Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya vipande na mabaki ya mabomu vilivyookotwa katika makazi ya watu wanaoishi karibu na kambi ya Jeshi la wananchi Mbagala jijini Dar es Slaam ambapo nyumba kadhaa ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kupoteza maisha wakati ajali ilipotokea katika ghala la kuhifadhia silaha za kivita katika kambi hiyo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa usalama na utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali Paul Meela,Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Emmanuel Nchimbi,Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema.(Picha na Freddy Maro)
Thursday, April 30, 2009
" Hapa Ilikuwa Lazima Vumbi Litimke!"

" Pole Bi.Mariam!"
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mtoto Mariam Isihaka(8) aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi huko Mbagala jijini Dar es Salaam jana mchana.Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Selemani mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar es Salaam.( Picha na Freddy Maro)
| Reactions:: |
Maelezo
Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Mifupa ya Moi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbil(kulia) wakimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto aliyevaa mavazi maalum) maelezo ya mgonjwa aliyejeruhiwa vibaya na moja ya mabomu yaliyolipuka katika ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhia dhana za kivita katika kambi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania huko Mbagala, jijinji Dar es Salaam.Mgonjwa huyo amepoteza mguu wa kulia na amepoteza damu nyingi na napumua kwa kutumia mashine maalumLife Supporting machine.Rais Kikwete alirejea jijini Dar es Salaam leo akitokea mjini Arusha ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulimalizika jana jioni.(picha na Freddy Maro)
| Reactions:: |
Wednesday, April 29, 2009
Picha Ya Pamoja
East African Community Heads of State in group photo shortly after the end of the 10th Summit of Community held at Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha.From left President Yoweri Kaguta Museveni,President Mwai Kibaki of Kenya, President Paul Kagame of Rwanda who is also the current Chairman of the community,The united Republic of Tanzania President Jakaya Mrisho Kikwete,and President Pierre Nkurunzinza of Burundi(photo by Freddy Maro)
| Reactions:: |
Milipuko Ya Mabomu: Taarifa Zaidi
SUKHDEV CHHATBAR, Associated Press Writer, anataarifu:
ARUSHA, Tanzania – Huge blasts rocked an ammunition dump at an army camp in Tanzania's commercial capital on Wednesday, officials said.
Several people were feared dead, according to police spokesman Mohamed Mhina. The blasts lasted for about two hours and fires were still burning two hours after that, he said.
Local media reports said houses around the military base were on fire and several people had been injured. Local schools have called parents to come pick up their children. The blast rattled windows in houses 37 miles (60 kilometers) away, said resident Kate Esmail.
William Nchimbi, the deputy defense minister, said bombs, bullets and other ammunition exploded in an armory at the Bagala Army Camp in the coastal city of Dar es Salaam.
"We have formed a team to assess the source and the loss incurred," Nchimbi told journalists in the northeastern town of Arusha, where he was attending a regional leaders' meeting. He did not take any questions.
Ammunition dumps are volatile and easily ignited. The Bagala Army Camp is surrounded by civilian homes but is far from downtown Dar es Salaam.

Dar Es Salaam Imetikisika Kwa Milio Ya Mabomu
Leo kuna wengi waliokatisha usingizi wao wa mchana. Kila mtu alikuwa macho jijini Dar Es Salaam. Hata fundi saa huyu wa Mtaa wa Jamhuri nilimkuta akifuatilia kwa makini kinachoendelea Mbagala.
Nilisimama kona ya Jamhuri na Morogoro Road. Nilijiandaa kuvuka barabara kwa miguu kuelekea Kariakoo pale mlio wa kwanza wa bomu uliposikika. Saa yangu iliniambia ni saa 10:30. Milio mingine ikafuatia, si wengi walioshtuka.Kuna hata waliodhani kuwa inatoka kwenye majengo ya maghorofa yanayojengwa jirani. Haraka taarifa zikaanza kupatikana kuwa kuna mabomu yanayolipuka kwenye kambi ya jeshi Mbagala. Dar Es Salaam ikawa imebadilika. Kila kona kukawa na simulizi na watu wanaofuatilia kwa karibu. Majira ya saa nane ikaja taarifa za watu kuambiwa watoke kwenye majengo marefu. Niliona wafanyakazi wengi wakiwa nje ya ofisi zao. Shughuli nyingi zilisimama. Nilifika jengo la Jmall pale Mtaa wa Samora na kukuta maduka yamefungwa na watu wakiharakisha kutoka ndani ya jengo hilo.
Kuna taarifa za majeruhi na watu waliopoteza maisha yao katika tukio hilo. Tunasubiri taarifa zaidi za kuthibitishwa na vyombo husika na vile vile tathmini ya kilichotokea. Tunawapa pole wote walioathirika na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.
| Reactions:: |
' Kikao Cha Mlango Kufungwa'
Closed Door Meeting. The East African Heads of state meet in the closed door session during the 10th summit of the East African Community Heads of state at Ngurdoto mountain lodge in Arusha this morning.From Left President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, President Mwai kibaki of Kenya,The Current chairman of the East african Heads Of state Summit President Paul Kagame of Rwanda, The President of The United Republic of Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete and President Pierre Nkurunzinza of Burundi.(photo by Freddy Maro)
| Reactions:: |
Tete A' Tete
Tuesday, April 28, 2009
ZAIN: Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Moi waitambia Kampala Zain Africa Challenge
* Muhimbili, Zambia kuchuana leo
Dar es Salaam, Jumanne, Aprili 28, 2009
Chuo Kikuu cha Moi kutoka Kenya juzi kiliibuka na ushindi dhidi ya Chuo Kikuu cha Kampala kutoka Uganda katika mechi ya tisa ya mashindano ya chemsha bongo ya Zain Africa Challenge (ZAC).
Chuo Kikuu cha Moi kiliwang’oa mashindanoni wapinzani wao Chuo Kikuu
cha Kampala, kwa kuwachapa kwa pointi 650 dhidi ya 540.
Mashindano ya ZAC yanaendeshwa kwa siku 31 katika mtindo wa mtoano na
yanashirikisha vyuo vikuu 32 kutoka katika nchi nane za Afrika zinazozungumza Kiingereza ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.
Mpaka sasa, vyuo vikuu vilivyofuzu raundi ya pili ni Jomo Kenyatta, Egerton kutoka Kenya, Ibadan, Lagos (Nigeria), Mzumbe (Tanzania), Mbarara, Busoga (Uganda) na Valley View (Ghana); ilhali vyuo vilivyoaga mashindano hayo ni Kwame Nkhuruma (Ghana), Chuo Kikuu cha Malawi (Malawi), Njala (Sierra Leone), SAUT, Hubert Kairuki (Tanzania), Copperbelt (Zambia) na Abubakar Tawafa Balewa (Nigeria).
Licha ya kutupwa nje ya mashindano hayo, kila mwanafunzi ataondoka na
zawadi ya dola za Marekani 500 na vyuo vyao kila kimoja kitaambulia dola
5,000.
Mashindano hayo yataendelea leo (Jumatano ya Aprili 29, 2009) kwa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili kutoka Tanzania kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Zambia kutoka Zambia, mchuano utakaooneshwa katika televisheni ya ITV saa tatu usiku.
Tanzania sasa inawakilishwa na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Chuo Kikuu cha Mzumbe na Teknolojia (IMTU) baada ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kutolewa.
Zain pia inatoa zawadi anuwai kwa watazamaji wa televisheni ambao wanapata fursa ya kujibu maswali kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0789 555588. Vyuo hivyo vinashindania tuzo maridhawa kutoka Zain na donge nono la dola 50,000 kwa chuo kitakachoibuka mshindi. Mashindano hayo yameandaliwa na Zain ili kuinua kiwango cha elimu barani Afrika na pia kuwapatia washiriki fursa ya kujenga mtandao na urafiki utakaotadumu kwa muda mrefu.
Vyuo vikuu vingine vinavyoshiriki mashindano hayo na nchi zinazowakilisha katika mabano ni Chuo Kikuu cha Cape Coast, Chuo Kikuu cha Maendeleo, Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Chuo Kikuu cha Kenya na Chuo Kikuu cha Moi (Kenya).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Mzuzu, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Federal,
Chuo Kikuu Akure, Chuo Kikuu cha Nigeria (Nigeria), Chuo Kikuu cha Kampala, Makerere, Chuo Kikuu cha Uganda Martyrs (Uganda) na Chuo Kikuu cha Northrise (Zambia).

Mwalimu Mwakasege; Alabama

Ndugu, Jamaa na Marafiki,
Tunapenda kuwakaribisha kwenye conference ya neno la Mungu itakayohudumiwa na watumishi wa Mungu CHRISTOPHER & DIANA MWAKASEGE toka Tanzania.
Conference hii ya namna ya kipekee kabisa na yenye ujumbe maalum kwa wakati huu na majira haya tunayoishi kwa kila mtu itafanyika Birmingham, AL USA Mei 22 - 24, 2009.
Mungu amekuwa akiwatumia hawa watumishi ndani na nje ya nchi kwa Upako na wengi wamefunguliwa,kuponywa na kutiwa moyo kupitia huduma hii.
Ahsanteni sana,
| Reactions:: |
Monday, April 27, 2009
KWANZA JAMII KUONEKANA MITAANI KESHO!

Na kwenye mtandao uliokarabatiwa wa http://www.kwanzajamii.com
( Ndio maana Bagamoyo Sendi Tena! Nitabaki Kinondoni Biafra mpaka nimalizie mawili matatu yaliyobaki katika website ya KJ )
| Reactions:: |
Sherehe Za Muungano Ujerumani

Sherehe za muungano Ujerumani
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Ahmada Ngemera, amesema kuwa suala la mtu kuhoji muungano ni kuhoji matakwa ya Watanzania.
Alisema hayo katika sherehe za kuadhimisha miaka 45 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Berlin.
Balozi Ngemera amesema kuwa muungano wa Tanzania ni muungano pekee uliyodumu barani afrika, na kwamba ni mfano kuwa afrika inaweza kuwa moja.
PIC ya kwanza
Aboubakary Liongo wa dw, Sudi Mnette ambaye kwa sasa yuko dw, wakizungumza na balozi Ngemera, mwanzo kulia huku Naibu Balozi Ali Siwa akisikiliza kwa makini
Malumbo S.Malumbo
| Reactions:: |
Kumekucha: Kilimanjaro Vs Bongo FC!
Timu za Watanzania za FC BONGO ya Finland na KILIMANJARO ya Sweden zitachuana rasmi siku ya Jumamosi tarehe 27.6.2009 katika viwanja vya Finnair Stadium Helsinki Finland.
Timu hizo ambazo zilichuana kwa mara ya kwanza mwaka jana huko Stockholm na Kilimanjaro wakabahatika kuwafunga Fc Bongo mabao 4-3 kwa taaabu.
Inasemekana kuwa Fc Bongo walichukiwa sana na uamuzi wa refa kuwapa bao la nne vijana wa kilimanjaro kwa mpira ambao ulikua ushatoka nje, pia baada ya mpira kuisha wakapewa pilau dume bila ya nyama,
Habari kutoka Helsinki zinasema kuwa Vijana wa Fc Bongo wanajinoa vibaya sana Kuwalipizia kisasi watani wao hao kutoka nchi ya jirani.
Kocha na Mlezi wa Fc Bongo Abdalla Ezza ameahidi kuwapa fundisho kubwa la kandanda kwa wageni wake hao wa Kilimanjaro, anaamini kikosi kilichoenda stockholm mwaka jana kilikua hakijatimia kwani wachezaji wake (Key Players) wengi hakuweza kusafiri nao kwani walikua ndio kwanza wamerudi makazini kutoka kwenye likizo zao za summer na hawakuweza kupata ruhusa makazini.
Nao Kilimanjaro wakizidi kujiamini kuwa wataweza kuwanyamazisha wenyeji wao huko Helsinki.
Habari zaidi kuhusu mechi hiyo tembelea website ya kilimanjaro hapa http://fckilimanjaro.snabber.se/
Pichani hapo Kilimanjaro na Fc Bongo kwa pamoja baada ya mpira kuisha mwaka jana huko Stockholm
| Reactions:: |
Viongozi Na Wanachama
Inasikitisha
Gezaulole Baba,Gezaulole Mama !

" Twendeni Kibugumo na Mwanadilatu kwenye makao mapya!". Bila shaka kuna mnaoukumbuka wimbo huo wa enzi zile za operesheni ya kusaka wazururaji Dar Es Salaam. Vijana ' wazururaji' mjini walikuwa wakipakiwa kwenye malori na kupelekwa vijiji vya Gezaulole, Kibugumo,Mwanadilatu. Leo wenye kuishi huko wanaondolewa kwa ' vijisenti' na wakati mwingine kuondolewa kwa hila kupisha 'wawekezaji' wenye kuvutiwa na maeneo hayo ya kando ya bahari. Naam. Watoto na wajukuu wa 'Wazururaji' wale wa miaka ya 70 wanaandaliwa mazingira ya kurudi tena mjini 'kuzurura'!
| Reactions:: |
Sunday, April 26, 2009
Chemsha Bongo Ya Zain
Mtazamaji wa televisheni, Rachel Maseke akionyesha simu aliyokabidhiwa na Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju (kushoto), Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi kwa kujibu kwa ufasaha maswali katika mashindano ya chemsha bongo ya Zain Africa Challenge (ZAC) yanayoendelea. Kulia ni Meneja Masoko wa Zain, Ellen Lupili.
| Reactions:: |
Miss Tanzania EU
MISS TANZANIA EU 2009 REGISTRATION continues!!!!
Application Form for Miss Tanzania European Union
www.misstanzania.eu
Mashindano haya ya urembo yatashirikisha warembo wakitanzania toka nchi za jumuiya ya Ulaya (Schengen) yatafanyika Essen Germany.
Washindi 3 wa mwanzo watawikilisha warembo wengine huko United kingdom katika mashindano ya Miss Tanzania Europe mwishoni mwa mwezi Juni.
Jiandikishe sasa!!
info@misstanzania.eu
+49 174 45656 44

Ali Kiba Atumbuiza Napoli
Saturday, April 25, 2009
MSIBA: Martha Sinkara

Familia ya Nyingo “Lingalangala” wa Houston, Texas inapenda kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki popote pale duniani kuwa Mama yetu Mpendwa Martha Sinkara amefariki dunia nyumbani kwake Ludewa Iringa tarehe 22/4/2009. Taratibu zote za mazishi zimefanyika huko huko Ludewa tarehe 24/4/2009. Kwa wote wenye mapenzi mema tunaomba sala zenu ili Mwenyezi Mungu amjalie neema katika safari yake hii ya mwisho.Bwana ametoa na Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe milele. Amina
| Reactions:: |
Friday, April 24, 2009
Kibera
Thursday, April 23, 2009
Wednesday, April 22, 2009
SOMA KWANZA JAMII KWENYE MTANDAO!

KWANZA JAMII liko mitaani kuanzia jana Jumanne, Aprili 21, 2009. Unaweza kulisoma kwenye; http://www.kwanzajamii.com
| Reactions:: |
NINA TATIZO LA NETWORK
Wapendwa,
Kumekuwa na kimya kingi kutoka kwangu. Ni kutokana na tatizo la network eneo nilipo hapa Iringa, inakatikakatika. Naahidi kuungana nanyi mara tu network ikirudia hali ya kawaida.
Poleni kwa usumbufu.
Maggid

Monday, April 20, 2009
Kivuko Kipya!
Samaki Bwelele, Hawana Soko!
Zain Africa Challenge
Egerton kuchuana na Wanigeria Zain Africa Challenge
* Hubert Kairuki kupimana na Waganda Jumatano
Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19, 2009
Chuo Kikuu cha Egerton kutoka Kenya kinatarajia kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Abubakar Tawafa Balewa kutoka Nigeria (leo, Jumatatu ya Aprili 20, 2009), katika mechi ya saba ya mashindano ya chemsha bongo ya Zain Africa Challenge (ZAC) yanayoendelea jijini Kampala, Uganda.
Pia wawakilishi wengine wa Tanzania, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki wanatarajiwa kupimana ubongo na Chuo Kikuu cha Busoga kutoka Uganda (Jumatano ya Aprili 22, 2009), mchuano utakaooneshwa katika televisheni ya ITV saa tatu usiku.
Tanzania sasa inawakilishwa na vyuo vikuu vinne ambavyo ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki, Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Teknolojia (IMTU) baada ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kutolewa wiki iliyopita Chuo Kikuu cha Lagos cha Nigeria katika mechi ya tano.
Mpaka sasa, vyuo vikuu vilivyofuzu raundi ya pili ni Jomo Kenyatta kutoka Kenya, Mzumbe, Mbarara kutoka Uganda, Ibadan Lagos na Valley View (Nigeria); ilhali vyuo vilivyoaga mashindano hayo ni Kwame Nkhuruma (Ghana), Chuo Kikuu cha Malawi (Malawi), Njala (Sierra Leone), SAUT na Copperbelt.
Licha ya kutupwa nje ya mashindano hayo, kila mwanafunzi ataondoka na
zawadi ya dola za Marekani 500 na vyuo vya kila kimoja kitaambulia dola
5,000.
Zain pia itatoa zawadi anuwai kwa watazamaji wa televisheni ambapo
watapata fursa ya kujibu maswali kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba
0789 555588. Vyuo hivyo vinashindania tuzo maridhawa kutoka Zain na
donge nono la dola 50,000 kwa chuo kitakachoibuka mshindi. Mashindano
hayo yameandaliwa na Zain ili kuinua kiwango cha elimu barani Afrika na
pia kuwapatia washiriki fursa ya kujenga mtandao na urafiki
utakaotadumu kwa muda mrefu.
Vyuo vikuu vingine vinavyoshiriki mashindano hayo na nchi zinazowakilisha katika mabano ni Chuo Kikuu cha Cape Coast, Chuo Kikuu cha Maendeleo, Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Chuo Kikuu cha Kenya na Chuo Kikuu cha Moi (Kenya).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Mzuzu, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Federal, Chuo Kikuu Akure, Chuo Kikuu cha Nigeria (Nigeria), Chuo Kikuu cha Kampala, Makerere, Chuo Kikuu cha Uganda Martyrs (Uganda) Chuo Kikuu cha Northrise na Chuo Kikuu cha Zambia (Zambia).
Mashindano ya ZAC yanaendeshwa kwa siku 31 katika mtindo wa mtoano na
yanashirikisha vyuo vikuu 32 kutoka katika nchi nane za Afrika zinazozungumza Kiingereza ambazo ni Sierra Leone, Ghana, Nigeria, Uganda, Kenya, Tanzania, Zambia na Malawi.
| Reactions:: |
Sunday, April 19, 2009
Nimerudi Iringa Usiku Huu
Nikitokea Dar kupitia Bagamoyo, Miembe Saba, Mlandizi na kuendelea.
Poleni kwa mimi kushindwa kuwaingizia picha kwa zaidi ya saa 24. Ni kutokana na sababu za kiufundi. Natumaini kesho hali itarejea ya kawaida.
Kwa sasa nimefurahi kurudi Iringa yetu ya baridi ya wastani. Si ya joto kama la Dar na Bagamoyo.
Na kazi zinaendelea bila joto wala mbu!

Saturday, April 18, 2009
BAP Aeleza Kisa Cha Kujiita Born Again Pagan!

( Ni baada ya kuulizwa na msomaji kwenye Kwanzajamii.com)
Batamwa na wasomaji wengine watukufu:
Ufuatao ni mkitadha wa jina la kalamu la “Born Again Pagan” kwa mwenye kutaka kujua:
Siku moja ya Jumatatu nilisafiri kwa ndege kuelekea sehemu za Midwest, huko Wichita, Kansas, hapa Amerika.
Nilijua safari itakuwa ndefu kwani walisema tungepitia Chicago. Kwahiyo, niliamua kununua gazeti la New York Times – gazeti kubwa kwa wingi wa kurasa na maeneo yake.
Niliingia na kukaa na abiria mwenzangu ambaye alikuwa na Biblia kwenye kimeza chake akienda Chicago. Tuliamkian na kujuliana mambo ya safari.
Baada ya kupaa na kuendelea na safari usalama usalimini, mimi huku nikiendelea kusoma gazeti langu, mwenzangu alifungua Biblia yake.
Kabla ya kutua Chicago, alianza kuniuliza kwa Kiingereza kuwa hilo gazeti la ma-“liberali’ lilikuwa na hadithi gani za maana siku hiyo.
Huku niking’amua kuwa huenda mwenzangu alikuwa ni m-“koservative” (mfaidhina, nilijaandaa kumkabili.
Nilimweleza machache na kuzingatia hadithi moja ya vita huko Afghanistan.
Yeye akaanza kunihubiria kuwa ni wajibu wa watu wa Mungu kuingilia kati katika vita hiyo.
Mimi nikamwuliza endapo binadamu kweli ana haki ya kumpigania Mungu vita.
Akajibu ndio, na kunitolea mifano mingi kutoka Agano la Kale!
Nilimsikiliza kwa makini. Nikasema hiyo ni kweli. Lakini Yesu alikuja kama “Prince of Peace”! Ndio maana hakuna hayo ya vita katika Agano Jipya.
Niliendelea: Yesu anatufundisha kugeuza shavu lingine, na kusamehe saba mara sabini. Mtoa adhabu ni Mungu peke yake, na kadhalika.
Na kwamba Yesu alimwambia Petro aachane na kumpigania. Na kumwonyesha majeshi ya Mungu!
Mara akaniuliza endapo nilikuwa m-Kristu. Nikamjibu ndio. Kumbe nikachokoza nyuki!
Mswali yakazidi…kuhusu ya Biblia na kumhakikishia kuwa naisoma.
Alitaka kujua kama mimi ni mlokole (born again) Nikamjibu ndio.
Punde akapaza sauti, “Aleluya! Mungu asifiwe kwa kutuweka viti vya karibu.”
Hapo ndipo nikamjibu kuwa kakosea. Yeye akaguna kuonyesha kwa nini.
Nikamjibu, “I am a Born Again Pagan”.
Akakaa kimya na kunikodolea macho! Hakuzungumza nami tena!
Mara tukaambiwa kuwa tulikuwa tunatua O’Hare Airport.
| Reactions:: |
Friday, April 17, 2009
BAP: Uchaguzi Wa Marekani Na Fundisho Kwetu

SEHEMU YA TATU
Na Born Again Pagan,
ILI kutimiza lengo la upande wangu, ninajaribu kuchangia juu ya taratibu na mienendo ya demokrasia ki-matendo (functioning democracy). Uchambuzi huu utafuata baadhi ya vigezo vya michakato ya voting mechanics, kama ninavyoitafsiri hapa chini. Mazuri yake tutayafanyia external applications, endapo tutapenda kufanya hivyo, ili tuyaige (kulingana na hali halisi ya nchi yetu ya Tanzania tuipendayo). Hii itatusaidia katika kuweza kujenga, kutandaza na kudumisha desturi na kanuni za ki-utawala (ki-uongozi) kwa minajili ya kufanikisha utamaduni wa demokrasia katika nchi yetu tuipendayo. Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
| Reactions:: |
Thursday, April 16, 2009
Bajaj Za Ethiopia

Picha hizo nimezichukua karibuni mji uitwao
Adama au Nazareth kule Ethiopia. Bajaj hizo kule ni maarufu kwa jina
"BIMBI" ambapo tafsiri yake ni MBU. Jina hili nimelipenda maana ukitafakari
kwa kina utaona vipikipiki hivi kweli vinafanana na mbu kimaumbile hata mlio
wa injini yake vinapotembea. Moja la muhimu nililoliona jipya ni bimb hizo
kuwa na milango kwenye cabin ya abiria ambayo unaweza kuwekwa na kutolewa.
Ubunifu huu naona haujafika hapa kwetu. Unaonaje na huku kwetu tukaana
kuvitaiza jina la kihehe la "SOOGO"
Mwenyekiti nawasilisha wanachi nao wafaidike.
Mwanakijiji Pasumilemnyiga Changalakiki (Louis Kasuga)
| Reactions:: |
Laltaika: Je, Mjerumani Aliacha Mali Tanganyika?
Makala ya utangulizi wa kona hii ilikuomba msomaji kutuma maoni yako kuhusu kuwepo kwa mali za thamani za Wajerumani katika misitu ya iliyokuwa Tanganyika. Inafurahisha kuona idadi ya watu walioguswa na mada hii.
Ni wazi, kuwa minon’gono, au niite uvumi, huu haukuanza juzi. Inawezekana ulianza mara baada ya Wajerumani kufunga virago vyao na kuwapisha ‘binamu’ zao Waingereza kuitawala Tanganyika kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Ninaendelea kupokea maoni yako. Leo tutachambua maoni ya baadhi ya Wajerumani. Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
| Reactions:: |
Subscribe to:
Posts (Atom)