ya 1-1 Juni 2 2007 jijini Mwanza. Nizar Khalfan alifunga bao la dakika ya 17 lakini Demba Ba akaisawazishia Senegal zikisalia dakika 17 mpira kumalizika. Mbele ya mashabiki zaidi ya 20,000 akiwemo Rais Jakaaya Kikwete.

Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha Stars walioshiriki michezo hiyo miwili bado wapo kama vile Shadrack Nsajigwa, Salum Swed, Nizar, Haruna Moshi, Athuman Idd Shabaan Nditi, Henry Joseph toufauti na Senegal ambayo wachezaji we ngi wa kikosi cha kwanza wanasakata kandanda barani Ulaya.

Na ifahamike kuwa hicho kipigo cha mabao 4-0 ndicho kikubwa zaidi kwa Stars tangu Maximo aanze kibaru cha kuinoa timu hiyo Agosti 2006.

Hata hivyo Stars inashuka dimbani bila viungo wake wawili Athumani Idd ambaye Maximo anasema hayuko fiti asilimia 100 na Kigi Makasi mwenye kadi mbili za njano huku Godfrey Bonny ambaye alikuwa akisumbuliwa na tumbo akianza, inatarajia kushuka ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi.

Stars ilikuwa ya kwanza kutua katika mji wa Abidjan kwa fainali hizo za kwanza na wachezaji wake wameonesha kuwa na ari ya mchezo hasa kutokana na mazoezi waliyoyafanya wakichekelea hali ya hewa inayofana na ya Dar es salaam kutoka na nyuzi nyoto kufikia sentigrade 29.

Mbrazili Maximo alisema:’kushinda mchezo wa kwanza ni muhimu mno ili kupandisha ari na hamasa ambayo tayari iko juu miongoni mwa wachezaji wangu’.

‘Tanzania sasa inaapanda kufanikiwa kushiriki mashindano makubwa baada ya miaka 29 kieleelzo kuwa nchi iko katika mwelekeo wa kuwa moja ya miamba ya soka sote tinawajibika kuonesha kuwa kufuzu kwetu kwa fainali hizi haikutokea kwa bahati bali kazi kubwa ilifanyika’ alisema Maximo ambaye meci ya leo itakuwa ni 42 kwake kuongoza timu ya Taifa.

Kulingana na mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika tangu timu kuwasili hapa Abidjan ukiondoa wachezaji ambao hawawezi kushiriki mchezo wa leo ni dhahiri kuwa kikosi kitakuwa kama ifuatavyo:

Shaaban Dihile, Nsajigwa, Juma Jabu, Swed, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Geofrey Bonny, Henry Joseph Nizar, Haruna, Jerson Tegete na Mrisho Ngasa.

Mchezaji chipukizi Mwinyi Kazimoto aliyevaa jezi ya Stars kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Zimbabwe anatarajia kuwapo katika benchi la wachezaji wa akiba pamoja na Deo Munishi, Kevin Yondani Nurdin Bakari Mussa Hassan Mgosi, Abdi Kassim na Amir Maftah.
Reactions::

Kipanya

Reactions::

Ugali Wetu Wa Kila Siku

Asante ya picha: Clarence Mahunda, Tanga.
Reactions::

Raha Ya Tanga!

Wagosi wanakwambia ukitaka kufaidi kama watoka Dar shurti Tanga wende na Raha Leo.Hapa ni Visiga na hili ni mojawapo.Kwa nyuma limeandikwa CHUDA RAHA.Chuda ni moja ya vitongoji vya Tanga mjini.Karibuni mtembelee Tanga.
Imeletwa na mwenzetu Clarence Mahunda, Tanga
Reactions::