Subscribe:

Tuesday, March 31, 2009

Mpunga Huo, Usipouchagua....


Utaula wa chuya!
Reactions::

Mheshimiwa Mwenyekiti


Pichani ni Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania waishio Mysore, India. Anaitwa Mwinga Mungwe. Alichaguliwa jana jioni. Hongera sana!
Reactions::

HUU NDIO MSIMAMO WETU





TAHARIRI: HUU NDIO MSIMAMO WETU
NDUGU Msomaji, leo Jumanne Machi 31, 2009 , Tanzania kama nchi imeendelea kufurahia uhuru wa kutoa maoni kwa njia ya vyombo vya habari. Hii ni kwa kuwa na gazeti jipya na huru la ‘Kwanza Jamii’. Hivyo basi, unalolisoma sasa kwa mara ya kwanza ni gazeti la ‘ Kwanza Jamii’. Kama ilivyo kwa jina lake, ni gazeti la jamii, ni gazeti lako.

Kwanza Jamii ni gazeti la kijamii lililoanzishwa na wanajamii kwa ajili ya wanajamii wa Kitanzania ndani na nje ya mipaka yetu. Pamoja na nia ya kibiashara kwa maana ya kupata faida, waanzilishi wa gazeti hili wamesukumwa na vipaumbele vikuu viwili; mosi, tunaamini kwamba nchi hii imejaaliwa kuwa na vyombo vingi vya habari vinavyojumuisha redio , magazeti na televisheni.
Na tunaamini pasi na shaka, kuwa kuna Watanzania wengi hawapajapata nafasi ya kutosha kutoa maoni yao kwa nia ya kushauri, kukosoa, na hata kupongeza juu ya mustakabali wa mwenendo mzima wa utendaji wa vyombo mbalimbali vya usimamizi wa rasilimali za umma na usimamizi wa mifumo mbalimbali ya kiutawala.
Hivyo basi, Kwanza Jamii tuna azma ya kupanua wigo kwa Watanzania kupata nafasi hiyo ya kupata habari, kuelimika na kuburudika . Si hivyo tu, na hata Watanzania wenyewe, kupitia kalamu zao, kompyuta na simu zao, kusema yale wanayotaka kusema kupitia gazeti hili. Maana, Kwanza Jamii ni gazeti lao bila kujali tofauti za kikabila, kidini na kirangi.
Pili, zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini. Kwanza Jamii litashirikiana kwa karibu na ndugu zetu hao ili kubaini kero, karaha, taabu na hata raha wanazozipata kwenye maeneo yao hayo. Ingawa jambo hilo lina gharama, lakini tunaahidi kujitahidi kuwafikia Watanzania wenzetu hawa kwa namna moja au nyingine.
Tunajua , kuwa wapo wenzetu mahodari wa kusema bayana kwa nia njema, lakini pia, miongoni mwa asilimia 80 hiyo ya Watanzania, wapo wasioridhishwa na mambo fulani fulani kwenye mfumo wetu wa kimaisha. Hata hivyo, kwa sababu mbalimbali, hawana uwezo wa kunyanyua kalamu au ndimi zao na kukemea. Hawa tunawaomba wasifadhaike na kukata tamaa.
Kwanza Jamii tumejipanga na tumewaletea wachambuzi wanazuoni na wasio wanazuoni. Ni wachambuzi mahiri kabisa katika maeneo yao. Na tuamini, kuwa wapo tayari kuwaondoa upweke na kusemea mioyo yenu kwa nia njema kabisa ya kushiriki kuijenga nchi yetu. Maana, hawa ni wasomi waliosomeshwa kwa kodi za wanajamii walio wengi wa kule vijijini. Ni jukumu la wasomi hawa kuanza kutumia maarifa yao kuisaidia jamii pana walioiacha nyuma yao.
Na katika zama hizi za kuwafichua wabadhilifu wa mali za umma waliojipatia jina jipya la mafisadi, inasemwa mitaani, kuwa mafisadi hao wameanzisha, na wanaendelea kuanzisha na hata kuvifadhili vyombo vya habari na wanahabari wenyewe kwa nia ya kufunika maovu yao. Sisi- Kwanza Jamii, tunaomba tujipambanue kungali mapema, kuwa gazeti hili halikuanzishwa kwa faida iliyotokana na shughuli zozote za kifisadi.

Hivyo basi, tunatoa wito kwa wale wote wanaojijua, kuwa wanachuma mali zao kwa njia za kifisadi, kuwa gazeti hili si mahali salama pa kukimbilia ili kuwapakizia ubaya wale waliobaini unyang’au wao. Kwanza Jamii tunaahidi pia kushirikiana na wale wote wanaokandamizwa kutokana na mfumo wa uongozi kwenye vijiji vyao, mitaa yao, makazini na hata majumbani mwao. Ingawa , katika kufanya hivyo, hatuko tayari kuingilia uhuru wa familia bila utashi wa wahusika. Kwamba tutazingatia miiko ya taaluma ya uandishi wa habari. Na tukumbuke, hakuna uhuru usio na mipaka.
Kwanza Jamii tutapigana bega kwa bega na wale wote walio tayari na wenye dhamira ya dhati ya kupambana na maovu katika jamii yetu. Kwanza Jamii tutakosoa kwenye makosa na tutashauri penye mkanganyiko. Lakini pia hatutasita kusifu na kupongeza panapostahiki.
Kwanza Jamii hatutamwonea mtu au taasisi yeyote ile kwa dhamira na makusudi ya kutaka kuonea. Na katu hatutomwogopa wala kumwonea aibu yeyote atakayekiuka utaratibu wa kisheria tuliojiwekea katika mfumo wa maisha yetu, uongozi wetu, siasa zetu na tamaduni zetu .
HUU NDIO MSIMAMO WETU.
Reactions::

Viriyala Tunaye Kwenye Kwanza Jamii!


Kijana machachari Ahmed Viriyala kila itapowezekana, ameahidi atakuwa anatoa mchango wake kwa jamii kwa katuni zake za kuburudisha na zinazobeba ujumbe wa kufikirisha kama hiyo ya leo kwenye ' Kwanza Jamii'.
Reactions::

Mwanzo Mgumu!


Mwonekano wa ' Kwanza Jamii' sivyo vile ilivyotakiwa iwe. Mast-head hiyo ni ya upande wa nyuma.Ni makosa ya kiufundi! Hutokea binadamu akajikuta amevaa shati nje ndani na hasa nyuzi na rangi za shati zinapowekwa na kufumwa kwa umahiri!
Makosa hayataisha, ila tunaahidi toleo lijalo tutayapunguza. Kwanza Jamii litawekwa kwenye mtandao pia, tuko katika kukamilisha details za mwisho mwisho kabla ya kulirusha hewani!
Reactions::

Jukumu Ni Lile Lile


Katika siku tatu zilizopita mimi na wenzangu tulikuwa na harakati nzito za usiku a mchana kuhakikisha kuwa, japo katika mazingira magumu, ' Kwanza Jamii' , gazeti la jamii,linawafikia wanajamii katika tarehe tuliyowaahidi. Shukrani za pekee kwenu nyote mlioonyesha utayari wa kuandaa kazi zenu na kuzituma kwangu zikiwa na ubora mkubwa. Mmechukua muda wenu kufanya kile ambacho jamii ya Watanzania itanufaika nacho. Toleo la kwanza la ' Kwanza Jamii ni mwanzo wa maandalizi ya toleo lijalo, tutaendelea kupokea kwa moyo mmoja, michango yenu ya makala. Ahsanteni sana.
Reactions::

Timu Ya Kwanza Jamii Hii Hapa!


Wengine mnakaribishwa sana kuchangia fikra zenu zenye kujenga na kwa ustawi wa nchi yetu.
Reactions::

Ujumbe Wa Kitaifa!

Reactions::

Monday, March 30, 2009

Sunday, March 29, 2009

Mambo Ya Japan Haya!


Mkuu hapa Japan hawa jamaa wakiwa bara barani wanaogopewa kuliko hata simba nakuambia. Hapa Driver 's wote watafuata sheria, No simu no speeding na wote wamefunga Mkanda.
Reactions::

Saturday, March 28, 2009

Hesh...maaa!


Mikumi, jana.
Reactions::

Vipi Mzee?


Mikumi, jana.
Reactions::

Hapa Biashara Ya Magazeti Imeharibika!


Kwa siku ya jana. Gari la EMS lilikatika T-belt saa kumi alfajiri usiku wa kuamkia jana. Niliwakuta hapo Mikumi majira ya saa tano asubuhi. Ilimaanisha wasomaji wa magazeti kwa mikoa ya Iringa na Mbeya wangeyapata jioni au kutokuyapata kabisa. Pichani ni Bwana Hamisi ( mbele) na Sakala wakiwa katikati ya mbuga ya Mikumi.
Reactions::

Friday, March 27, 2009

Kijiwe Cha Demokrasia


Vyama vyote vimewakilishwa. Mwangata, Iringa.
Reactions::

Ndugu Waishio Japan

NDUGU WATANZANIA WAISHIO JAPAN.

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOISHI JAPAN
(TANZANITE SOCIETY) UNAPINDA KUCHUKUA NAFASI HII KUWATANGAZIA
WATANZANIA WOTE WANAOISHI JAPAN HUSUSANI MAENEO YA
KANAGAWA,TOKYO,CHIBA NA MAENEO JIRANI KUWA KUTAKUWA NA
MKUTANO WA WANACHAMA WOTE UTAKAOFANYIKA:

TAREHE: 29/03/2009
SIKU : JUMAPILI
MAHALI : UKUMBI WA ODAKYU SAGAMIHARA
MUDA : KUANZIA SAA KUMI NA MBILI JIONI(12:00)

PAMOJA NA MAMBO MENGINE, AJENDA ZA MKUTANO HUU NI KAMA
IFUATAVYO.
1.KUTOA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA JUMUIYA
2.KUJADILI ULIPAJI WA ADA ZA KILA MWEZI KWA WANACHAMA
3.KUJADILI SUALA LA USAJILI WA JUMUIYA
4.MENGINEYO.

UONGOZI UNAOMBA TUJITOKEZE KWA WINGI SIKU HIYO NA VILEVILE
TUZINGATIE MUDA.

MKUTANO UTAANZA RASMI SAA 12 KAMILI JIONI.

NATANGULIZA SHUKRANI.

KATIBU MKUU MSAIDIZI WA JUMUIYA.
ABBY SENKORO


========================================================
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society)
M/Kiti: 090-3899-0638 Makamu M/kiti: 080-30975744
Katibu Mkuu: 090-4130-4754 Katibu M/Msaidizi : 090-9801-4433
K/Mwenezi : 080-3532-4043
=======================================================
Reactions::

Thursday, March 26, 2009

MSIBA

Familia ya Mallya Kilauwo inasikitika kutangaza kifo cha Cecilia Damas Thadey Mallya
kilichotokea 24/03/2009 kwa ajali ya kugongwa na gari.
Marehemu alizaliwa 13/12/2002,alikuwa anasoma darasa la pili shule ya Msingi Maili Sita.
Mazishi yatafanyika siku ya ijumaa 27/03/2009 nyumbani kwao Maili-sita Moshi.
Unaweza kuwapatia pole wafiwa.

0715-384608 Damas Mallya (baba mzazi)
0754-042821 Honesta Kiria (mama mzazi)
1816-462-2100 Lucy Mallya : Missouri
1515-779-2774 John Mallya : Des Moines


Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana lihimidiwe-AMEN.
Reactions::

" Mama Hapo Umekosea!"


Pichani mtoto Gladness anaonekana kama vile anamwelekeza jambo mama yake aitwaye Flora. Ilikuwa ni kwenye warsha ya maktaba kwa jamii pale Ilula FDC jana.
Reactions::

Viriyala Huyu Hapa!

Reactions::

Nashiriki Kuendesha Warsha Ilula


Inahusu Maktaba za jamii. Inafanyika kwenye Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ilula, Kilolo, Iringa. Ilianza jana na inamalizika leo. Inashirikisha wadau kutoka vyuo vya maendeleo ya wananchi vya Ilula, Njombe na Ulembwe vyote vya Iringa. Kuna wadau pia kutoka vijiji na maeneo yanayovizunguka vyuo hivyo. Warsha hii imefadhiliwa na shirika la Misaada ya Kimaendeleo la Forum Syd la nchini Sweden.
Reactions::

" Iko Hivi..."


Flora, mmoja wa washiriki wa warsha, akielezea kilichojadiliwa na kikundi chake kuhusiana na namna ya kuishirikisha jamii kwenye mipango ya maktaba katika vijiji vinavyokizunguka Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ulembwe, Njombe.
Reactions::

Mjadala Wa Kimakundi


Kwenye warsha ya maktaba za jamii, Ilula FDC, jana.
Reactions::

Huyu Mtoto Akifika La Kwanza Hakamatiki!



Anaitwa Gladness (4) yuko sambamba na mama yake aitwaye Flora kwenye warsha ya Maktaba za jamii inayomalizika leo pale Ilula, Iringa.
Reactions::

Kumbukumbu Ya Marijani Wa Rajab


Hayati Marijani Rajabu

Ni miaka 14 tangu Marijani Rajabu au “Jabali la Muziki” aiage dunia. Marijani alikuwa nyota njema ya muziki kwa miaka mingi. Aliweza kushiriki katika uimbaji na utunzi wa nyimbo nyingi ambazo zilipendwa, zinapendwa na zitaendelea kupendwa au kusikilizwa kwa miaka mingine nenda rudi. Globu ya Jamii kwa kushirikiana na www.bongocelebrity.com wanatoa salamu kwa wapenzi wote wa Jabali la Muziki na kuwakumbusha kwamba leo ndio siku ya kumuenzi. Rai ingine ni kwa waandaaji wa Kili Music Awards kumuenzi Marijani katika tuzo watoazo.


sikiliza vibao vyake viwili kwa kubofya hapa
BongoCelebrity
Reactions::

Mahunda Huna Haja Ya Kututangazia!


Klabu ya Yanga juzi ilichukua ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2009/10. Na Clarence Mahunda, Hale, Tanga.


( Yanga siku zote ni Yanga, utawajua tu. Simba ubingwa hatuutangazi hivyo!) Tukiweka utani pembeni, tunawapongeza Dar Young Africans, ubingwa mwaka huu mlistahili.
Reactions::

Ajali


Kaka hii ni ajali ya basi la Tonda iliyotokea juzi jumatatu pale kinegembasi kilomita 20 kabla hujafika makambako,gari yetu ilikua moja ya magari yaliyofika muda mfupi baada ya tukio,basi lilikua linatoka dar kwenda mbeya,abiria mmoja aliyefahamika kwa jina la said aliyekuwa akitoka dar kwenda mbeya alifariki pale pale angalia kwenye picha kuna mguu ndo wake,mama mwingine na mzee mmoja walifia makambako dispensary.

--
Godfrey Richard Mwanakulya
P.o box 200
Iringa
Tanzania
+255 714 592 665

Ritzinkuja 1 F 35 20380
Turku
Finland
Reactions::

Sweet Eazy!

Reactions::

Wednesday, March 25, 2009

Koma Nini Tena?

Reactions::

" Sisi Ni Ndugu Kabisa!"


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa wanasiasa wa Comoro kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yao ili kulinda na kutunza amani na utulivu kwa manufaa ya wananchi na visiwa vyao.

Rais Kikwete ameyasema katika hotuba yake kwa wananchi wa Comoro katika ukumbi wa Bunge ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara ya kiserikali katika visiwani vya Comoro.

“Wanasiasa wana dhamana ya kulinda wana Comoro, wanasiasa ndiyo chanzo, mkiamua nchi iwe na umoja, amani na utulivu itakua , mkiamua visiwepo nchi itakosa vyote” amesema Rais Kikwete na kuwaasa kuchagua umoja, amani na utulivu.

Amesema siku zote watu wa nje hulaumiwa, lakini nao hushirikiana na watu wa ndani na hivyo wanasiasa wakiacha kushirikiana na watu wa nje dhidi ya maslahi ya nchi amani na utulivu vitadumu.

“Mara nyingine tamaa za madaraka na mali husababisha kuvunjika kwa amani na wananchi ndiyo wahanga wa tama hizi za wanasiasa, heshimuni yale mnayokubaliana kufanya wakati wa mazungumzo, mkikiuka hizo taratibu mlizokubaliana mnaleta matatizo” Rais Kikwete ameongeza na kusema kuwa mkataba wa Fomboni, mkataba ambao umeweka taratibu za mapatano baina ya visiwa vya Comoro ni chanzo na njia nzuri ya maridhiano.

“ Mkataba wa Fomboni umeweka misingi mizuri ya Demokrasia, kwa kubainisha kuwa viongozi watachaguliwa na wananchi, visiwa vyote vitatu vya Ngazidja, Anjouan na Moheli vina heshima moja na sawa na kwamba viongozi watabadilishana baina ya visiwa”. Amesema Rais Kikwete.

Mapema baada ya kuwasili Rais Kikwete amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro mheshimiwa Ahmed Abdallah Mohamed Sambi katika ikulu ya Comoro na kuelezea nia yao ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.

Rais Kikwete ameahidi kufungua ubalozi mdogo visiwani Comoro haraka iwezekano ili kurahisisha mawasiliano baina ya nchi na wananchi wake.

Katika ziara hii, Tanzania na Comoro zinategemea kutiliana saini mikataba mbalimbali ya kibiashara na kijamii.

Baadaye leo (25.Machi, 09) Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajia kutembelea kisiwani Anjouan ambapo atapokea Tuzo kufuatia mchango wa Tanzania katika kuvikomboa visiwa vya Anjouan kutoka katika serikali ya Uasi ya Kanal Mohammed Bacar na baadaye kufungua tawi la Exim Bank.

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Moroni, Comoro

24. Machi, 09
Reactions::

Ziara Ya Ali Kiba Ufaransa Yafana



MABAUNSA ILIBIDI WAFANYE KAZI YA ZIADA KUWAZUIA MASHABIKI KUMVAMIA ALI KIBA JUKWAANI KAMA MNAVYOONA KWENYE PICHA HUKU WAKINA DADA KELELE HUKU WAKIITA ''ALI KIBA MARRY ME!!!''


KATIKA MASHABIKI WALIOKUWEPO MMOJA WAPO ALIKUWA MCHEZAJI MAARUFU WA TIMU YA DARAJA LA KWANZA NCHINI UFARANSA AUXIRRE-NANTE KUTOKA KENYA AITWAYE DENNIS OLIECH ANAYEONEKANA KATIKATI YA MASHABIKI AKIWA AMEVAA KOFIA NYEUPE.


BAADA YA HAPO SIKU YA JUMAPILI ALI KIBA PAMOJA NA TIMU YAKE WALIANDALIWA CHAKULA CHA USIKU NA WENYEJI WAO WA UFARANSA KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA PIA KILIKUWA NA WANAMAMZIKI WA KIKE KUTOKA UGANDA ANAEISHI UHOLANZI ANEYEPIGA MTINDO WA RAGGEA TONE.
MDAU, UFARANSA
Reactions::

Kiba Nyumbani Kwa Promota


Nyumbani kwa promota David Senyagwa
Reactions::

Tuesday, March 24, 2009

SIKILIZA " KWANZA JAMII" MTANDAONI!


Katika kila tufanyalo, tukumbuke, kuwa kuna Watanzania wenzetu kwa mamilioni ambao hawana huduma muhimu kwa mwanadamu. Kuna lazima ya sauti zao kusikika; SIKILIZA: http://www.kwanzajamii.podomatic.com
Reactions::

Kondoa

Reactions::

Umbali

Reactions::

CUF Nzega


Tabora.
Reactions::

Mitaa Ya Kati Mpwapwa


Dodoma.
Reactions::

Monday, March 23, 2009

Moto Wa Kuotea Mbali!


Mwanamziki wa dansi MR.Buti Jiwe aka Garinoma,Jr. anayefanyia shughuli zake nchi Holland! ameibuka na Album ya moto wa kuotea mbali yenye jina na nembo yake
"Buti Jiwe".Mwanamziki huyu Mr.Buti Jiwe,ni kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi" wa
bongo,Mr.Buti Jiwe amejijengea umaarufu nchini Uholanzi na amepania kwa mwendo
wa kasi wa kutimia BUTI JIWE lake kuhakikisha dansi lake linasambaa kila mahali duniani!
Nia yake hiyo nzuri inamfanya kupokelewa kwa mikono miwili ya washabiki pamoja na
bendi mabali mbali za mziki wa dansi katika kila kona.
Mr.Buti Jiwe anatoka katika familia ya wenye damu ya mziki,lakini mafanikio yake yanatokana na kujitima pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyo nayo,ambayo inawezekana kuwa mfano wa kuigwa na kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi".
Mr.Buti Jiwe na CD yake "Samahani" inaonekana kuanza kutawala vituo mbali mbali vya radio barani Ulaya.
Mwendo huo wa kasi wa MR.Buti Jiwe,Garinoma (Jr) unaelekea kupiga teke kwa njia ya mziki katika kila kona duniani,Mwanamziki huyo kijana mwenye majina ya kutisha
Mr.Buti Jiwe aka Gari!Noma! anafananishwa na gari lenye mwendo wa kasi ya hatari kimziki! gari ambalo ukidandia ni hatari ya NOMA.
wale wadau wanaotaka kuisambaza CD ya Mr:Buti Jiwe wasisite kuwasiliana na buti jiwe
at butijiwe@yahoo.com
Reactions::

Mahunda: Urais Hausomewi, Dj Kachukua Nchi!


"...ndugu zangu,uwaziri hausomewi..." Haya ni maneno ya Mh.Kikwete wakati akitangaza baraza la mawaziri mwaka 2005.Hata urais hausomewi.Ingawa kwa hapa kwetu inahitajika shahada yoyote(si mimi ndivyo ilivyo).
Huko Madagaska DJ amechukua nchi,nna imani ataweza kama wenyewe wamemtaka kwa utaratibu wao,UKIZINGATIA HAUSOMEWI..Imeletwa na Clarence Mahunda, Hale, Tanga.
Reactions::

Makanisa Yako Mengi!


Hili ni la upenyo, Dodoma.
Reactions::

Rujewa 1988!


Mbarali, Mbeya. Sasa Rujewa imekuwa ' ka-mji haswa'. Na umeme alituletea marehemu Ukiwaona Ditopile Wa Mzuzuri alipokuwa wizara ya nishati.
Reactions::

Mh. Rais Kwenye Msiba Wa Mwanandugu


JK (aliyevaa kanzu ya Rangi ya udongo) akishiriki katika kuuswalia mwili wa Marehemu Mbaraka Selemani Kikwete wakati wa ibada ya Mazishi iliyofanyika kijijini Msoga,wilaya ya Bagamoyo leo jioni. Marehemu Mbaraka Kikiwete ni mtoto wa Kaka yake JK, Mzee Selemani Kikwete. ( Picha: Michuziblog)
Reactions::

Maisha Ndivyo Yalivyo


Mara nyingi humo ninamopita hukutana na Watanzania wenzetu wanaotembea kwa miguu kilomita kwa kilomita. Huwa kuna mawili; hakuna usafiri, au hawana nauli. Pichani ni njia ya kwenda Mpwapwa, Dodoma.
Reactions::

Nani Anasema Watanzania Ni Wavivu Wa Kufikiri?


Huyo aliye pichani hajalala, anafikiri.Inahusu maisha. Pichani ni Dodoma Mjini. Nilikuwa huko majuma kadhaa yaliyopita.
Reactions::

" Tutaishi!"


Iringa Mjini.
Reactions::

Kijiji Cha Nini Hii!


Chamwino, Dodoma ( Niliipiga picha hii nilipokuwa mikoa ya Kanda ya Kati hivi karibuni)
Reactions::

Kijiko Hiki!


Cha enzi na enzi.
Reactions::

Isimila Stone Age Site


Iringa.
Reactions::

Sunday, March 22, 2009

Winter Kali Lakini Inapendeza!



Ni Helsinki, Finland. Je mwenyekiti nipite njia ya mkato hapo kwa kutumia dakika 5 au nizunguke kwa dakika 15? maana hapo kawaida ni maji winter ndio yanaganda. Ila wazawa hadi wanavua samaki kama unavyowaona!
Reactions::

Mwaka 1988- ' Naonja Maji Kijijini Kwetu Nyeregete!'


Alikozaliwa baba yangu. Ni kilomita 8 kutoka mji wa Rujewa, wilaya ya Mbarali, Mbeya.( Picha nyingine zinanishtua hata miye mwenyewe. Imepita zaidi ya miaka 20 na bado napenda staili hiyo ya mavazi; batiki/kitenge na jeans!)
Reactions::