Subscribe:

Friday, July 31, 2009

Kuna Ofisi Mjini....




Ni lazima uachane na jeans, na hata batiki ndipo usikilizwe! Afadhali 'enzi za Mwalimu!' Lakini kwetu Iringa hata hii leo bado unaweza kuingia kwa RC ukiwa umetinga Jeans na batiki huku vumbi la shambani likionekana hadi kwenye viatu.
Reactions::

Dar Leo Asubuhi

Kilwa Rd. Kushoto ni Shule Ya Sekondari Jitegemee
Reactions::

Jitegemee

Wanafunzi Wa O-Level Wa Shule Ya Sekondari Jitegemee
Reactions::

Sweet Easy!

Reactions::

Thursday, July 30, 2009

Warembo



Pichani ni warembo watakaochuana siku ya tarehe 7/8/2009 ijumaa, pale yatch club kwa mpambano mkali wa kumsaka, atakae mvua taji Nasreen Karim 2009.mchuano unaonekana kuwa mkali kwani washiriki woote wako bomba saaana!! JE KANDA YA ZIWA INAWEZA KUTOA TENA MISS TANZANIA? MATUMAINI YAPO TUNAWAOMBEA WAFANYE VUZURI HESHIMA IRUDI TENA KANDA YA ZIWA. kwa picha zaidi waingie florasalon.blogspot.comAsante
Reactions::

Mkutano Wa Watanzania Afrika Kusini

Mkutano wa kuanzisha jumuia ya watanzania katika Jimbo la Gauteng

Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng (Johannesburg na Pretoria) wanatarajia kufanya mkutano wa kuanzisha jumuia yao tarehe 22 mwezi wa Agosti 2009 jijini Johannesburg.
Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu jumuia hii pamoja na kuchagua viongozi wa kudumu.

Watanzania wanaoishi kwenye miji ya Johannesburg na Pretoria ambao wangependa kuwa wanachama na pia kushiriki kwenye uchaguzi wa uongozi wa jumuia wanakaribishwa kuwasiliana na wajumbe wafuatao kwa maelezo zaidi:

Brian Mshana b_mshana@yahoo.com
Laurean Rugambwa bwanakunu@gmail.com
Faustine Ndugulile drfaustinen@aol.com

Shukrani

KAMATI YA MAANDALIZI
Reactions::

Mtoto Ametoweka Nyumbani Iringa



Maggid,

Tafadhali kwa msaada wako ktk tovuti yetu na blog.

Mtoto Omary Jamal Mwinyibohari wa Miyomboni Iringa,ametoweka nyumbani kwao Iringa tangu tarehe 28 July,2009.Ripoti ya Polisi No.IR/RB/3449/2009
Ana umri wa miaka 12 na anasoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Wilolesi,Iringa Manispaa.
Yeyote atakayemuona awasiliana na Naim Mwinyibohari 0782 55 75 92, Saad 0718 99 29 39,
Seif Rashid 0755 98 40 77,Dr.Zaytun 0787 52 71 70.
Reactions::

Dar Leo Asubuhi

Posta Ya Zamani
Reactions::

Posta Ya Zamani

Reactions::

Mr. Chiwanga

OCTOBER 24,1972:The Minister for National Education, Mr Simon Chiwanga, returns from Paris Where he attended the 17th session of UNESCO. On the same flight was the Principal Secretary in the Ministry of Foreign Affairs,Mr A.Nyaki (behind Mr Chiwanga,(Daily News Archives)
Reactions::

Wednesday, July 29, 2009

Utamu Wa Boga Ule Kwa Vidole!




Leo nimekumbuka kwetu Iringa. Pichani nilipokaribishwa boga la kuchemsha kitongoji cha Mwangata, Manispaa ya Iringa mwaka jana.
Reactions::

Leo Magazetini Kurudi Hewani Kesho Alhamisi

Huduma hiyo imekosekana kwa siku kadhaa sasa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Najitahidi kuhakikisha inarudi hewani kesho alhamisi,inshallah.
Maggid
Reactions::

Tuesday, July 28, 2009

Mbwa Wa Manzese


Makala hii ilichapwa na KJ namba 17 ( toleo la wiki jana). Kuna baadhi wameshindwa kuisoma vema kwenye website na blog kutoka kwenye copy ya gazetini. Naiingiza tena humu. Pichani ni mama mchoma mahindi wa Mpwapwa, Dodoma.

Tusome alama za nyakati:

Mbwa wa Manzese

NAKIKUMBUKA kisa alichopata kusimulia Mwalimu Nyerere kunako mwanzoni mwa miaka ya 80. Ilikuwa ni kwenye kilele cha sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi pale uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam.

Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi ikiwamo mishahara midogo na mengineyo.

Wakati huo Serikali chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

Ilipofika wakati wa kutoa hotuba Mwalimu Nyerere alisema;

“ Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay aliyenenepeana na manyoya yanayoteremka machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese aliyekondeana . Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; “ Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!

- Naam, miye ni mbwa kama wewe.

- Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi.

Mbwa wa Manzese akajibu; “ Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!”

Kisa kile alichosimulia Mwalimu kilikuwa ni cha kifalsafa. Naamini katika alichokisema Mwalimu, nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Neno uhuru lina maana kubwa ingawa ni neno fupi sana. Asiye na uhuru ni mtumwa.

Leo hii naandika kwa furaha kuwajulisha kuwa nimeng’atuka kufanya shughuli za kiutendaji katika gazeti hili la KWANZA JAMII nililoshiriki kuliongoza tangu mwanzo wake hadi kufikia toleo la 16 juma la jana. Hakuna Jumanne ambalo halikufika mitaani tangu toleo la kwanza. Naam. Ni miezi minne ya kazi ngumu. Umefika wakati wa kuwaachia wengine ili nifanye mengine.

Nawashukuru kwa dhati kabisa wachangiaji wa makala na habari katika gazeti hili. Wengi wao wamejitolea na wanaendelea kujitolea. Wanaandika bila kulipwa chochote. Wanajitolea kwa jamii yao, kwa nchi yao. Hawa ni ‘ wapiganaji’, wanawake kwa wanaume, ambao bila kujitolea kwao, hakika gazeti hili ulisomalo lingekuwa marehemu mwezi mmoja tu baada ya kuanzishwa kwake.

Kwenu nyote mnaolitakia mema gazeti hili na nchi yetu kwa ujumla, tukae tukijua, kuwa mapambano ya kuipigania Tanzania na hata kulifanya gazeti hili liendelee kuwapo mitaani bado ni magumu sana. Hatuna sababu ya kukata tamaa.Tukishindwa kukimbia tutembee, tukishindwa kutembea tutambae.Na hata tukishindwa kutambaa, tupambane mpaka risasi ya mwisho, mpaka pumzi ya mwisho.

Ni nani basi anayechukua nafasi yangu?

Kijana Benedict Sichalwe amechukua rasmi jukumu langu kama mwenza. Sichalwe ana msimamo, hana makundi na anaheshimu maadili ya taaluma yake. Alianzia katika gazeti la Dimba mwaka 1993 na kwa sasa ametokea katika jarida la RAI baada ya kumaliza mkataba wake.

Binafsi nimejifunza mengi katika kuliongoza gazeti la kada hii ya KWANZA JAMII. Kuna walionisaidia bila kunipa masharti yeyote, nawashukuru sana. Nawashukuru pia hata wale walioonyesha utayari wa kunisaidia ingawa kwa masharti. Niliyakataa masharti yao kwa kutamka huku nikiwatazama usoni, bila kuwaonea haya.

Anayenifahamu anajua kuwa naweza kukubaliana na kufanya kazi na yeyote yule katika kilicho na maslahi kwa nchi yetu bila kujali itikadi, dini , rangi au kabila la muhusika. Nitafanya hivyo hata kama kwa kujitolea tu.

Ukweli sina chama, na sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Sina makundi. Nina marafiki karibu katika vyama vyote vikubwa vya kisiasa hapa nchini. Wakati wa mchakato wa uchaguzi wa 2005, kwa kuandika makala mbili za kumwelezea Dr. Salim Ahmed Salim na nyingine kupinga ubaguzi wa kisiasa uliofanyika dhidi yake, basi, kuna walioamini kuwa nilikuwa mmoja katika kambi ya Dr. Salim. Ukweli sikumfahamu Dr. Salim kwa kukutana naye hadi Februari 5 mwaka huu nilipomtembelea na kukutana naye kwa mara ya kwanza ofisini kwake. Azma yangu kuu ilikuwa ni kusalimiana na kufahamiana naye, basi.

Siku zote naamini, kuwa kama thamani ya mwandishi haijulikani, basi, mwandishi huyo ana thamani kubwa, na kinyume chake. Hakuna anayejua thamani yangu kwa maana ya bei ya kuninunua.

Nilipoanzisha jarida la michezo la GOZI SPOTI sikuzungumzwa sana. Gozi Spoti lilidumu kwa mwaka mmoja. Ajabu nilipoanzisha gazeti hili la KWANZA JAMII , haraka nikasoma mitandaoni watu wakinijadili. Ikasemwa kuwa KWANZA JAMII linamilikiwa na mafisadi, hivyo basi hata mimi nimenunuliwa na hata kuitwa fisadi.

Kila mtu ana uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni yake. Naheshimu uhuru huo na nitaendelea kuupigania. Hata hivyo, waliozungumza hayo juu yangu ni watu wasionifahamu. Nami sikupoteza hata dakika moja kulumbana na watu wasionifahamu na wala wasiojitambulisha kwa majina yao halisi.

Baadhi ya wanaonifahamu wanajua nilianzisha na kuendesha gazeti nikiwa kidato cha pili shuleni pale Sekondari ya Tambaza. Niliandika kwa kalamu ya wino na kwa mkono katika karatasi za A-4. Niliweza kubandika kwenye ubao wa matangazo kile nilichoandika, kikasomwa na wanafunzi wenzangu hata walimu . Hiyo ni historia yangu pia. Ninajivunia nayo.

Nitafanya nini sasa?

Nitabaki kuwa mwandishi wa makala kupitia safu hii. Kuna mengi ya kuandika, na nina azma ya kuandika kitabu. Maana, katika miaka yangu ya uandishi, nimekutana na watu wa kada mbali mbali. Mathalan, kuna bwana mmoja mwenye dhamana ya uongozi alipata kuniuliza; hivi wewe unaandika ili kumfurahisha nani?

Mwezi Novemba, 1996 nilikuwa kijijini Ilula, Rais Mkapa akiwa na mwaka mmoja madarakani alikwenda huko kufungua mradi wa umeme uliokamilika. Kwenye hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa wakati huo, Bw. Nicodemus Banduka alimwambia Mheshimiwa Mkapa kuwa mkoa umemwandalia ng’ombe wawili wa maziwa. Watasafirishwa kwa njia ya gari kwenda Ikulu. Ilikuwa ni zawadi ya ng’ombe si kumfurahisha Mkapa, bali kujipendekeza kwa Mkapa. Nani alimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa Rais ana shida ya maziwa?!

Hivyo basi, swali nililoulizwa na Bwana yule lilikuwa; “hivi wewe unaandika ili kujipendekeza kwa nani? “ Kitabu nitachoandika kitaitwa ‘Ng’ombe wa Ikulu’. Ni mkusanyiko na mwendelezo wa fikra zangu. Natumaini nitaishi kukiandika na kukichapa. Ahsanteni.

0788 111 765



Reactions::

Huduma Ya Leo Magazetini Kurudi Hewani

Wakati wo wote kuanzia leo.
Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

Monday, July 27, 2009

KWANZA JAMII JUMA HILI




Reactions::

Leo Hakuna Habari Magazetini!

Kwa wale mlioanza kuzoea huduma ya kusoma habari za magazetini kupita blogu hii nasikitika leo hakukuwa na habari hizo. Nimeayaangalia magazeti yote ya leo sikuona lenye habari! Na hiyo ndiyo habari kubwa! ( UTANI) .

Tukiacha utani, habari hizo hazikuwafikia leo kutokana na sababu zisizozuilika. Inshallah, kesho tunaweza kuendelea.

Maggid
Reactions::

Jumatatu Yangu Inaanza Hivi...


Taratibu kabla sijaanza kuvuta kasi!
Reactions::

Sunday, July 26, 2009

Huko Sweden Hivi Ndivyo Mnavyoegesha Magari?!


Au ndio ukienda Roma fanya kama Waroma!
Reactions::

Saturday, July 25, 2009

MSIBA TANZANIA NA UJERUMANI

NDUGU,JAMAA, MARAFIKI NA WADAU WA BLOG HII YA JAMII,

NINGEPENDA KUWATAARIFU YA KUWA NIMEPATWA NA MSIBA WA MAMA YETU MPENDWA BI KHADIJA( NADIA) OMARY ARUBATI AMBAYE AMEFARIKI DUNIA SIKU YA IJUMAA MCHANA TAREHE 24.07.09, MSIBA HUPO KINONDONI NYUMBANI KWA MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MHESHIMIWA BWANA SALUM LONDA NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA LEO SIKU YA JUMAMOSI SAA SABA MCHANA KATIKA MAKABURI YA KISUTU.


MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MPENDWA MAMA YETU MAHALA PEMA.


AMIN


Allah says in the Qur'an (2:152-156):


“Fadhkurunii adhkurukum, washkuru lii walaa takfuruwn* Yaa ayyuhal-ladhiina aamanuu! sta’inu bi swabiri was-swalaah, innallaha ma’aswaabiryn* Walaa taquuluw liman yuqtalu fiy sabilillah amwaatum bal ahyaau, walaqil-laa tash’uruun* Wa lanabluwannakum bishay-in minal khaufi waljuu’i, wa naqswim-minal amwaali wal amfusi wa-th-thamaraat, wabash-shiris-swabiriyn* Alladhyna idhaa aswaabat hum muswyba, qaalu innalillahi wa inna ilaihi raaji’uun”


Therefore remember Me, I will remember you; and be thankful to Me and do not be ungrateful to Me. O ye who believe! seek help with patient perseverance and prayer; for Allah is with those who patiently persevere. And say not of those who are slain in the way of Allah: "They are dead." Nay, they are living, though ye perceive (it) not. And We will most certainly try you with somewhat of fear and hunger and loss of property and lives and fruits; and give good news to those who are patient. Who, when a misfortune befalls them, say: Surely we are Allah's and to Him we shall surely return.






Malumbo S.Malumbo
Reactions::

Friday, July 24, 2009

Ali Hassan Mwinyi

MAY 27, 1988: Ghanaian Leader Jerry Rawlings Talks With President Ali Hassan Mwinyi During OAU Summit In Addis Ababa (Daily News Archives)
Reactions::

Punguzo La 50%! ARISE BEAUTY

Habari za leo MTEJA



Tunapenda kukujulisha kua tuna punguzo la 5% hadi 50% kwa baadhi ya vitu dukani. Orodha ni ndefu sitaweza kuwapeni kwenye ujumbe huu (na tovuti www.arise-tz.com haina orodha yote) tunaomba tembelea kwenye maduka yetu upate chaguo lako.



Tembelea tovuti yetu www.arise-tz.comTuna bidhaa za wanaume na wanawake

Perfume za kike na kiume unajaribu /unajipulizia dukani ujue kama unapenda harufu kabla ya kununua

Deodorants za kike na kiume

Foundation na vipodozi vya kila aina.



Kama una OILY skin au dry skin

kuna mtaalamu wa make upping na facial kwa ushauri.



Tuna products za Mary Kay, Victoria's Secret, Avon, MAC, Bath + Body &Works, LA Girl nk



Tutembelee sasa (tuna location 2) ili umweleze na mwenzako kuhusu punguzo hili.





Kama ujumbe huu umekuudhi au tumetuma zaidi ya email moja tafadhali tusamehe!!



Wasiliana na



Rose B. Gaspar

Meneja Mkuu

0784 521171

0784 456046, 0753 335011



Tuna Location 2 hapa Dar

LOCATION #1:
Shekilango Rd; SINZA MAPAMBANO "MADUKA YA BLUE", pembeni mwa LILY'S BAR na inatazamana na ukumbi mdogo wa UTOJI HALL


LOCATION #2:
MIKOCHENI KARIBU NA KWA MWALIMU-
JUED BUSINESS CENTER
Direction:
Kutokea Rose Garden, ukifika TALK of the TOWN jengo linalofuata linaloangaliana na Saleeka Apartments. Pembeni ya ARISE BEAUTY SUPPLY kuna ATM ya CRDB. Ukienda mbele kidogo unafika kwa Mwalimu.
Reactions::

Thursday, July 23, 2009

Tuujadili Ukatili Huu



Sikatai kwa asilimia 100 kuchapa mtoto kiboko cha maonyo, lakini inapofikia hatua kama hii, kweli kuonya kwa kiboko ni fundisho ama ni ukatili?
Huyu ni mtoto wa kike, amechapwa na mwalimu wake wa kiume, ni katika Sekondari moja huko Iringa, imetokea jana July 22, 2009, mtoto akaogopa kwenda polisi au hospitali kwa kuhofia kwa mwalimu atamwadhibu zaidi. Aliyenitumia picha hii anasema kisa cha kuchapwa hivi ni hasira iliyojificha kwa mwalimu huyo kwa kushindwa kutimiza azma yake nyingine toka kwa binti huyu.
Nimetumiwa picha hii toka Iringa, aliyenitumia hajajua jambo muafaka la kufanya, naomba kuweka kwenu ili watu wajadili na kutoa mapendekezo kipi kifanyike kuhusiana na hali hii.
Mapendekezo yenu nitayafikisha kwa aliyenitumia picha hii kwa hatua zaidi atakazoweza kuchukula kulingana na maoni yenu.
.end.
Subi
Reactions::

Dar Leo Asubuhi

Kigamboni
Reactions::

Kigamboni


Reactions::

Kulikoni?

23,Julai 2009
Reactions::

Sokoine

June 19,1978: Defence Minister Edward Moringe Sokoine (right) Opens OAU Liberation Committee in Dar es Salaam(Daily News Archives)
Reactions::

" Mashine Hiyo, Kazi Kwenu!"



Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dr.Leslie Mhina mashine ya kuhudumia watoto wachanga(Suction pump) na vitanda vya kujifungulia mama wajawazito katika hafla fupi iliyofanyika katika hospitali kuu ya Kitete jana(Jumatano).
Reactions::

" Haya Ilikwendaje?"



Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete akimjulia hali Bi.Zuhura Jabu na mwanaye mchanga Mariam Sihaba aliyejifungua muda mfupi katika Hospitali ya Kitete ya Mkoa wa Tabora jana wakati Mama Kikwete alipotembelea wodi ya wazazi katika hospitali hiyo.(Picha na Freddy Maro).
Reactions::

Wednesday, July 22, 2009

Likizo- Kazi Inaendelea!



Kuna wanaoniuliza kama nimehama Iringa,la hasha, sijahama. Niko likizo- kazi Dar Es Salaam. Nafanya kazi zangu na wakati huo huo natafuta muda wa kukutana na kuongea na baadhi ya watu wa Dari Salama. Kuna mengi ya mjini nahitaji kuji-update. Isitoshe 2020 ni mwaka wa uchaguzi. Naitafuta misingi ya kujenga hoja ya Kinondoni- Biafra kujitenga na Magomeni, Mwenge na Sinza na hivyo kuwa jimbo la uchaguzi ifikapo 2020! ( Hilo la mwisho ni utani kwa wale wasionielewa ninapofanya utani!)
Reactions::

Dar Leo Asubuhi

Posta Mpya.
Reactions::

Pweza

Reactions::

Mwaliko

Kwa Watanzania wote na marafiki zetu,

Kamati ya chama cha kirafiki kati ya Finland na Tanzania inayo heshima kubwa kuwakaribisha Watanzania / Wafini wote pamoja na familia na marafiki zao kwenye pikniki itakayofanyika tarehe 26/07/2009 kuanzia saa 6.00 (sita) mchana, katika kisiwa cha Iso Vasikkasaari.

Maelezo ya jinsi ya kufika sehemu ya pikniki Iso Vasikkasaari unaweza kuyapata hapa:
http://www.espoo.fi/default.asp?path=1;28;11866;15440;16054;16056

Sehemu nzuri ya kuondokea ni kutoka Nokkala, Matinkylä Nokkalanpuistontie ambako boti inaondoka kwa ratiba ifuatayo:
Nokkala - Iso Vasikkasaari: 10.30, 11.45, 12.30, 13.45, 14.30, 15.45, 16.30, 17.45, 18.30

Kutoka kisiwani boti litaondoka kwa ratiba ifuatayo:
Iso Vasikkasaari - Nokkala: 12.00, 13.15, 14.00, 15.15, 16.00, 17.15, 18.00, 19.15, 20.00

Gharama ya tiketi ya usafiri wa kwenda na kurudi kutoka kisiwani ni Euro 4, bure kwa watoto wote chini ya miaka 7.

Jitokezeni kwa wingi katika siku hii muhimu ili tupate kufahamiana na kujumuika pamoja kama familia.

Tafadhali kamati itashukuru kama utamjulisha yeyote ambaye hajapata taarifa hii.

Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga namba: 040 7333397 / 040 5892123
Reactions::

Tuesday, July 21, 2009

Varsity Colleges

LIBENEKE LA VARSITYCOLLEGE TANZANIA

Mtandao wako wa wasomi Tanzania (www.varsitycollegetz.ning.com) unapenda kukushukuru kwa ushiriki wako wa kuchangia mada mbalimbali pamoja na kupost sholarships na nafasi mbalimbali za kazi. Hii yote ni katika kusaidiana watanzania sisi kwa sisi katika swala zima la elimu na maendeleo.

Tunachukua nafasi hii kuwakaribisha tena wadau kujiunga nasi kuendeleza libeneke la elimu nchini. Karibu upate information juu ya scholarships, kazi, na ujuzi mbalimbali. Karibu utoe mada na uchangie mada na wasomi wenzako.

Vile vile tunatoa ushauri wa bure kuhusu maswala mbalimbali ya elimu nje ya nchi. Karibu sana www.varsitycollegetz.ning.com

A.Kitogo
Reactions::

Watanzania Waingia Mitini Sweden

No trace after Gothia Players
The five players from Tanzania reported missing after the Gothia Cup is not found. The other team went home on Monday.

The missing players were born between 1990 and 1993 and played all of the same law.
According to Nils Lundqvist, polisinspektör the Forensic Unit, it is not unusual with disappearances during the tournament.
- It is the usual rubbish after Gothia. Each year, we have lost young people. There are a handful of sticks, mostly from African countries, "he says.
The police are sticking to an active investigation after people, but calls for them and then they become an issue for the Swedish Migration Board. It is not a crime.
- Staying in the hope to get it better, I do not know how we would look at it. Then when the visa expires, it can be no question of wrongful-support, "says Nils Lundqvist.
He said that a Lebanese team did last year.
2002, a number of girls from Tanzania's law. Four years later two of them worked as prostitutes in Gothenburg. Such a scenario is rarely in the head of the person who deviates from their team during the tournament.
- We hope to be able to support themselves as good footballers. It is well thought, "says Nils Lundqvist.





Malumbo S.Malumbo
Reactions::

Mjini Hapa! Hapo Ni Wapi?

Reactions::

Monday, July 20, 2009

And The Opposite.....


... Yes, Sir!
Reactions::

Connected!

Reactions::

Old Boys!



Niko na Makamu wa Rais wa TFF, Othman Nyamlani. Nilimtembelea jana Jumapili asubuhi pale White Sands Hotel. Wako kwenye semina elekezi ya FIFA. Othman naye ni class-mate na rafiki wa siku nyingi tangu enzi zile za Tambaza Boys Secondary School.
Reactions::

Dar Leo Asubuhi

Temeke
Reactions::

Kurasa Za Ndani





Reactions::

Temeke

Kituo cha usalama
Mwisho wa lami
Reactions::

Sunday, July 19, 2009

Kina Klothing


Salaam kwa wadau wote wa blogu hii.

Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa tumefungua duka letu mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia www.kinaklothing.com

Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.

Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.

Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.

Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.

Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.

Tutembelee www.kinaklothing.com na tuambie mawazo yako.

Pia usisahau kujiunga nasi katika ukurasa wetu ya facebook (http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819) na kutufuatia katika http://www.twitter.com/kinaklothingKaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni.

Amani.

Mkuki na Susan (Kina Klothing)
Reactions::

Saturday, July 18, 2009

Friday, July 17, 2009

Thursday, July 16, 2009

Dr. Mathew Mwanjali- ' Kiboko Cha Kipindupindu'



Leo nilikuwa na mazungumzo marefu na Dr. Mathew Mwanjali pale Kunduchi Beach Hotel. Dr. Mwanjali ni Meneja Mradi wa ' Safe Water System unaoendeshwa na PSI'. Dr.Mwanjali ndiye aliyeongoza mapambano ya kukitokomeza kipindupindu jijini Dar. Walipoanza mradi wao mwaka 2006 kulikuwa na wagonjwa 15000 na vifo 300 vya wagonjwa. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, wakabaki wagonjwa wasiozidi mia na hamsini na bila kifo. Kwa sasa hofu ya mlipuko wa kipindupindu Dar ni historia, haipo. Kwa sasa Dr. Mwanjali na wenzake wameingiza componets nyingine katika mradi wao ili kuwasaidia waathirika wa UKIMWI.

Dr. Mwanjali na mimi tumekulia 'kijiji' kimoja- Kinondoni Biafra. Tumesoma darasa moja pale Tambaza Sekondari. Tumetembea kwa miguu kwenda na kurudi shuleni Tambaza Sekondari, enzi hizo tukiwa na akina Taki Mussa, Benedicto Ndomba na wengineo. Hakika,sote ( Mwanjali na mimi) tulifurahi sana kukumbushana ya enzi hizo za ' kijijini' Biafra na Tambaza ya Mzee wetu marehemu Kalumuna aliyekuwa Mkuu wetu wa Shule.
Reactions::