Subscribe:

Sunday, May 31, 2009

" Kwanza Nikushukuru....."



Ni siku ambayo Mbunge Mh. Anne Kilango alipokabidhiwa zawadi ya vifaa vya michezo kutoka kwa mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Mohammed Raza pale Ukumbi wa Maelezo juma la jana.
Reactions::

Fr. Mushi: " Mapadri Tumezoea Utani!"

Naomba na mimi nichangie walau mada hii. Kwa wanakao DC mimi ni Padri Mushi. Nadhani waliochangia hoja na kuona ina udini, kwa upande wangu sioni udini wowote. Nadhani ni kama utani mingine ambayo sisi Mapadri tumezoea kuisikia ikielekezwa kwetu. Mimi napenda watu waliogushwa na utani huu wachukulie ni utani wa kawaida, ni kama wanajua Philosophy basi waangalie joke hii in Philosophical approach kuliko kuendelea kuzozona kwenye hili, nadhani ni utani wa kawaida tu. Nadhani baadhi wamekasirika sababu hakuna utani unazungumziwa juu ya Uislam au wachungaji wa madhehebu mbalimbali...kwa wale waliogushwa ningependa mjue kitu kimoja important "we are catholics" hicho ni muhimu zaidi.....mtasikia matani mengi sana juu ya mapadri...

Fr. Mushi
Reactions::

Da' Subi: TeknoHama Na Tanzania

A relative of mine sent me an email asking a multitude of questions, I tried to answer like 4 of them and then I gave up.
I needed some stats to back up almost everything he asked.
My apology for any repetition on some of the questions, I tried the best I could to trim them down.
Now, this is what he is looking for:
What language do people in Tanzania mostly use?
Do people use the internet cafe much more nowadays or is everyone not really on the internet?
What do you think that everyone trying to do on the internet?
Are they doing social networking Myspace? Facebook? Youtube? or creating websites?
Are people usually looking for jobs on the internet?
What do people do on a typical day? like college students, city folks, people with internet at home? I mean, what is their daily activity for the most?
Do people listen to the news, or look for jobs? look for music online, videos?
What sites are popular out there?
What kind of online activity is important out there?
Other than on the internet, what do people do in their regular life that uses technology?
How much technology is there in Tanzania? cell-phones, laptops, pcs...
Please let me know...its for my project at school for my MASS MEDIA communication class. We are at the end of class, doing this global awareness and if I could present people with something from our Country, that would be GREAT! I want to show people in my class that our country is not just "huts" and people hunting for animals and elephants walking around. I want to tell them what exactly we do and that we are using technology and its becoming popular and that more and more people are doing it online..
Thank you very much for your time!
M.

.end.
nukta77@gmail.com
Reactions::

Wakulima Na Bidhaa Zao


Ni katika moja ya vijiji vya kando ya barabara ya Morogoro-Dodoma. ( Ahsante ya picha: Dr. Louis Kasuga, Mtwara)
Reactions::

Saturday, May 30, 2009

Mambo Ya Twanga Hayo!


Movenpick Dar Es Salaam. Ni katika kuzindua albamu yao ya ' Mwana-Darisalama'. Imeletwa na mdau wa http://www.kwanzajamii.com
Reactions::

Mtego Wa Panya Hunasa Wasio Panya!



Pichani ni Mnazi Mmoja. Nilipofika mahali hapo niliweza kuelewa pia kuwa panya ni tatizo katika nyumba zetu nyingi.
Reactions::

Tafakuri Jadidi Ya Juma Hili



Itafakari picha hii iliyopigwa kwenye moja ya vijiji mkoani Lindi. Kama una hoja changia katika muktadha wa kimaendeleo. ( Asante ya picha Dr. Louis Kasuga)
Reactions::

KUMBUKUMBU YA MAMA CHAHALI

ILIKUWA SIKU,WIKI,MIEZI NA SASA UMETIMIA MWAKA TANGU BWANA ALIPOKUCHUKUA MPENDWA WETU MAMA ADELINA MAPANGO (Mama CHAHALI).PENGO ULILOTUACHIA HALITOZIBIKA MILELE.KINACHOTULIWAZA NI MAPENZI YA BWANA.JAPO SIE TULIKUPENDA,LAKINI YEYE ALIKUPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AKAKUCHUKUA SAA4.30 USIKU WA TAREHE 29/05/2008.JAPO HAUKO NASI KIMWILI,LAKINI TUKO SOTE KIROHO.

KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE PHILEMON CHAHALI,NACHUKUA FURSA HII KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA SALA/DUA WAKATI TUNAMUUGUZA MAREHEMU ADELINA,NA SAPOTI MLIYOTUPATIA KUTUFARIJI BAADA YA MSIBA.BWANA AWABARIKI SANA.

BWANA ALITOA,BWANA ALITWAA.JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE,AMEN.

PUMZIKO LA MILELE UMPE EE BWANA,NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE.APUMZIKE KWA AMANI.AMEEN
Reactions::

Friday, May 29, 2009

Home Sweet Home! Nimeingia Iringa Usiku Huu

Nikitokea Dar.

Bagamoyo sikwenda!
Reactions::

Thursday, May 28, 2009

Spark Africa!

Reactions::

Sweet Easy!

Reactions::

Man United Tanzania



Kaka Hizo ni baadhi ya picha za matukio katika sherehe ya ufunguzi wa jumuiya ya mashabiki wa Manu U hapa TZ. Iliyofanyika tare 27 May '09,Regency Park Hotel na kuhudhuriwa na Balozi wa Uingereza akiwa kama mgeni rasmi kwaajili ya shughuli hiyo.

Asante.
Maingu.
Reactions::

Ni Barca!


Ni Mpira!
Reactions::

Wednesday, May 27, 2009

Je, Padri Aliongopa?

A distinguished young woman on a flight from USA to Dar es salaam,
Tanzania asked the Priest beside her:

Woman: "Father, may I ask for a favor?"

Priest: "Of course. What may I do for you child?"
Woman: "Well, I bought an expensive woman's electronic hair dryer for my
mother's birthday that is unopened and I am well over the Customs
limits, and I'm afraid they'll confiscate it. Is there any way you could
carry it through Customs for me.......... Under your robe perhaps?"

Priest: "I would love to help you, dear, but I must warn you: I will not
lie."

Woman: "With your honest face, Father, no one will question you."



When they got to Customs, she let the priest go ahead of her.

Custom Officer: "Father, do you have anything to declare?"

Priest: "From the top of my head down to my waist, I have nothing to
declare. "

The official thought this answer was strange.

Custom Officer:: "And what do you have to declare from your waist to the
floor?"

Priest: "I have a marvelous instrument designed to be used on a woman,
but which is, to date, unused."

Custom Officer:: (Roaring with laughter, said) "Go ahead, Father." Next!

Now............................................. truly, did the priest
lie?
Reactions::

Kinondoni Biafra, Tena !



Mkurugenzi wa ASET Da' Asha Baraka anasoma kila kitu. Mheshimiwa ni Mjumbe wa NEC,CCM,hivyo basi na gazeti la Uhuru lazima alikamate. Pichani ni maeneo ya karibu na kwetu,Kinondoni Biafra,jana asubuhi.
Reactions::

Mama Salma: "Kataeni Mapenzi, Zingatieni Shule"



Na Mwandishi Wetu
Mtwara.
Hayo yamesemwa na mke wea Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Salma Kikwete alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani humu. Alizungumza na wanafunzi wa sekondari ya wasichana ya Mangamba katika manispaa ya Mtwara.

Mama Salma aliwaambia wanafunzi hao kuwa anazo taarifa zinazosema kuna mimba zipatazo 284 katika kipindi cha kuanzia Januari 2008 mpaka Machi 2009 mimba hizo zimepatikana katika shule mbalimbali mkoani humu.

Akitoa takwimu alizo nazo ni katika wilaya ya Mtwara Mjini mimba 11 shule za msingi sekondari 20 wilaya ya Mtwara vijijini msingi 55 sekondari 23 Tandahimba msingi 35 sekondari 48 Newala msingi 21 sekondari 9 Masasi msingi 14 sekondari 2 Nanyumbu msingi 27 sekondari 19. Jumla ya mimba zote za wanafunzi katika kipindi hicho ni 284

Amesema kwa wanafunzi hakuna sababu ya kukimbilia mapenzi iwapo huna elimu. Ni bora kwanza upate elimu hayo mambo mengine yafuate abadae. Amewataka wanafunzi kukataa kufanya mapenzi bali wazingatie elimu ndiyo ufunguo wa maisha yao ya badae. Katika shule hiyo mama Kikwete alitoa cheki ya shilingi 1,860,000/= kwa wanafunzi wanao lipiwa na kutunzwa na shirika lake la WAMA. Pia ametoa shilingi 1,000,000/= kwa shule hiyo kuwasaidia wanafunzi mbalimbali katika mahitaji yao.

Kabla ya hapo Mama Kikwete alizungumza na jumuia ya wanawake mkoani hapa UWT na kuwaambia wasiwaogope watoto wao wa kike kuzungumza nao kuhusu athari za kuputa mimba za utotoni wakiwa wanafunzi. Amewaasa akina mama hao kujitokeza katika kugombea nafsi za uongozi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vitongoji kule vijijini ili kupatikane idadi kubwa ya viongozi wa kuongoza nyazifa mbalimbali.

Katika nyakati za mchana mama Salma alizungumza na baraza la wazee katika ukumbi wa RC HALL na kuwaeleza kuwa wao kama wazee wana wajibu mkubwa wa kutatua matatizo yote yanapo tokea na kuyamaliza. Alishangazwa na hoja iliyo tolewa na mzee Mpeme kuwa kuna mpasuko ndani ya chama cha CCM na kufanya kuwepo na makundi mawili ndani ya chama kimoja hoja ambayo ilipingwa na mzee Rashidi Chilandwa na kumwomba mama Kikwete awaachie wazee mambo hayo watayamaliza wenyewe.
Reactions::

Tuesday, May 26, 2009

CCM Washinda Busanda


Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Busanda Finias Magesa (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo mara baada ya kupata matokeo kwamba chama chao kimeshindwa kwenye uchaguzi huo.


MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lolesia Bukwimba ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Busanda baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine vilivyokuwa vikishiri uchaguzi huo mdogo wilayani Geita kwa kura 29,242 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho hata hivyo kimekataa matokeo, kilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 22,799.


Chama cha Wananchi (CUF) kilichopata kura 977 na cha United Democratic (UDP) chenye kura 271, viliingia mtini baada ya wagombea na mawakala wake kutoshiriki mchakato wote wa kuhesabu na kuhakiki kura katika hatua ya mwisho.


Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, Dani Mollel alisema idadi ya waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 135,163, jumla ya waliopiga kura ni 55,660, kura halali zilikuwa 53,309 na zilizoharibika ni 2,069. ( Chanzo na habari na picha: Michuziblog)
Reactions::

Meza Ya Magazeti


Chuo Kikuu, Dar Es Salaam.
Reactions::

Monday, May 25, 2009

Kaka Freddy Na Mie



Leo jioni nilipata bahati ya kuhudhuria workshop ya kaka Freddy kuhusu masuala mbali mbali ya kimaisha. Kulikuwapo na vijana wapato 13.Alikuwapo pia Mussa Twaha Kitonge, huyu ni class-mate wangu pale Tambaza enzi hizo. Nilifurahi sana kukutana na kaka Freddy na ndugu yangu Mussa Twaha Kitonge, na zaidi kuona vijana waliohamasika kutaka kujifunza. Tulifanya mambo mengi pamoja tukiwa na mkufunzi Freddy Macha, nitayasimulia siku nyingine. Tuliondoka pale Nyumba ya Sanaa kunako saa tatu usiku.
Reactions::

' Darasa La Usiku, Kwa Wanaume Tu!'


Wanawake zamu yao ilikuwa jana. Pichani ni baadhi ya Vijana Washiriki wakimsikiliza Freddy Macha.
Reactions::

'Imam' Freddy


Nyumba Ya Sanaa leo usiku.
Reactions::

Baadhi Ya Wadau


Walioudhuria workshop ya kaka Freddy Macha pale Nyumba ya Sanaa.
Reactions::

KWANZA JAMII KESHO JUMANNE


Lina mengi ya kuelimisha na kuburudisha.Usikose nakala yako!
Reactions::

" Bwa Mdogo Achana Na Mimi!"



Ukisikia shughuli pevu ndio kama hiyo pichani. Leo nilipita mitaa ya kati Temeke nikakutana na mechi hiyo ya mchangani. Katika mechi hiyo hiyo refa alisimama mbali na kubaki akitabasamu tu pale madaruga yalipokuwa yakirushwa.
Reactions::

Maishani; Kuna Wachache Wanaowekewa Ngazi...


Za Kupandia juu. Kuna wengi tunaolazimika kutafuta mbinu zetu wenyewe za halali za kupandia juu. Hata kama tutaishia njiani, tusichoke kujaribu tena na tena. Pichani ni Kinondoni Biafra leo jioni.
Reactions::

Ofisi Za Kwanza Jamii Kinondoni Biafra

Reactions::

....Movement Of Jah People!



Na Mwandishi wetu
Dar Es Salaam.

Washiriki wa chama kinachoitwa Tanzania Rastafari Movement (TARAMO), saa tano asubuhi leo hii walikusanyika pale Posta ya zamani na kuanza kuadhimisha siku ya Ukombozi wa Afrika. Mratibu wa maadhimisho hayo, Ras Mponeja , ndiye aliyekuwa akitoa taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliojisogeza kuangalia kinachoendela maeneo hayo.

Kwa mujibu wa mratibu huyo maadhimisho hayo yamefanyika ili kuwaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga kupigana dhidi ya uvamizi wa wakoloni.

“Leo taasisi yetu imekusanyika hapa ili kuwaenzi babu zetu ambao walijitoa muhanga kupambana na wavamizi au wanyonyaji waliovuamia bara la Afrika na kuanza kutunyonya na kusababisha hali hii tulionayo leo. Hivyo, tumekusanyika hapa na shughuli yenyewe ndio hivyo unaona imeanza na bado kuna jamaa zetu kibao wapo njiani wanakuja, si unajua tena usafiri ulivyo tabu kwenye jiji hili.” Alisema mratibu huyo huku akifunga funga rasta zake .
Reactions::

Hapa Kila Mtu Ana Uhuru Wa Kutoa Maoni Yake....


Pichani ni Soko Matola, Mbeya 1989.

Mheshimiwa M/kiti najua ni kawaida ya watu wengi wanapopewa maoni ambayo ni hasi kwao hawana kaiwaida ya kukubali au kama watakubali basi huwa hawezi kuyasema kwa wengine kuwa nilishauriwa hivi(kwenu ninyi wenye blog ni kutoyatoa wengine wasome).

Ukweli ni kwamba umekuwa na tabia ya kurudia rudia kuweka posts ambazo umeweka siku za nyuma hii si mbaya kama kuna tukio linamuhusu muhusika fulani na hukufanikiwa kupata picha yake. Lakini wewe kila siku hapa ni Kinondoni Biafra mwaka 1989 au Soko Matola au sijui Rujewa kila siku na kila wakati. Mimi huwa nashindwa kukuelewa hivi hii archive ina maana gani maana kama mtu anapenda kuangalia matukio ya nyuma ataenda kwenye archive sasa wewe kila siku Kinondoni 1989 inachosha mkuu, mbona kuna picha nyingi na matukio mengi unaweza kuweka si lazima urudie rudie inachosha sana.

Haya ni mawazo yangu
Reactions::

RC Tarimo: Ushirika Ni Njia Pekee Ya Kupinga...



USHIRIKA NI NJIA PEKEE YA KUPINGA UNYONYAJI.

Na Mwandishi Wetu,
Masasi, Mtwara

Mkuu wa mkoa wamtwara Kanali mstaafu Anatori Tarimo amaeyasyma hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa chama cha ushirika cha mkoa wa Mtwara (MAMCU)katika ukumbi wa masasi sekondari mwishoni mwa wiki.

Tarimo amesema njia ya kumkomboa mkulima ni kuwa mwana ushirika na ndiyo njia pekee ya kuupiga vita unyoyaji ulio kisiri katika kuwanyonya wakulima wa zao la ko;rosho hapa mkoani pia kwa kufuata mfumo wa stakabadhi ghalani mfumo ambao ume waletea tija wakulima wengi katika miaka hii miwili iliyopita. Amesema wakulima wame weza kununua usafiri,kujenga nyumba bora na za kisasa zaidi,kuimarisha mashamba yao,simu za mikononi kwa mawasiliano na ndugu zao hata vyama vyamsingi vingine kununua matrekta ya kulimia.

Amesema kufuatana na mfumo huo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa 2008 jumla ya shilingi bilioni 27.1 zimekwenda kwa wakulima ambapo awali zingekwenda kwa walanguzi wale waliokuwa wakijimwagia bia wakati ule kabla ya mfomo huu wa stkabadhi ghalani kubunuwa.jambo ambalo ilikuwa ni dhuruma kubwa sana kwa wakulima wenu.

Alieleza kuwa wakati wa kubuni mfumo huu walikumbana na changamoto kadhaa ambazo alizitaja kama kulikuwa na watumishi wachache waliokuwa wakishrikiana na wafanyakazi wa ushirika pamoja na walanguzi kujaribu kuharibu mfumo huu usikubalike na wamkulima mkoani, lakini baada ya mfanikio hayo machache wakulima waliweza kunufaika na kile walicho kiuza katika vyama vyamsigi na mafanikio yake ndiyo haya mnayo yajadili leo hapa nakuoanda mbinu nyingine za kuboresha mfumo huu uimarike

Aliesema nivizuri kwa kila chama cha msingi kufunga hesabu za fedhe katika mapato na matumizi kwa masimu unapo malizika na kubaini manbo fulanifulani yaliojitokeza katika manunuzi ya mazao ya wakulima kwa msimu na kuwasomea wakulima kabla ya mkutano mkuu.kuitishwa. Aidha Tarimo amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuwa macho na walanguzi wana jipitisha huko na huko kanza kulangua korosho ametoa agizo iwapo watabainika watu hao wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Naye meneja mkuu wa MAMACU LTD. Bw, Omega Mnali amesema kufuatana na kufanikiwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kumewapa heshima kubwa kwa wakulima mkoani humo na amesema kuwa sasa wanajipanga katika ununuzi wakila zao mkoani humo linunuliwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Hatahivyo meneja huyo ametoa chaongamoto zilizopo kwa msimu ujao ni kuwahi kupeleka fedha katika vyama vya msingi haraka na kuanza kununua korosho. pamoja na hayo meneja huyo amwaeleza wajumbe kuwa chamachake kimesha jiweka vyema katika kukabiliana na usumbufu wa maghala ya kuhifadhi korosho msimu ujao kwa kujenga maghala yake huko Nanyumbu,Masasi,na Mtwara.

Mhasibu wa chama hicho Bw,Crement Kimolo amesema kwa msimu wa mwaka jana MAMCU walikopa shiligi 114 milioni kununulia mazoao kutoka benki ya CRDB tawi la mtwara na baada ya kuuza mazao hayo katika soko la dunia wamesha rejesha mkopo huo CRDB. Na hawana deni popote.
Reactions::

Sunday, May 24, 2009

Wadau Wa Hali Ya Hewa



Ndugu mjengwa,
Hao ni wadau waliofuzu course ya miezi 6 inayohusu Kupambana & Kuendana na mabadiliko ya hali nchi (CLIMATE CHANGE - MITIGATION AND ADAPTATION) November 2008 inayoandliwa kwa pamoja na Sida na SMHI wakishirikiana na SWECO yote ni mashirika ya Sweden. Hapo ni Juu ya sand dunes za GOBABEB ndani ya Namib desert 140Km kutoka Walvis bay Namibia. Hiyo ni baada ya kumaliza regional seminar iliyofanyikia Walvis bay na GOBABEB Reserach and Training Centre Namibia 9-11 May, 2009

Ni course nzuri kwa ndugu zangu watanzania na mnaweza kuaply kupitia website www.smhi.se ambayo huwa inafanyika kwa mwezi mmoja Norrkoping na stockholm Sweden then unafanya project kwa miezi 5 kabla ya kwenda kupresent sehemu itakayopangwa kutokana na washiriki waliokuwepo. kila mwaka inafanyika mara 2. Mabadiliko ya hali nchi yamrkua changamoto hasa kwa nchi nyingi zinazoendelea ukizingatia wanaosababisha ni mataifa yaliyoendelea kutokana na kuzalisha GHG kwa wingi.

Ni hayo tu Mzee mjengwa
Reactions::

Kinondoni Biafra 1989

Reactions::

Saturday, May 23, 2009

Biashara Ziko Nyingi


Hii ni ya kuuza shuka.
Reactions::

Nchi Ya Amani!


Jamaa amechoka, katandika boksi lake na kuuchapa usingizi wa mchana. Ni mtaa wa Jamhuri, Dar leo alasiri.
Reactions::

Chagga Street


Dar, leo mchana.
Reactions::

Inauzwa


Habari ndugu,
Naomba uturushie mchuma huo ktk globu ya jamii.Unauzwa na mdau anaitwa Kassim Bundallah,anapatikana Tanesco,HALE -TANGA.Bei ni maelewano.Kwa mhitaji awasiliane naye kwa simu namba 0713 858 113.
Reactions::

Friday, May 22, 2009

Dos Santos; " Tupande"- Si Kama DECI!



Kwenye moja ya mashairi ya Marcelino Dos Santos ( Pichani) anasema; " We Must Plant". Hazungumzii kupanda kama ilivyokuwa kwa ' matapeli' wa DECI, bali kupanda fikra za kimapinduzi miongoni mwa wanajamii. Miaka miwili iliyopita nilipata bahati ya kukutana na kuongea na Marcelino Dos Santos jijini Nairobi, Kenya. Marcelino Dos Santos ni 'Kingunge' wa Msumbiji aliyeamua kubaki na Ujamaa. Na hakika jamaa ni ' kichwa' kweli kweli!
Reactions::

Sanda Nyeusi Yaja ( Si Bu-Sanda Nyeusi!)




Sanda nyeusi yaja

Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam.

BAADA ya jopo la wakaguzi kutoka Afrika Kusini lililokesha likiigakua filamu mpya inayotarajiwa kuleta mapinduzi ya filamu nchini ya Sanda Nyeusi, sasa filamu hiyo itaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa.
Habari kutoka kwa maafisa wa kampuni ya Kiu Investment LTD iliyotengeneza filamu hiyo zinasema kuwa, wakaguzi hao wameorodhesha sehemu kadhaa zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho ili iwe na ubora wa kimataifa.
“Filamu hii imetengenezwa kwa ajili ya kuuzika kimataifa, hivyo basi wameorodhesha sehemu zinazotakiwa kuboreshwa, kwa vile imetengenezwa katika kiwango cha kuoneshwa kwenye majumba ya sinema yenye hadhi ya kimataifa,” alisema Myovelwa Mfwaisa, meneja wa mandhari wa filamu hiyo.
Aliongeza kuwa, flamu hiyo imerudishwa studio kwa ajili ya kumaliziwa kuboreshwa sehemu zilizopendekezwa na wataalamu hao na baada ya hapo itakuwa sokoni nchini nzima na kwingineko duniani.
Filamu ya Sanda Nyeusi iliyorekodiwa mkoani Morogoro, imeigizwa kwa sehemu kubwa na Latifa Idabu, Issa Mussa ‘Cloud’, Korongo Hamis na Hashim Kambi.
Wakitoa maoni yao, wakaguzi hao waliotoka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa, Sanda Nyeusi ni hatua kubwa sana kwa medani ya filamu nchini kwa vile imekidhi matakwa mengi yanayohitajika kwenye filamu.
Reactions::

JK Kwenye Mazungumzo Na Obama



The US President Barack Obama Welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete to his Oval office in the White House this afternoon.The two Presidents and their close assistants held talks concerning bilateral relations between the two countries.President Kikwete is on weeklong working tour of United States.




President Jakaya Mrisho Kikwete, President Barrack Obama and The US Secretary of State Hillary Clinton during the official talks held at Oval Office in the White House, in Washington DC this afternoon.




President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with his host The US President Barrack Obama at the Oval Office in the White House, in Washington this afternoon.





President Jakaya Mrisho Kikwete signs a visitors book shortly after he arrived at The White House in Washington DC where he held talks with the US President Barrack Obama this afternoon(photos by Freddy Maro)
Reactions::

Thursday, May 21, 2009

Biafra Nimerudi Tena!

Niko Kinondoni Biafra. Nitakwenda popote nitakapojaliwa kwenda,lakini, siku zote nitapenda kurudi Kinondoni Biafra. Naam. Nimewasili Kinondoni Biafra jioni hii nikitokea Iringa. Habari za kusikitisha za ajali ya Dr. Mwakyembe nilizipata kwa njia ya simu njiani nikija Dar. Ilikuwa ni saa tatu na robo asubuhi nilipokuwa eneo la Mazombe, kilomita 35 kutoka Iringa Mjini. Tunamtakia kila la heri apone haraka.
Reactions::

Ajali Ya Mwakyembe Katika Picha





Shimo lililosababisha ajali ya Mwakyembe. Picha ya juu Dr. Mwakyembe akiwasili Dar kwa matibabu zaidi. Ajali hiyo ilitokea leo asubuhi enemo la Ihemi kilomita zipatazo 50 kabla ya kuingia Iringa kutokea Mbeya. Picha na Francis Godwin, Iringa.
Reactions::

Kazi

DO YOU WANT TO GROW? CAREER IN FINANCIAL SERVICES INDUSTRY?



Are you Ambitious, flexible and results driven ,Young, focused,energetic, and currently have some experience in financial services sector/industry?



Here are some opportunities to further grow your career:



Our Client, an up-coming micro financing institution operating nation wide, is looking to further expand and grow wider and increase capacity in delivering best financial services/lending to clients available nation wide.





We are now looking for people to fill in Branch Manager roles available in various locations: Mbeya, Songea, Sumbawanga, Moshi, Njombe etc



A branch manager is expected to lead own branch team and effectively manage company assests to ensure that the brach achieves its performance and efficiency targets.



Branch Manager must therefore possess a diploma/degree in business studies or equivalent, 4yrs experience in management over and above listed personal attributes. In addition must have a driving licence.




Loan officer roles are also available in similar locations. Loan Officer will be responsible for ensuring that they assist their branches to meet performance targets by ensuring that they solicit new clients and achieve their sales targets and deliver services in a professional manner.



Loan officer must possess diploma/degree in busniess studies or equivalent, have 2 years financial/banking experience or equivalent, candidates with sales experience will be considered. Driving licence a must.



How to apply:

Send your current cv only, in word document to: job.provider60@gmail.com by 23rd May 2009-05-20
Reactions::

Zain Chap Chap



Mnenguaji, Mussa Kifukwe akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Zain Chap Chap uliofanyika Dar es Salaam jana. Zain imeingia ubia na Kampuni ya Bakhressa kusambaza muda wa maongezi kupitia simu selula ili kupeleka huduma za Zain karibu na wateja.
Reactions::

Ma- Miss Wa Mjini



Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam.

KAMPUNI inayoandaa shindano la cha Miss Dar City Centre , Sisi Entertainment ya jijini Dar es Salaam , mapema leo ilitaja baadhi ya makampuni ambayo yamejitokeza kudhamini shindano hilo ambalo limepangwa kufanyika mwezi ujao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, John Doto , alitaja makampuni hayo kuwa ni kampuni ya simu Vodacom Tanzania,
Sycko Media , AMREF kupitia Angaza Zaidi na Global Publishers.

Kambi ya kitongoji cha Miss Dar City Centre ilianza siku ya Ijumaa jioni ambapo waandaaji , washiriki na mwalimu wa shindano hilo walijitambulisha kwa waandishi wa habari pale Ramada Hotel, Ilala , jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alitaja majina ya warembo ambao wamejitokeza kwenye shindano hilo ni Anne Moses (19), Neema Mashala ( 20), Caroline Izidor (18), Christine Ivan (22) na Husna Maulidy( 18).

Wengine ni Elizabeth Ernest (20), Emma James (22), Bhoke Misiwa (22), Mary Thomas (22), Judith Muro (20), Magreth Peter (21)Ziada Hemba (19), Mariam Othman( 19) na Emaster Charles (19). Washiriki wengine ni Jovina Michael (18), Mwantumu Yusuph (18), Golder Mmari(21), Catherine Rajabu (23), Everine Johan na Brender Alewis .
Warembo hao wameanza mazoezi ukumbini hapo chini ya mkufunzi wao anayeitwa Rehema R. Uzuwiy ambaye aliwahi kuwa Miss Ruvuma mwaka 1999.
Reactions::

Mahabuba



Mahabuba Yaja Kwa Kishindo

Na Mwandishi Wetu,

FILAMU iliyotamba vilivyo ya Mahabuba sasa inatarajia kuingia mtaani katika
sehemu yake ya pili. Hilo limejulikana juzi baada ya Khalfan Abdalah, Mkurugenzi wa kampuni ya Riyamy Production LTD ya jijini Dar es Salaam kubainisha hilo. Kampuni hiyo ndiyo yenye dhamana ya kusambaza filamu hiyo.

“Mahabuba Part II itaingia kwenye soko la filamu kwa mifumo ya VHS, VCD na DVD, hivyo natumia fursa hii kuwaomba mashabiki wetu wakae mkao wa kula kwa ujio wa filamu hiyo. Kama wanahitaji wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0754-665044 .” alisema Abdallah.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa wale ambao wanahitaji filamu hiyo wafike pale ofisini kwake mtaa wa Msimbazi / Magila karibu na klabu ya timu ya Simba.

Alifafanua kuwa ndani ya filamu hiyo kuna waigizaji wengi maarufu kama vile Single Mtambalike ‘Rich Rich’, Rose Ndauka, Godlivan Gordan na Jacob Steven (JB) ambao wamefanya kazi ya uhakika jambo linalomfanya awe na matumaini makubwa kwamba Mahabuba II itafanya vema sokoni.

Aidha, Abdallah alisema kuwa kampuni yake ipo mbioni kuingiza filamu nyingine tatu mpya ikiwemo Bongo Super Comedy 1 ambayo imechezwa na wachekeshaji nyota wote wa hapa Tanzania kama vile Senga, Bambo, Masele, Kiwewe, Mzee Majuto na wengineo.
Reactions::

Memorial

Reactions::

Dullayo



Combine ya longtime tu toka kitaa 'Makavu live' inakuja rasmi na tayari jamaa wameshaachia nyimbo inayowatambulisha vizuri tu inayoitwa ONGEA MWANA iliyotayarishwa na producer Vil wa V nice production, studio ambayo ilivamiwa na majambazi siku za hivi karibuni.

Makavu live imeundwa na wasanii 5 wa muziki wa kizazi kipya ambao ni Omary Muba'Omy G', Abraham Kasembe'Dullayo', Xavier Renne 'Xdizo', Pompin na Isihaka Salehe 'Eazy man'.

Jamaa walikua wanakutana maskani mitaa ya ukonga huko pande za airport wakawa wanachanana kwa ma-freestyle makalimakali ambayo walikua wanayaita makavu, ndipo walipopata familia yao iliyo batizwa jina la makavu live.

Tayari wameshafanya nyimbo nyingi tu za bongofleva mpaka za mnanda zilizotengenezwa na maproducer tofauti hapa jijini. Wanasema " kiparatuni chetu kinatusaidia sana hasa kubadilishana uzoefu katika sanaa kwani kuna wasanii kibao wenye style na skills tofauti tofauti, Mungu atatusaidia familia itakua na
tutaibua wasanii wengine wenye vipaji vilivyojificha".

Yupo mwana hiphop mkongwe, Omy G msanii mwenye sauti ya pekee aliyetoka tangu mwaka 2000 na nyimbo ya 'kindumbwendwe'akiwa na kundi la FDC, kwasasa alitoa nyingine inayoitwa 'choo cha kike'kabla ya kuachia 'Skiliza mchumba' aliyomshirikisha Dullayo, mwingine ni Dullayo anae-shine sana na 'bila yule'
akimshirikisha Mwana-Fa, pia yupo Xdizo alieachia kali yake inayoitwa 'Dhahabu zilizopotea' ikitengenezwa na Marco Chali bila kumsahau Pompin mkali wa freestyle na Eazy man anae-shine sana kwenye nyimbo yao ya mnanda inayoitwa 'maneno wapi'.

Pamoja na kuwa wapo kwenye kundi moja kila msanii yuko huru na anaendelea kusuka albam yake bila kuadhiri muungano wao. Sasaivi wapo katika mchakato wa kutangaza muungano wao, wanapiga picha za pamoja na video ya nyimbo zao mpya.

source; Makavu live, Box 25495, DSM. email; makavulive@yahoo.com
tel.0655 77 51 50
0713 36 70 34
0652 31 80 03
0717 50 03 93
Reactions::

Wednesday, May 20, 2009

Sweet Easy!

Reactions::

IJUMAA YENYE TOFAUTI: KUTANA NA FREDDY!




IJUMAA YA KUKUTANA NA MWANDISHI

Wiki hii katika mjumuiko wetu wa kila Ijumaa katika Mkahawa wa Vitabu Soma tunawakaribisha kukutana na mwandishi wetu wa mwezi Mei ndugu yetu FREDDY MACHA. Mwandishi huyu ambaye pia ana fani kadhaa za kisanii atazungumzia kitabu chake cha “Mpe Maneno Yake” ambacho ni mkusanyiko wa visa mbalimbali alivyovishuhudia katika jamii alizowahi kuishi na kutembelea. Vilevile Freddy atatumbuiza kwa nyimbo, ghani na mashairi na pia atazungumzia kwa nini uandishi na fasihi ni muhimu kwa jamii. Freddy Macha ni mwandishi na mwanamuziki wa Kitanzania anayeishi nchini Uingereza. Kwa miaka zaidi ya 30 amekuwa akiandika makala mbalimbali katika magazeti yetu hapa nchini kuhusiana na mikasa ya kijamii.

Siku: Ijumaa 22 Mei, 2009 :

Muda: Saa Kumi na Moja Jioni- Saa Mbili

Mahala:Soma Mkahawa wa Vitabu

Tafadhali njoo na daftari au shajara yako. Njoo na maswali yako. Vitabu, matini na kanda za muziki zitakuwepo dukani. Nyama choma toka mgahawani itakuwepo
Reactions::

Freddy Macha



Freddy Macha kafanya maonyesho na kuongoza semina mbalimbali za sanaa za maonyesho na fasihi miaka mingi. Hapa anaonekana akitongoa shairi lake maarufu linalokejeli urasimu katika tamasha la muziki na ushairi (“Soul to Soul”) mjini Copenhagen, Denmark, 1985. (picha na Jørn Stjerneklar).



Kitabu cha hadithi fupi fupi : “Mpe Maneno Yake” kilichochapishwa mwaka 2006 na E & D Limited Dar es Salaam kitakuwa moja ya mada husika za semina zake Freddy Macha hususan katika fani ya uandishi na maisha ughaibuni.
Reactions::

Libeneke La Ikulu!

katika upekuzi nimekutana na blogu ya ikulu
naomba wajulishwe wana jamii
http://mawasilianoikulu.blogspot.com/

Nina wito mmoja:
Je wataalam wa computer hawawezi kutusaidia kutengeneza libeneke la mkuu wetu wa nchi?
kwani hilo naona linafanana kabisa na la kwako mkuu , na mbaya zaidi lina hostiwa (hosting) na google bure!!
si vizuri kwa usalama wa taarifa za mkuu wetu.
mbaya zaidi itakuwa siku wakiamua google kukata service (kama walivyofanya zile website zilizopokuwa hosted bure na yahoo geocities)hakuna mtu wa kuwauliza kwani ni bure.
tujifunze toka kwenye tovuti za ikulu ya kenya,uganda na rwanda

asante bro

Jina:kapuni
Reactions::

Media

The International Institute for Journalism (IIJ) of InWEnt – Capacity Building International, Germany, announces its Summer Academy "Freedom and Responsibility in the Media" for young journalists to be held in Hamburg, Germany from July 26 to August 21, 2009.

Course Objectives: The Summer Academy aims at promoting media freedom and journalistic ethics by empowering young, up-and-coming journalists to make ethical decisions in their daily working routine as well as under difficult circumstances. The programme is a unique opportunity to broaden the knowledge on the key topic of press freedom, discuss professional ethical standards and reflect on their reasons of being. It seeks to cover both practical experience and profound insights into the political and ethical framework that guides the practical journalistic work.

Readmore:
http://cambodiajobs.blogspot.com/2009/05/summer-academy-freedom-and.html

--~--~---------~--~----~------------~-------~--~----~
Scholarship and Job are posted at
http://Cambodiajobs.blogspot.com
Reactions::

Tuesday, May 19, 2009

BAP: I Love This Doctor !




Q: Doctor, I've heard that cardiovascular exercise can prolong life. Is this true?
A: Your heart is only good for so many beats, and that's it... don't waste them on exercise. Everything wears out eventually. Speeding up your heart will not make you live longer; that's like saying you can extend the life of your car by driving it faster. Want to live longer? Take a nap.

Q: Should I cut down on meat and eat more fruits and vegetables?
A: You must grasp logistical efficiencies. What does a cow eat? Hay and corn. And what are these? Vegetables. So a steak is nothing more than an efficient mechanism of delivering vegetables to your system. Need grain? Eat chicken. Beef is also a good source of field grass (green leafy vegetable). And a pork chop can give you 100% of your recommended daily allowance of vegetable products.

Q: Should I reduce my alcohol intake?
A: No, not at all. Wine is made from fruit. Brandy is distilled wine, that means they take the water out of the fruity bit so you get even more of the goodness that way. Beer is also made out of grain. Bottoms up!

Q: How can I calculate my body/fat ratio?
A: Well, if you have a body and you have fat, your ratio is one to one. If you have two bodies, your ratio is two to one, etc.

Q: What are some of the advantages of participating in a regular exercise program?
A: Can't think of a single one, sorry. My philosophy is: No Pain...Good!
Q: Aren't fried foods bad for you?
A: YOU'RE NOT LISTENING!!! ...... Foods are fried these days in vegetable oil. In fact, they're permeated in it. How could getting more vegetables be bad for you?

Q: Will sit-ups help prevent me from getting a little soft around the middle?
A: Definitely not! When you exercise a muscle, it gets bigger. You should only be doing sit-ups if you want a bigger stomach.

Q: Is chocolate bad for me?
A: Are you crazy? HELLO Cocoa beans! Another vegetable!!! It's the best feel-good food around!

Q: Is swimming good for your figure?
A: If swimming is good for your figure, explain whales to me.

Q: Is getting in-shape important for my lifestyle?
A: Hey! 'Round' is a shape!

Well, I hope this has cleared up any misconceptions you may have had about food and diets.

AND.....

For those of you who watch what you eat, here's the final word on nutrition and health. It's a relief to know the truth after all those conflicting nutritional studies.

1. The Japanese eat very little fat and suffer fewer heart attacks than Americans.

2. The Mexicans eat a lot of fat and suffer fewer heart attacks than Americans.

3. The Chinese drink very little red wine and suffer fewer heart attacks than Americans.

4. The Italians drink a lot of red wine and suffer fewer heart attacks than Americans.

5. The Germans drink a lot of beers and eat lots of sausages and fats and suffer fewer heart attacks than Americans.

CONCLUSION: Eat and drink what you like. Speaking English is apparently what kills you.
Reactions::

Watanzania Wawachapa Wahabeshi 5-2



Ni Mysore, India. Bonyeza hapa upate uhondo zaidi; http://www. kilinyepesi.blogspot.com
Reactions::