Subscribe:

Monday, August 31, 2009

Hapa Ndio Sinza Kwa Wajanja!




Kuchaji simu na betri maana yake nini?
Reactions::

Sunday, August 30, 2009

BREAKING NEWS!! Zitto Hatogombea Uenyekiti


( Picha hiyo juu niliipiga mwezi Agosti mwaka jana wakati Zitto Kabwe alipohutubia wananchi wa Iringa.)Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ndani ya CHADEMA Zitto Kabwe leo usiku amelazimika ( shwa?) kutoa jina lake katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Uenyekiti Taifa ndani ya CHADEMA. Mbowe sasa atapigiwa kura za NDIYO au HAPANA na wajumbe wa mkutano mkuu. Swali ni je, Zitto atakipa mgongo chama chake?
Reactions::

Saturday, August 29, 2009

Friday, August 28, 2009

Che Guevara Alilala Wapi Dar Es Salaam?



Nimekisoma kitabu kiitwacho " The African Dream"- The diaries of the revolutionary war in the Congo. Ama hakika ni kitabu chenye maelezo yenye kusisimua, kufurahisha na kusikitisha juu ya mwanamapinduzi Che Gueavara na harakati zake za mapambano ya ukombozi wa kimataifa. Ni kweli kuwa Che aliingia Dar April 1965 na alikutana na Nyerere ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Congo Mashariki.

Hata hivyo, katika kitabu hicho Che hakuweka wazi jina la hotel aliyoishi alipokuwa Dar. Lakini kwa Dar ilivyokuwa hata miaka ya 70 ambayo nami nina kumbukumbu ya kutosha kwa kuona, basi,kulikuwa na restaurants nne pale katikati ya jiji ambazo nami nimeziona kwa macho na nimepata kuingia mara kadhaa utotoni, nazo ni Zahir Restaurant ( Sasa New Zahir Restaurant iliyo Mtaa wa Msikiti). Ni Restaurant hii ambayo Che alikwenda mahali hapo kwa chakula na chai. Kulikuwa pia na Royal Restaurant na Nakhuda Restaurant zote zikiwa Mtaa wa Jamhuri. Restaurant ya nne iliitwa The Khalid pale mtaa wa Kipande.

Hitimisho. Kama Che Guevara alikunywa chai na kula chakula Zahir Restaurant,basi,yawezekana kabisa aliishi Zahir Guest House iliyokuwa nyuma ya mgahawa huo. Kwanini hilo halikuwekwa wazi katika kitabu cha kumbukumbu zake ziwezi kujua,maana siamini kama aliishi kwenye moja ya hoteli za gharama jijini Dar kwa vile hakutaka hata kwenda New Africa Hotel ambapo ndio ilikuwa kijiwe cha akina Abeid Karume na wapigania ukombozi wengine. Che Guevara hakutaka kabisa kuonekana na mawakala wa CIA.
Reactions::

Huduma Ya Leo Magazetini Itaendelea Jumanne

Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

Salum + Maimuna = KWELI !



Waliosema hayawi,sasa yamekuwa! Ndoa ilifungwa siku ya Jumamosi 15 August 2009 Mjini Mtwara kati ya Bw. Salumu Kafuku na Bi. Maimuna Shomari. Hongera sana!
Reactions::

Anakumbukwa: Coll James Mtoto Wa Dandu




Poleni na hongera za Ramadhani. Mbali ya matatizo yote, nilikuwa naomba jambi kwako ili tumkumbuke James Maligisa Dandu aka Cool James aliyetutoka kwa ajali miaka saba iliyopita. Nafikiri wengi bado tunamkumbuka na tutaendelea kum- miss. RIP CJ.
Blackmpingo
Reactions::

Kijiwe Unakitengeza Mwenyewe!



Pichani ni Ahmed Viriyala, mchora katuni wa KWANZA JAMII, ni rafiki yangu. Amezama kwenye kurasa za gazeti. Kisutu jana jioni.
Reactions::

Thursday, August 27, 2009

Aboubakar ' Sure Boy' Salum!




Nimekutana naye leo mitaa ya 'mjini mjini'. Huyu jamaa hakuwa wa kawaida enzi zake. Naikumbuka mechi ile ya Taifa Stars na Sudan pale National Stadium. Zikiwa zimebaki dakika tatu mpira kwisha tulikuwa tumelala bao moja bila. Watazamaji walishaanza kutoka kiwanjani. Nilimwona Aboubakar akipokea pasi winga ya kulia kuelekea goli la Kaskazini. Alikuwa akiondoka kwa kasi na mpira unaodundadunda huku akiwaacha kwa chena mabeki wawili wa Sudan. Kufumba na kufumbua Aboubakar alipachika bao safi la kusawazisha.

Wakati bado washabiki tunafurahi bao hilo Aboubakar Salum aliondoka tena na mpira kutoka winga hiyo hiyo ya kulia na kufanya maajabu mengine. Aliwalamba chenga mabeki wa Sudan na hatimaye akafunga bao la kihistoria katika dakika ya mwisho ya mchezo. Tangu siku hiyo,Aboubakar Salum akapachikwa jina la ' Sure Boy'. Hata nilipokutana naye leo akitokea ' winga ya kulia' ya mtaa nilijikuta nikimwita kwa sauti " Sure Boy!". Ilikuwa ni baada ya kumpiga picha ya mbali bila ya yeye kubaini. Naam. Nasi tuliwahi kuwa 'Taifa Kubwa'katika soka. Kidogo kidogo tumeanza kurudi katika ramani ya soka baada ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne ya JK katika kuinua na kuboresha kandanda. Inawezekana kama tutajipanga vema.
Reactions::

Watani Zetu Yanga Walikuwa Na Tatizo La Jezi!



Jezi zao zilikuwa za ovyo kabisa na wakalazimika kuweka jina la sabuni za mfadhili wao. Simba hatukuwa na tatizo hilo. Kila tukiingia tulipiga ' uzi' wa nguvu kama tulivyoita wakati ule. Hata hivyo,kikosi hiki cha Yanga ndicho kikosi bora Young Africans wamepata kuwa nacho. Enzi hizo nipokwenda kwenye mechi ya Simba na Yanga nilikuwa sina raha na first eleven ya Yanga. Aboubakar Salum ' Sure Boy' ni wa pili kutoka kushoto kwa waliochuchumaa.
Reactions::

Profesa Joseph Mbele Yuko Mjini!




Leo nimekutana na Profesa Joseph Mbele anayefanya kazi nchini Marekani na ambaye yuko nchini kwa sasa kwa ' Likizo- Kazi' fupi. Nilibahatika kumkaribisha chakula cha mchana pale kwenye mgahawa wa Makumbusho. Tulikuwa na mengi ya kuzungumza.
Reactions::

Profesa Anayemkubali Profesa Wa Jarida la Sani!



Profesa Joseph Mbele amenibainishia kuwa yeye ni mpenzi wa jarida la Sani la hapa Bongo, hususan katuni za akina Madenge, Pimbi, Lodi Lofa na Profesa Ndumilakuwili. Anasema akiwa Marekani anakosa sana uhondo wa katuni hizo. Katika katuni zote hizo Profesa Mbele anamkubali sana 'Profesa mwenzake', yaani Profesa Ndumilakuwili. Profesa Ndumilakuwili hupata shida sana katika kufanikisha mipango yake pamoja na kutumia akili yake ya kuzaliwa katika kuipanga mipango hiyo. Nilimwahidi Profesa Mbele kumnunulia gazeti la Sani na kumkutanisha na msaanii anayechora katuni ya Profesa Ndumilakuwili Bw. Ibrahim Washokera.
Reactions::

Mdharau Asili Yake Mtumwa!



Nikifika kijiji cha Makumbusho namkumbuka bibi yangu Amina Binti Muhando Mwaruka na chakula chake kitamu alichokiivisha chunguni.
Reactions::

Kama Unataka Vitamu Vya Asili.....



Nenda Kijiji Cha Makumbusho,Kijitonyama.
Reactions::

Haki Ya Mungu: Huyu Ndiye Haki Ngowi!



Pichani kulia akiwa na kijana mpita njia aliyefurahia kuwapo kwenye picha tu. Nimekutana na Haki Ngowi kwa mara ya kwanza leo kwenye mitaa ya katikati ya Jiji la Dar Es Salaam. Nimefurahi kupata bahati ya kugongana naye ana kwa ana. Vinginevyo tumekuwa tukiwasiliana na emails na kuchati tu.
Reactions::

Leo Magazetini





Reactions::

Kurasa Za Ndani






Reactions::

Tatizo La 'Watani Wa Jadi 'Ni Kujifanya Wasomi!

Hakika mimi nimekuwa nikiingia katika blog yako kila asubuhi na nimefurahishwa sana na jinsi unavyotumia jambo hili kutangaza maeneo mengi ya taifa lenu la Tanzania.Nilipata kufahamu kuhusu blog yako nilipoiona katika blog ya Mama Chemi(swahilitime).

Tangu wakati huo sijui ni kwanini lakini nimekuwa nikifurahia sana stori zako za Bagamoyo na Iringa pamoja na Morogoro.Yaani wewe huwa unatembea sana.Hili linanifurahisha sana.

Mimi niliwahi kuwasiliana sana na Chemi na ni yeye aliyenifanya nikafanikiwa kuunda blog yangu ambayo inajulikana kama MWEWE.

Ukienda katika blog ya swahilitime utaiona kule.Au ukiitaka kuingia na kuangalia unenda www.mhimili.blogspot.com

Blog hii ni yangu na ingawa ninajaribu,bado ni mchanga sana kwa mambo haya na hapa Kenya mawasiliano ya blog bado yako chini sio kama nyinyi wenzetu.Tatizo la Wakenya ni kujifanya wasomi na kupuuza kiswahili.Hili ni tatizo sugu.

Kazungu Samwel

Mombasa
Reactions::

Hii Ni Zaidi Ya Kupitisha Macho!




KWANZA JAMII lina wapenzi wake, Biharamulo hadi Bagamoyo. Pichani ni jamaa niliyemnasa jana mchana pale Bagamoyo akiwa amezama kwenye KWANZA JAMII. Kwa vile nilijiridhisha kuwa alivutwa sana na KJ niliamua kumnunulia nakala moja akasome kwa kutulia nyumbani au kijiweni na wenzake. Ni wengi wanaoishia kusoma vichwa vya habari kwa vile hawana uwezo wa kununua magazeti.
Reactions::

Thabeet Ameamua Kurudi Na Kubaki Nyumbani



Alipata kuishi Japan,ameamua kurudi na kubaki nyumbani.Anaendesha biashara yake ya spea za magari na pikipiki.Duka lake linaitwa Lumumba.
Reactions::

Mti Huu Ukikatwa.....



Na sehemu ya mji wa Bagamoyo itakuwa imekatwa. Ni mmoja wa miti ya zamani sana katika mji huo. Ni sehemu ya utambulisho wa mji huo.
Reactions::

Wednesday, August 26, 2009

Futru Na Mjadala



Leo jioni nilikula futari pale New Zahir Restaurant. Mahala pale wanakuja watu wa kada aina mbalimbali. Leo ilianzishwa mada ilikotea haijulikani,ilihusu waraka unaosemwa unaoandaliwa na Waislamu. Kila mmoja alisema lake, na mpaka naondoka pale New Zahir sikupata kujua uhakika wa chanzo cha habari ile. Baadae usiku huu nimesikia ikikanushwa na BAKWATA kuwa haihusiki na waraka huo.

Mahali pale, New Zahir Restaurant iliyopo mtaa wa Msikiti katikati ya jiji pana historia isiyojulikana na wengi,nilipata kuandika juu ya jambo hilo;

Kwamba Che Guevara aliwahi kutembelea mara kadhaa mgahawa huo wa ' Zahir Restaurant' kama ulivyojulikana wakati huo. Inasemekana Che Guevara aliingia Dar April 1965, alikutana na Nyerere na kupata baraka zake kuhusiana na ajenda yake ya kwenda Congo kuwasaidia wapiganaji wa Congo katika harakati za kuikomboa nchi yao. Che aliingia Mashariki ya Congo akiwa na kikosi cha askari 100; Hawa ni Wa-Cuba weusi waliopata mafunzo ya kijeshi Havana bila kuelewa kuwa walikuwa wanakwenda Congo. Uwepo wa Che Guevara jijini Dar April 1965 haukufahamika na wengi. Hata CIA hawakuelewa hilo. Hadi mwaka 1990 CIA waliamini kuwa Che Guevara aliingia Congo akitokea Congo Brazaville. Kwamba Che Guevara alikuwa Dar kwa juma moja na zaidi unadhihirisha ukweli wa simulizi kuwa Che Guevara alitembelea mgahawa wa Zahir ( Sasa New Zahir Restaurant) mtaa wa Msikiti na kuwa na mazoea ya kunywa chai na kula chakula mahala hapo. New Africa Hotel kulikuwa na mgahawa maarufu kule juu kabisa, lakini pale pangemfanya aonekane kirahisi hata na mawakala wa CIA. Che Guevara anamweleze Laurent Kabila ( Baba yake Joseph Kabila) kama mtu ambaye hakuwa makini katika kuendesha harakati za mapambano. Che anaandika kuwa Kabila alipenda sana pombe, hakuonekana kwenye uwanja wa mapambano, mara nyingi alituma ujumbe wa mdomo au maandishi kutoa maelekezo. Che alikwenda na kikosi chake Mashariki ya Kongo bila ya mwenyeji wake, Laurent Kabila. Laurent Kabila alikuwa na miaka 26 tu wakati huo. Kuhusu umri wa Kabila Che Gueavara anandika hivi; " Kabila is young, and it is possible that he will change. But I have very great doubts about his ability to overcome his defects in the environment in which he operates".
Reactions::

Futari Yangu Ya Magimbi Inanitosha!



Sahani shilingi elfu moja na mia tano. New Zahir Restaurant leo jioni.
Reactions::

Mambo Ya Pwani Haya!



Leo nilikwenda Bagamoyo kwa kazi ya saa kadhaa. Kabla ya kufunga safari ya kurudi Dar nilishuka pwani kwa matembezi mafupi ya kando ya bahari. Kamwe siwezi kwenda na kuondoka Bagamoyo bila kushuka pwani,kuiona bahari na kuyanawa maji ya bahari kama si kuogelea. Naam. Kuukanyaga mchanga wa pwani. Na pwani ina mambo mengi. Ili uyajue mambo ya pwani ni sharti utembee, utazame,utafakari ukiwa pwani.
Reactions::

Kiu Ya Kusoma!



Bagamoyo,leo Jumatano.
Reactions::

Nazi Mia Na Hamsini!


Bagamoyo leo mchana.
Reactions::

Soko Kuu Bagamoyo Leo Mchana

Reactions::

Leo Magazetini





Reactions::

Kurasa Za Ndani







Reactions::