Subscribe:

Saturday, October 31, 2009

Igoma, Ilemela, Isamilo, Buhongwa...



Mwanza ina vitongoji vingi na majina ya kuvutia, sijui yana maana gani, watani zangu mnisaidie.
Reactions::

Leo Ni Leo!



Simba tuko vizuri kwa sasa. Yanga presha iko juu. Natabiri tutaondoka na ushindi wa bao moja kwa bila! Watani mnasemaje? ( Pichani ni Nyamanolo, Mwanza)
Reactions::

Friday, October 30, 2009

" Mheshimiwa Sitakung'oa, Nitakupa Maelezo Tu!"



Mganga wa meno katika kliniki ya Meno kata ya Ilembo wilaya ya Mbeya vijijini Dr.Marietha Sanga akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mitambo mipya ya kuhudumia wagonjwa wa meno inavyofanyakazi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua kliniki hiyo jana. ( Picha: Freddy Maro)
Reactions::

" Haya, Nazindua!"




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi kliniki inayotembea(Mobile Health Lab) kwa ajili ya kutoa huduma za upimaji ukimwi na huduma nyinginezo za kimaabara katika uwanja wa Shule ya Msingi Ilembo, Mbeya vijijini.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya Dr.Inge Baumgarten na kulia ni afisa kutoka taasisi ya jeshi la Marekani ya Walter Reeed Army Institute Bwana Edward Sekonde.
Reactions::

Umati




Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Ilembo wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini.
Reactions::

" Hello Mr. President!"


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wafanyakazi wa kujitolea kutoka taasisi ya American Peace Corps Meesh Santoro(wapili kushoto) anayeishi kata ya Ilembo na Jenna Covey anayeishi Isangati Mbeya vijijini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwahutubia wakazi wa kata ya Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini jana mchana(Picha: Freddy Maro).
Reactions::

Kozi Ya Uandishi Wa Kiraia



Bado niko Mwanza, na siku nzima ya leo nashiriki kuendesha mafunzo ya uandishi wa kiraia. Ni kwa wadau wa habari wa Kanda ya Ziwa. Nami nina mengi ya kujifunza.
Reactions::

JK Kijijini Lufilyo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya wakishangalia wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo la taasisi hiyo iliyofanyika huko Lufilyo,Rungwe, mkoani Mbeya jana jioni.Taasisi ya Lucy Hope inawahudumia watoto Yatima kwa kuwalea na kuwapa elimu katika ngazi mbalimbali
Reactions::

" Zawadi Hii!"


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya na Mumewe Profesa Mark Mwandosya wakimkabidhi Rais Jakaya Kikwete picha iliyochorwa na Bi.Lucy Mwandosya inayoonesha ngoma ya utamaduni ya Rungwe wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la taasisi hiyo huko Lufilyo Rungwe jana jioni.
Reactions::

Lucy Hope Centre



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya pamoja na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya muda mfupi baada ya kuwahutubia wananchi wa Lufilyo,Rungwe wakati wa uwekaji jiwe la Msingi katika jengo la taasisi hiyo uliofanyika jana.Taasisi ya lucy Hope inawahudumia watoto Yatima.(Picha: Freddy Maro).
Reactions::

Emmanuel Na Jane


Emmanuel wa Sengerema Redio na Jane wa Mwananchi. http://www.mwananchi.co.tz
Reactions::

Test!


Byabato



Noeli xxx
Reactions::

Washiriki Darasani





Mwanza.
Reactions::

Mafunzo Yanaendelea!



Mafunzo yanaendelea!
Reactions::

Tunavyosafiri Ni Roho Mkononi!


Yakitokea tunasema; " Kazi ya Mungu" wakati kila mtu anaona kuwa chombo kimezidisha uzito! Pichani ni chombo kinachoiacha bandari ya Mwanza kwa wasafiri waendao Sengerema na Geita.
Reactions::

Nyamagana Stadium



Mwanza.
Reactions::

Kijiwe!


Mwanza Mjini, jana jioni.
Reactions::

Hii Ndio Mwanza!



Inapendeza!
Reactions::

Thursday, October 29, 2009

Msaada Wa Bajaji


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi usafiri aina ya Bajaji kwa mwanamke mlemavu Sara Mageni Sanga aliyekaa chini katika kijiji cha Lupalilo,Wilayani Makete,Mkoa wa Iringa jana jioni.Pembeni ya Rais kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bwana Mohamed Abdulaziz. ( Picha: Freddy Maro)
Reactions::

Mvuvi Naye Yumo Mashakani!




Jioni hii nilikuwa pale ziwani. Pichani hapo ni mvuvi anayejaribu kuwauza samaki wake aina ya sato wapatao 6. Ndio kwanza katoka kuwavua na bado wanapumua. Wote hao kwa shilingi elfu sita, lakini wateja hao pichani wanalilia aheri, kwamba bei ipungue!
Reactions::

KWANZA JAMII Linasomwa Mwanza!




Kwenye moja ya mitaa ya Jiji la Mwanza nilimkuta binti mrembo akilisoma KWANZA JAMII la juma hili.
Reactions::

Watani Zangu Hawasongi Ugali, Bali Matofali!



Kama kuna kitu kimewashinda watani zangu Wanyamwezi na Wasukuma, basi ni sanaa ya kusonga ugali. Ugali sharti uanze na kukorogea uji, sasa haya ya kuchemsha maji na kutia unga ni kama wafanyavyo watani zangu ndio hutoa matofali, ugali mgumu. Tukiacha utani, leo pale kando ya ziwa nilikula ugali mtamu wa Kinyamwezi ( wa dona) na samaki freshi aina ya nembe aliyevuliwa leo leo! Mwanza kuzuri!
Reactions::

Mwanza Imetulia!




Ni mji mzuri, lakini leo kuna joto kali kama la Dar. Nyuzi joto 29.
Reactions::

" Naam. Hawa Ndio Kondoo!"



Mmiliki wa Shamba la Mifugo lililopo eneo la Ifunda,Mkoa wa Iringa Bwana Mark Taylor akimwonesha Rais Jakaya Kikwete baadhi ya kondoo wa mfano wanaozalishwa katika shamba hilo leo asubuhi. ( Picha: Freddy Maro)
Reactions::

Uwanja Huu Simba Hatuna Hamu Nao!



Unanikumbusha usiku mmoja wa huzuni kuu miaka ile ya sabini pale watani zetu Yanga walipotufunga bao 2-1. Mechi ilichezwa usiku. Kulikuwa na Sunday Manara, Gibson Sembuli na Kitwana Manara. Hawa jamaa ndio waliotuzamisha! Tukiacha utani, naamini Yanga ile ilitisha.
Reactions::

Safari Ya Mwanza Nimeianzia Kipawa



Leo saa nne asubuhi. Abiria tulikuwa wengi tukapewa Boeing 737 badala ya ndege zile ndogo.
Reactions::

Wote Ni Watoto Wake!



Mwanza Mchana Huu.
Reactions::

Hivi Ngetwa Ni Nanihii Ya Nini?



Watani zangu Wasukuma na Wanyamwezi mnisaidie! Pichani ni Mwanza mchana huu.
Reactions::

Nimewasili Kwa Watani Wangu Mchana Huu!



Nikitokea Dar. Mwanza Mji mzuri, ni miaka mingi kidogo tangu niwe hapa kwa mara ya mwisho. Kuna mabadiliko, jiji linakua na yote yenye kuambatana nayo. Nimepata nafasi ya kukatisha mitaa ya jiji la Mwanza na vitongoji vyake, nimeongea na baadhi ya wenyeji wa jiji hili pia. Nitakuwa na mengi ya kusimulia hata kwa njia ya picha. Naam. Nimeshapiga picha kadhaa.
Reactions::

Kuna Wanaoishi Chini Ya Mibuyu!


Kuna Wanaoishi Chini Ya Mibuyu!
Pichani ni juzi asubuhi, nje kidogo ya kijiji cha Ruaha Mbuyuni, mpakani mwa Iringa na Morogoro upande wa Morogoro.
Reactions::

Wednesday, October 28, 2009

Mkulima Mashakani



Debe moja la vitunguu bei ya juzi ni shilingi elfu tatu. Mwaka jana kipindi kama hiki nilinunua debe la kitunguu kwa shilingi elfu saba. Wakulima niliongea nao wanasema huu ni mwaka wa hasara, maana gunia zima la vitunguu linauzwa kwa elfu ishirini.
Reactions::

Mikumi Hapa!


Jana asubuhi.
Reactions::

KWANZA JAMII MIKUMI!


KWANZA JAMII lilikuwa mitaani jana Jumanne.
Reactions::

Da' Subi

Naomba nafasi katika blogu yako kuwataarifu wasomaji kuwa tovuti ya mpya ya wavuti.com imechukua nafasi ya iliyokuwa nukta77.com na nukta77.blogspot.com
Naomba yeyote aliyekuwa ameweka linki ya nukta77 aihariri na kuweka wavuti.com

Karibuni sana kutembelea kwa taarifa za nafasi za masomo na kazi kwa burudani na bila kusahau habari na porojo!
Asanteni.
wavuti.com
Reactions::

Sitaweza Kuingiza Picha Kwa Siku Ya Leo

Kuna tatizo la kiufundi limejitokeza. Nalifanyia kazi.
Poleni kwa usumbufu.
Maggid
Reactions::

Tuesday, October 27, 2009

Nimewasili Kinondoni Biafra Mchana Huu

Nikitokea Iringa. Safari yangu niliianza leo alfajiri. Nina picha za njiani. Zitakuja!
Reactions::

Krismasi Imekaribia!




Iringa, jana mchana.
Reactions::

Monday, October 26, 2009

Agnes Na Sharifa



Agnes Andersson ( Kushoto). Mtangazaji mahiri wa redio ya Ebony FM ya hapa Iringa akiwa na mdogo wake aitwaye Sharifa. Pichani ni maeneo ya Uhindini, Iringa Mjini leo asubuhi.
Reactions::

Athuman Mwalubadu



Mtangazaji Ebony FM na mwigizaji. Ni msanii mahiri. Iringa, leo asubuhi.
Reactions::

Blandina Nyoni



Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bibi Nyoni hivi karibuni alitembelea Taasisi ya Moyo Tanzania.
Reactions::

" Vyandarua Hivi, Navikabidhi!"



Meneja Uhusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Ibrahim Msengi vyandarua pamoja na mashuka kwa ajili
ya wodi ya wazazi ya hospitali ya taifa ya Bombo. (Picha: Ahmed Michuzi)
Reactions::

JK Kutua Iringa Leo



Kwa ziara ya kikazi. Na jana usiku Tanesko wameturudishia umeme mapema, ama kweli, mgeni njoo, mwenyeji apone!
Reactions::

Sunday, October 25, 2009

" Haya, Nimekabidhi!"





Leo jioni hapa Iringa nilikabidhi vifaa vipya vya mchezo wa soka kwa kocha wa timu ya watoto ya G-Kids ya hapa Iringa. Ni pamoja na jezi mpya na kaptula za kutosha vikosi vitatu, mipira kumi na moja na viatu. Vyote vina thamani ya shilingi za Kitanza...nia milioni mbili na zaidi. Huu ni msaada kutoka klabu ya Degefors IF ya nchini Sweden ambayo juzi tu imepanda daraja na kuingia daraja la kwanza ( Super Ettan). Tumepata pia msaada wa vifaa vya michezo kutoka klabu ya Ostefarnebo IF ya daraja la nne nchini Sweden. Haya ni matokeo ya mahusiano mazuri tuliyoyaanzisha yapata miaka miwili iliyopita. Nikiwa kama Mwenyekiti wa klabu yetu ya G- Kids na kocha msaidizi, nawashukuru sana , kwa niaba ya wenzangu, rafiki zetu wa Sweden. Natoa pia changamoto kwa Watanzania mlio ughaibuni, jitahidini kujenga mahusiano na vilabu vya maeneo mnayokaa ili kwa namna moja au nyingine muweze kufanikisha mahusiano na vilabu vya hapa nyumbani. Kwa njia hii nasi huku nyumbani tunaweza kunufaika hata kwa kujifunza tu wenzetu wanavyojenga oganaizesheni yao ya michezo.
Reactions::